Ijumaa, 12 Januari 2018
Jumatatu, 8 Januari 2018
Serikali kuimarisha Elimu Nje ya Mfumo Rasmi
Waziri
wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa. Joyce Ndalichako amesema Mkakati wa
Serikali ni kuimarisha Elimu Nje ya Mfumo Rasmi ili kuwapa nafasi watoto
wanaoshindwa kujiunga na Mfumo huo wa Elimu kuwa na fursa nyingine ya kupata
Elimu na Ujuzi ambao utawasaidia katika kulileea Taifa Maendeleo .
Kauli hiyo ameitoa leo jijini Dar es salaam katika ofisi ndogo za Wizara alipokutana na kufanya mazungumzo na balozi wa Uingereza Sarah Cooke, balozi wa Sweden katrina Rangnitt na balozi wa Canada Alexandre leveque wanaowakilisha nchi zao hapa nchini
Waziri Ndalichako amewaambia Mabalozi hao kuwa Elimu Nje ya Mfumo usio Rasmi ipo kwa ajili ya kuwasaidia wale walioshindwa kujiunga na Mfumo Rasmi wa Elimu, hivyo hata wale watakaopata ujauzito wanashauriwa kujiunga katika mfumo huo ili kuendelea na masomo yao mara baada ya kujifungua.
Profesa Ndalichako amesema lengo la serikali ni kuwapa fursa wanafunzi wanaokosa nafasi au wanaoacha shule kwa sababu mbalimbali waweze kupata Ujuzi na Elimu katika njia nyingine ikiwemo mafunzo ya ufundi katika Vyuo vya Ufundi Stadi na Vyuo vya Maendeleo ya Jamii mafunzo ambayo yatawawezesha kujiajiri ama kuajiriwa.
Akizungumzia Mkakati wa Serikali katika kupambana na changamoto za mtoto wa kike kupata elimu , Profesa Ndalichako alisema mpaka sasa serikali kupitia Programu ya lipa kulingana na Matokeo, EP4R imeshajenga zaidi ya mabweni 300 katika maeneo mbalimbali nchini hasa yale yaliyo katika mazingira magumu na kutoa wito kwa wafadhili mbalimbali kuunga mkono jitihada za Serikali kwa kuchangia ujenzi wa mabweni katika maeneo yenye mazingira magumu kwa ili kuwasaidia wanafunzi wawezekufanya vizuri katika masomo yao.
Akizungumza kwa niaba ya Mabalozi wengine Balozi wa Sweden nchini Tanzania Katarina Rangnitt amesema wamefurahishwa sana kusikia kutoka kwa Waziri kuwa watoto wanaopata mimba shuleni wanapata fursa nyingine ya kupata Elimu na ujuzi nje ya mfumo usio rasmi ambao utawasaidia katika kuendeleza maisha na kuewa Elimu ndiyo nguzo pekee katika kujieletea Maendeleo.
Kauli hiyo ameitoa leo jijini Dar es salaam katika ofisi ndogo za Wizara alipokutana na kufanya mazungumzo na balozi wa Uingereza Sarah Cooke, balozi wa Sweden katrina Rangnitt na balozi wa Canada Alexandre leveque wanaowakilisha nchi zao hapa nchini
Waziri Ndalichako amewaambia Mabalozi hao kuwa Elimu Nje ya Mfumo usio Rasmi ipo kwa ajili ya kuwasaidia wale walioshindwa kujiunga na Mfumo Rasmi wa Elimu, hivyo hata wale watakaopata ujauzito wanashauriwa kujiunga katika mfumo huo ili kuendelea na masomo yao mara baada ya kujifungua.
Profesa Ndalichako amesema lengo la serikali ni kuwapa fursa wanafunzi wanaokosa nafasi au wanaoacha shule kwa sababu mbalimbali waweze kupata Ujuzi na Elimu katika njia nyingine ikiwemo mafunzo ya ufundi katika Vyuo vya Ufundi Stadi na Vyuo vya Maendeleo ya Jamii mafunzo ambayo yatawawezesha kujiajiri ama kuajiriwa.
Akizungumzia Mkakati wa Serikali katika kupambana na changamoto za mtoto wa kike kupata elimu , Profesa Ndalichako alisema mpaka sasa serikali kupitia Programu ya lipa kulingana na Matokeo, EP4R imeshajenga zaidi ya mabweni 300 katika maeneo mbalimbali nchini hasa yale yaliyo katika mazingira magumu na kutoa wito kwa wafadhili mbalimbali kuunga mkono jitihada za Serikali kwa kuchangia ujenzi wa mabweni katika maeneo yenye mazingira magumu kwa ili kuwasaidia wanafunzi wawezekufanya vizuri katika masomo yao.
Akizungumza kwa niaba ya Mabalozi wengine Balozi wa Sweden nchini Tanzania Katarina Rangnitt amesema wamefurahishwa sana kusikia kutoka kwa Waziri kuwa watoto wanaopata mimba shuleni wanapata fursa nyingine ya kupata Elimu na ujuzi nje ya mfumo usio rasmi ambao utawasaidia katika kuendeleza maisha na kuewa Elimu ndiyo nguzo pekee katika kujieletea Maendeleo.
Jumamosi, 6 Januari 2018
JAMHURI YA
MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA
ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA
|
Anwani
ya Simu: “ELIMU”
DAR
ES SALAAM
Simu:
0262963533,
Tovuti:www.moe.go.tz
|
Chuo cha Masomo ya Biashara na Sheria,
Chuo Kikuu cha Dodoma
S. L. P. 10
40479 DODOMA
|
TAARIFA KWA UMMA
Ndugu
Wanahabari,
Kama
ambavyo wengi wenu wanafahamu, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia inaendelea
na programu yake ya ukarabati mkubwa wa shule kongwe za Sekondari nchini. Programu
ambayo itahusisha jumla ya shule kongwe 89. Katika awamu hii ya kwanza ambayo
imetekelezwa kwa miaka miwili sasa, yaani mwaka wa fedha 2016/17 na 2017/18,
jumla ya shule 46 kati ya 89 zipo kwenye mpango wa ukarabati huu. Taarifa ya
programu hii ya ukarabati ni kama ifuatavyo:
- Shule 10 za sekondari ambazo ni Mpwapwa, Musoma Ufundi, Mtwara Ufundi, Ifakara, Kantalamba, Tanga Ufundi, Ifunda Ufundi, Moshi Ufundi, Bwiru Wavulana na Kibiti zinaendelea kukarabatiwa kwa usimamizi wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Mbeya (MUST). MUST ni taasisi ya kielimu, kwa hiyo wamekuwa makini sana na ratiba za shule. Shule zote hizi ziko katika hatua za mwisho za ukarabati na wanafunzi wanaendelea na masomo kama kawaida;
- Shule za Sekondari za Iyunga, Chidya, Tambaza, Zanaki na Kisutu zinakarabatiwa chini ya Uongozi wa Shule na Bodi za Shule kwa usimamizi wa Halmashauri za Wilaya zao. Nazo pia ukarabati unaendelea vizuri sana.
- Shule ya sekondari ya Ndwika ambayo iko Wilaya ya Masasi, inajengwa upya chini ya Halmashauri baada ya taarifa ya wahandisi kubaini kuwa majengo yake hayawezi kufanyiwa ukarabati.
- Shule za Sekondari za Nyakato na Ihungo nazo pia zinajengwa upya kufuatia kuharibiwa vibaya na tetemeko la ardhi lililotokea katika Mkoa wa Kagera mwezi Septemba, 2016. Na kwa upande wa Shule ya Sekondari ya Rugambwa, hii inajengewa nyumba 8 za walimu ambazo zilibomoka kutokana na tetemeko hilo;
- Vilevile Wizara kupitia Mamlaka ya Elimu Tanzania inakarabati Shule za Sekondari 17 ambazo ni : Ilboru, Same, Pugu, Mwenge, Nganza, Mzumbe, Kilakala, Tabora Wavulana, Tabora Wasichana, Msalato, Dodoma, Ruvu, Korogwe, Bwiru Wasichana, Sengerema, Bihawana na Kondoa Wasichana. Katika ya hizi mpaka sasa shule 10 zimeshakamilika na saba zitaanza kukarabatiwa hivi karibuni bila kuathiri masomo.
- Shule za Sekondari 9 ambazo ni Jangwani, Azania, Kibaha, Kigoma, Tosamaganga, Malangali, Milambo, Minaki na Nangwa zinaendelea kukarabatiwa chini ya usimamizi wa Wakala wa Majengo Tanzania – TBA ambazo zipo kwenye hatua mbalimbali za ukarabati, ambapo shule ya Songea Wasichana bado haijaanza kukarabatiwa.
- Ndugu Wanahabari kama mnavyotambua shule zetu zinafunguliwa kesho kutwa tarehe 8 Januari.
- Wizara baada ya kufanya tathmini ya kina imegundua kuwa kwenye shule zinazokarabatiwa na TBA kumekuwa na tatizo la ukamilishwaji wa miradi katika muda uliopangwa. Miradi yote iko nyuma ya ratiba. Na mbaya zaidi ni kwamba baadhi ya shule haziko tayari kabisa kupokea wanafunzi na wakaendelea na masomo yao kwa ukamilifu. Yaani mazingira ya ufundishaji na ujifunzaji hayajakamilika.
- Hivyo basi baada ya mashauriano na wenzetu wa Ofisi ya Rais TAMISEMI tumekubaliana kuhairisha kuanza kwa muhula wa kwanza kwa shule za Milambo, Jangwani na Azania.
- Kwa shule hizi muhula wa kwanza utaanza tarehe 22 Januari 2018.
- Ratiba za masomo katika shule hizi itarekebishwa ili wiki hizi mbili ziweze kufidiwa. Utaratibu wa kawaida ni kufidia muda huu wakati wa likizo fupi na likizo ndefu ya mwezi ya mwezi Julai.
Wizara
kwa kushirikiana na Serikali za Mikoa na Halmashauri husika itafanya usimamizi
wa karibu kuhakikisha kuwa shule hizi zinakamilika katika kipindi hiki cha wiki
mbili.
Tunaomba
radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza kwa wazazi/walezi na wanafunzi
wanaosoma na waliochaguliwa kujiunga katika kidato cha kwanza katika shule hizi.
Natumaini mnatambua nia njema ya Serikali ya kutaka kuimarisha mazingira ya
shule hizi ambazo zilikuwa zimechakaa sana.
Nachukua
fursa hii pia kuwaagiza Wakala wa Majengo, TBA, kutekeleza majukumu yao
kulingana Mikataba tuliyoingia nao. Pamoja na shule hizi Kongwe pia tumewapa
kazi za ujenzi wa Kampasi ya MUHAS-Mloganzila. Matarajio yetu ni kwamba Kampasi
hii itachukua wanafunzi wa kwanza mwaka huu. Nawaagiza TBA kuongeza juhudi pale
Mloganzila ili lengo hili likamilike.
Maelekezo
ya Waziri wangu Mhe. Prof. Ndalichako ni kuhakikisha kuwa tunafanya usimamizi
wa karibu ili miradi yote ya TBA ianze kwenda kulingana na Mikataba. Tutafanya
hivyo wakati pia tunaangalia taratibu za kisheria ili kama kuna hatua zozote
muafaka ziweze kuchukuliwa ili malengo yakamilike kulingana na matarajio.
Ninawashukuru
sana.
Dkt. Leonard D. Akwilapo
KATIBU
MKUU
06 Januari 2018
Ijumaa, 5 Januari 2018
SADC ESSAY WRITING COMPETITION FOR SECONDARY SCHOOLS, 2018
The Southern African Development Community (SADC) Secretariat has
organized the SADC students essay writing competition for year 2018. The Essay
writing competition is intended to broaden knowledge of the secondary school
going population on SADC activities. The competition is open to form 1 to 6
students. The students are required to begin researching on the topic prior to writing
and submitting to their Heads of School.
The 37th summit of Heads of State and Governments deliberated
that, the topic for year 2018 is “Partnering with the private sector in
developing Industries and Regional Value Chains”.
The topic for the essay competition is “Discuss how partnership
with private sector can promote industrial growth and foster development of
value chains in key priority sectors (such as agriculture, mining, health etc)
among SADC member states”.
The set of questions below are meant to guide students when
responding to the question above. Thus, on answering the above question,
student should answer all the questions listed below:
1. Discuss
in-depth, what you understand about industrial growth and value chains and how
SADC Member States could increase private sector involvement in industrial
growth and value chains. (20 Points)
2. Discuss
and fully explain the general forms of value added services which are
undertaken in the SADC region. (15 Points)
3. Collaboration
between governments and the private sectors is said to be key in developing
economies, explain your understanding of the term private sector engagement and
how it is key in developing industrial growth and value chains and give at
least four (4) examples of major business collaborative efforts that has made
huge impact in development region economy. (20 Points)
4. For
SADC Region to achieve any meaningful industrialization in form of industrial
growth and improvement in value chains, discuss the areas/ types of value added
services which are likely to produce meaningful; results in the present
context. (15 Points)
5. Presently
how do SADC member states engage the private sector in the development of their
industries, and in your opinion, how can these relationships be strengthened.
(15 Points)
6. What
interventions and/or measures should regional governments embark on in order
for private sector be key drivers of national economies. (15 Points)
Heads of schools are supposed to ensure that students adhere to
the following guidelines:
i. The
essay should not be longer than 1,500 words and not shorter than 1,000 words;
ii. Where
students have access to computers, they are advised to type their essays and
submit both the soft and hard copies;
iii. Students
who will type their essays will have to sign and initial the hard copies to
make sure that they have not been altered;
iv. The essay shall be
written in English language;
v. The
front page or cover page will display the name, sex, class, school address and
stamp, Headmistress/Headmaster’s email address, signature and phone no, region,
country;
vi.
The title of the essay should be written on the cover page (students should not
paraphrase the title);
vii. Definition
of Key concepts and a brief Historical/Background of SADC should be written in
the introductory paragraph;
viii. All reference
material must be written in the last page; and
ix. The
handwritten essays will be written on one side of the A4 paper with double
margin of two centimeters.
Students are expected to begin writing immediately and submit
their essays to their head of schools. The Head of School will then be expected
to constitute a marking panel which will choose best essays of the school. The
panel should go through the essays (Please do not mark the essays) and choose
three essays to be submitted to The Permanent Secretary; Ministry of Education,
Science and Technology, P.O. Box 10, Block 10, College of Humanities Dodoma not
later than 15th April 2018. The national adjudication will take place from 02nd
to 15th May 2018 in order to get three entries which will be submitted to the
SADC Secretariat in Botswana.
Thank you for your cooperation.
Dr. Leonard D. Akwilapo
PERMANENT SECRETARY
5/1/2018
Ndalichako: sijaridhishwa na kasi ya ujenzi Kigoma Sekondari, TBA wachukuliwa hatua
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce
Ndalichako amesema hajaridhishwa na kasi ya ujenzi wa shule ya Sekondari Kigoma
ilihali wakala wa Majengo wanaojenga shule hiyo walishapatiwa
fedha za awali kwa ajili ya ujenzi wa shule hiyo kiasI cha asilimia
30 na kuwa malipo ya fedha hizo yalishafanyika tangu mwezi machi mwaka Jana.
Waziri Ndalichako amesema shule ya sekondari Kigoma ni miongoni
mwa Shule Kongwe na tayari Serikali imekwishatoa fedha za kutosha
ambapo ukarabati wa shule ulitarajiwa kukamilika mapema Mwezi
Septemba, 2017 ili shule zitakapofunguliwa Januari 8,
2018 ukarabati uwe umekamilika na wanafunzi waweze kutumia miundombinu hiyo.
Waziri Ndalichako ametoa kauli hiyo akiwa mkoani Kigoma kwenye
ziara ya kikazi ya kukagua ujenzi na ukarabati wa shule mbalimbali
unaotekelezwa na Wizara yake kupitia Programu maalumu ya Lipa kulingana na
matokeo.
Kufuatia kusuasusa kwa ukarabati wa shule hiyo ya sekondari
Kigoma, Mkuu wa mkoa wa kigoma Brigadia Jenerali mstaafu Emmanuel
Magaga ameamuru kukamatwa na kuwekwa ndani kwa meneja wa Wakala wa
majengo wa TBA wa mkoa wa Kigoma Mgala Mashaka ili uchunguzi
ufanyike dhidi yake kutokana na kutuhumiwa kujihusisha na miradi binafsi,
pamoja na kuhusishwa na vitendo vya rushwa.
Akiwa mkoani Kigoma Waziri Ndalichako pia alikagua vifaa vya
maabara ambavyo tayari vimepokelewa kwenye shule mbalimbali za sekondari.
Alhamisi, 28 Desemba 2017
Waziri Ndalichako afungua vyumba vya madarasa Simiyu
Waziri wa Elimu, Sayansi na
Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako
amesema serikali itaendelea kuboresha miundombinu ya kujifunzia na ile ya
kufundishia lengo likiwa ni kuhakikisha Elimu bora inatolewa.
Waziri Ndalichako ameyasema
hayo wakati akifungua vyumba viwili vya madarasa vilivyojengwa kupitia Mradi wa
Lipa Kulingana na Matokeo (P4R) katika
Shule ya Msingi Mahembe iliyopo Kijiji cha Mahembe kata ya Sawida mkoani Simiyu
Kupitia ziara hiyo Profesa Ndalichako pia alizungumza na
wananchi wa Kijiji cha Habiya kilichopo
Wilaya ya Itilima na kuwataka wazazi kuhakikisha watoto wote waliofika umri
wa kwenda shule wanakwenda.
Kwa upande wake Mbunge wa
Jimbo la Itilima, Mkoani Simiyu Njalu Silanga amepongeza jitihada zinazofanywa
na Serikali za kuboresha miundombinu huku akiwataka wananchi wa Jimbo lake
kuitunza miundombinu hiyo kwa faida ya kijiji
hicho.
Alhamisi, 21 Desemba 2017
Jisajili kwenye:
Maoni (Atom)









