Serikali imezindua Mfuko wa Kuendeleza Ujuzi (SDF)
utakaowezesha watoa huduma za mafunzo ya ufundi katika ngazi mbalimbali kutoa
mafunzo yenye tija yatakayoweza kukuza stadi za kazi.
Akizindua
Mfuko huo Jijini Dar es Salaam Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof.
Joyce Ndalichako amesema mfuko huo unalenga kuboresha stadi za kazi, uwezo wa
kujiajiri na kuchangia ongezeko la wataalam
wenye stadi mbalimbali katika taaluma za Kilimo, Utalii, Nishati, Ujenzi,
Uchukuzi na TEHAMA.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce
Ndalichako akizungumza na wadau wa Elimu (hawapo pichani) waliohudhuria
uzinduzi wa Mfuko wa Kuendeleza Ujuzi (SDF) Jijini Dar es Salaam utakaowezesha
watoa huduma za mafunzo ya ufundi katika ngazi mbalimbali kutoa mafunzo yenye
tija yatakayoweza kukuza stadi za kazi uliofanyika.
Prof. Ndalichako amesema katika kuleta
ufanisi wa kukuza ujuzi Wizara yake itaanzisha kwa mara ya kwanza Baraza la
Taifa la Ujuzi (National Skills Council – NSC) ambalo litasimamia mabaraza ya
kisekta ya kukuza ujuzi (Sectoral Skills Council).
“Tayari Wizara ina makubaliano rasmi ya
ushirikiano (MoU) na Tanzania Private Sector Foundation (TPSF) itakayosaidia
uanzishwaji wa mabaraza hayo na Baraza
la Taifa la Ujuzi (NSC) litakuwa waangalizi wa mfuko huu wa SDF tunaouzindua
leo, hivyo sekta binafsi itakuwa na fursa ya kutoa mchango wake katika ukuzaji
ujuzi hapa nchini. “alisisitiza Prof. Ndalichako
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dk.
Leonard Akwilapo akizungumza na washiriki wa uzinduzi wa Mfuko wa Kuendeleza
Ujuzi (SDF) uliofanyika jijini Dar es Salaam ambapo amewataka wote watakaopata
fedha za Mfuko huo kuzitumia kwa malengo yaliyowekwa.
Naye
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) Dk. Erasmus Kipesha amesema Taasisi
yake ina jukumu la kuusimamia Mfuko huo na imedhamiria kuhakikisha kuwa
rasilimali zilizoelekezwa katika Mfuko huo zinatumika kwa weledi, taratibu,
haki, ubora, na ufanisi wa hali ya juu.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce
Ndalichako akimkabidhi Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania Dk. Erasmus
Kipesha mfano wa hundi kwa ajili ya Taasisi za Elimu ya Ufundi zitakazoshiriki
katika kukuza na kuendeleza ujuzi. Makabidhiano hayo yamefanyika wakati wa uzinduzi
wa Mfuko wa Kuendeleza Ujuzi (SDF) uliofanyika Jijini Dar es Salaam.