Wizara ya Elimu, Sayansi na
Teknolojia (WyEST) kwa kushirikiana na Benki ya Dunia, inafanya maandalizi ya
kutekeleza Mradi wa Kuboresha Elimu ya Juu kwa Mabadiliko ya
Kiuchumi (Higher Education for Economic
Transformation - HEET) Nchini. Lengo la Mradi ni kuongeza udahili katika
vyuo vikuu vya serikali, kuongeza ubora wa mafunzo ili kuendana na soko la
ajira kwenye programu za kipaumbele na kuboresha utendaji wa Serikali katika
kusimamia Elimu ya Juu nchini.
Utekelezaji wa Mradi utazingatia Miongozo
ya Usalama wa Mazingira na Jamii. Hivyo, WyEST imeandaa vikao vya wadau ambao ni:
Taasisi zitakazotekeleza Mradi wa HEET, Taasisi na wakala wa Serikali, Jumuiya
za wataaluma Taasisi za Elimu ya Juu, Jumuisha za Wanafunzi Taasisi za Elimu ya
Juu, Jumuiya za wanafunzi wenye mahitaji maalumu Taasisi za Elimu ya Juu, Asasi
zisizo za Serikali, Mashirika, Makampuni, watu binafsi na wadau wa maendeleo; kwa
ajili ya kupokea maoni ili kuboresha rasimu ya miongozo mitatu (3)
iliyoandaliwa. Miongozo hiyo ni Mwongozo wa Usimamizi wa Usalama wa Mazingira
na Jamii (Environmental and Social
Management Framework – ESMF), Mwongozo wa Uhamishaji wa Makazi na Watu (Resettlement Policy Framework - RPF) na
Mpango wa Ushirikishwaji wa Wadau (Stakeholders’
Engagement Plan –SEP).
Kwa kuzingatia
umuhimu wa miongozo hiyo, WyEST inawaalika wadau wote kutoa maoni kabla
miongozo hiyo haijapelekwa katika hatua nyingine. Mwisho wa kupoke maoni ni
tarehe 15 Januari 2020. Maoni ya wadau yanaweza kuwasilishwa kwa njia ya Posta
au Baruapepe kwa anuani ifuatayo: -
Katibu Mkuu,
Wizara ya Elimu, Sayansi na
Teknolojia,
S.L.P. 10,
DODOMA
Baruapepe: heet@moe.go.tz
Aione: Tabitha Etutu
Miongozo hiyo inapatikana kupitia tovuti ya WyEST www.moe.go.tz
Kwa maelezo zaidi
wasiliana na Tabitha Etutu kwa tabitha.etutu@moe.go.tz au Sakanda Gaima kwa sakanda.gaima@moe.go.tz.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
Zingatia: Mwanachama wa blogu hii tu ndiye anayeweza kuchapisha maoni.