Waziri
wa Elimu Sayansi na Teknolojia Profesa , Joyce Ndalichako amesema serikali iko tayari kuendelea kutoa
ushirikiano katika Taasisi binafsi ambazo zimeendelea kutoa mchango mkubwa
katika sekta ya Elimu hapa nchini.
Waziri
Ndalichako amesema hayo mkoani Dodoma wakati akizindua jengo la shule ya Msingi
Misercodia inayomilikiwa na kanisa katoliki Shirika la Watawa wa Misericordia.
Waziri wa Elimu,
Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako wkiwa na Waziri Mkuu Mstaafu
Mizengo Pinda wakati wa uzinduzi wa
Jengo la Shule ya Msingi Misercordia Mkoani Dodoma
Waziri
Ndalichako amesema Serikali imekuwa ikitambua na kuheshimu kazi kubwa
inayofanywa na kanisa hilo katika kusaidia ujenzi wa miundombinu kwenye sekta
ya Afya na Elimu hapa nchini na ikiwa ni pamoja na kutatua changamoto mbalimbali kwa wakati.
"Wakati
nakuja kuzindua shule hii nilimtaarifu
Mheshimiwa Rais Dkt. John Magufuli na ametuma salamu, amesema niwaambie
anawashukuru sana Maaskofu na Watawa kwa kuwa
mnaunga mkono juhudi za Serikali katika
ushiriki wa miradi mbalimbali ya maendelea kwa vitendo,”amesema Waziri
Ndalichako.
Waziri akiwa aa
Watawa wakati wa kuzindua Shule ya Kanisa ya Misercordia iliyopo Mkoani Dodoma
ambapo Serikali imesema iko tayari kushirikiana na Taasisi Binafsi katika maendeleo.
Waziri
huyo wa Elimu amesema , ujenzi wa Miundombinu hiyo umekuja wakati muafaka
ambapo uhitaji wa shule za mchepuo wa kingereza ni mkubwa , kutokana na
watumishi wengi wa serikali kuhamia Dodoma na hivyo kuhitaji shule kwa ajili ya
watoto wao.
Kuhusu
malezi ya wazazi, Waziri amesema hivi sasa wazazi wamesahau majukumu yao na
badala yake wamekuwa wakifanya kazi zote ambazo zilipaswa kufanywa na watoto
jambo ambalo sio sawa kwani wanajenga taifa la wavivu.
Wanafunzi na Walimu wa
Shule hiyo ya Misercordia wakati wa uzinduzi wa Jengo la gorofa katika shule hiyo.
Waziri
Ndalichako pia amezipongeza shule
nyingine za dini kwa kusimamia maadili kwa wanafunzi, ambapo
ametumia nafasi hiyo kuwakaribisha wawekezaji
kuja kuwekeza kwa kujenga miundombinu ya shule za msingi na sekondari kwani
hivi sasa Dodoma inauhitaji mkubwa wa shule kwa sasa.
Waziri
Ndalichako ameipongeza shule kwa kufanya vizuri katika matokeo ya kidato Cha
Nne na Sita na kuongoza kitaifa katika somo la kiingereza, pia amezipongeza
shule nyingine za dini kwa kusimamia maadili kwa wanafunzi.
Uzinduzi Jengo
la Shule ya Misercordia, iliyopo Mkoani
Dodoma uzinduzi huo umefanywa na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknlojia Prof.
Joyce Ndalichako ambapo Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda pia alishiriki
shughuli hiyo.