Wizara ya Elimu, Sayansi na
Teknlojia leo imewajengea uwezo Wabunge wa Kamati ya Bunge ya Huduma na Maendeleo
ya Jamii kwa kuwasilisha majukumu 14 yanayotekelezwa na Wizara hiyo
kwa mujibu wa hati idhini iliyotolewa April 22, 2016.
Akiwasilisha majukumu hayo Kaimu
Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango Makuru Petro ametaja majukumu hayo kuwa
ni pamoja na kutunga na kutekeleza Sera za Elimu, utafiti, Huduma za Maktaba,
Sayansi na Teknolojia na uendelezaji wa mafunzo ya Ufundi, kuendeleza Elimu kwa
kutoa ithibati ya mafunzo ya Ualimu na Maendeleo ya kitaalamu ya Walimu,
Kusimamia uendelezaji wa mafunzo katika vyuo vya Maendeleo ya wananchi, na
kusimamia mfumo wa tuzo wa Taifa.
Katibu
Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Leonard Akwilapo akifafanua
jambo kuhusu majukumu yanayotekelezwa na Wizara hiyo wakati wa kikao cha pamoja
na Kamati ya Bunge
ya Huduma na Maendeleo ya Jamii mkoani Dodoma.
Majukumu mengine ni kuainisha
mahitaji ya nchi katika ujuzi, kuweka viwango vya Taaluma ya Ualimu ikiwemo
kuanzisha bodi ya kitaalamu ya walimu, kusimami ithibati na uthibiti ubora wa
shule kwa kuweka viwango, kusimamia Huduma za machapisho ya kielimu ikiwemo
mitaala na vitabu, kuimarisha utumiaji wa Sayansi, Teknolojia na hisabati,
kuendeleza wataalamu wa ndani katika Sayansi na Teknolojia, kuratibu na
kusimamia utafiti, ubunifu katika fani za Sayansi na Teknolojia, kusimamia Tume
ya Taifa ya UNESCO, uendelezaji wa Rasilimali watu na kuratibu shughuli za
Idara, mashirika, wakala, programu na miradi iliyo chini ya Wizara.
Mkurugenzi
Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) Dkt. Aneth Komba akiwasilisha
utekelezaji wa majukumu ya Taasisi hiyo wakati wa kikao na Kamati ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii wakati wa kikao
cha pamoja kilichofanyika mkoani Dodoma.
Kupitia uwasilishaji wa majukumu
hayo ya Wizara wakuu wa Taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo walipata fursa ya
kujibu maswali mbalimbali yaliyoulizwa na Wabunge kwa lengo la kupata uelewa.
Baadhi ya Wakuu wa Taasisi zilizo chini
ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia wakishiriki kikao cha pamoja na
Kamati ya Bunge ya
Huduma na Maendeleo ya Jamii kilichofanyika mkoani Dodoma
Taasisi zilizoshiriki katika
kujibu maswali mbalimbali ya Wabunge ni pamoja na Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi
wa Elimu ya Juu, Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi, (NACTE), Tume ya vyuo
Vikuu Tanzania, (TCU), Taaaisi ya Elimu Tanzania (TET).
1.
Baadhi
ya Watendaji wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia wakishiriki kikao cha
pamoja na Kamati ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii kilichofanyika mkoani
Dodoma