Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Dkt John Magufuli leo ameweka jiwe la msingi kwa ajili ya
upanuzi wa Chuo Cha Ualimu Murutunguru, kilichopo Wilayani Ukerewe mkoani
Mwanza.
Rais Magufuli amesema Chuo Cha
Murutunguru kwa sasa walimu wanaohitimu ni ngazi ya cheti, lengo la serikali ni
kianze kutoa ngazi ya Diploma na baadae kikiongezewa miundombinu kiweze kutoa
shahada.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dk. John Pombe Magufuli akiweka Jiwe la
Msingi katika Chuo cha Ualimu Murutunguru Wilayani Ukerewe mkoani Mwanza ambapo
amewapongeza Viongozi wa Wizara
ya Elimu kwa kusimamia vizuri miradi inayotekelezwa na Wizara hiyo.
Rais Magfuli pia amewapongeza
Viongozi wa Wizara ya Elimu kwa kusimamia vizuri miradi inayotekelezwa na
Wizara hiyo.
Pia Rais amewashukuru
washirika wa Maendeleo hususan nchi ya Uingereza kwa kuendelea kufadhili miradi
ya Elimu.
Baadhi
ya Watumishi wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia wakishuhudia uwekaji wa
jiwe la Msingi kwa ajili ya upanuzi wa Chuo cha Ualimu Murutunguru kilichopo
Wilaya ya Ukerewe Mkoani Mwanza.
Upanuzi wa ujenzi wa Chuo hicho
unahusisha jengo la Utawala, vyumba vya madarasa, bwalo la Chakula, hosteli za
wanafunzi, jengo maalumu la kupokelea umeme na ujenzi wa mifumo ya Maji na
umeme.
Muda
mfupi baada ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako
kumpokea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dk. John Pombe Magufuli
kwa ajili ya kuweka Jiwe la Msingi la upanuzi wa Chuo cha Ualimu Murutunguru.
Ujenzi huo utagharimu takriban
bilioni mbili nukta Tatu na inatarajia kukamilika oktoba mwaka huu.
Muonekano
wa vyumba vya madarasa katika Chuo cha Ualimu Murutunguru, ambapo leo Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dk. John Pombe Magufuli ameweka jiwe la
msingi ambalo linahusisha ujenzi wa Jengo la utawala, bwalo la chakula, hosteli
za wanafunzi, jengo maalum la kupokelea umeme na ujenzi wa mifumo ya maji na umeme.