Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya
Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa James Mdoe ameongoza ujumbe wa
Tanzania kwenye mkutano Mkuu wa 62 wa kimataifa wa kuendeleza matumizi salama
ya nguvu za nyuklia unaofanyika mjini Vienna nchini Austria.
Akizungumza katika mkutano huo
mjini Vienna Profesa Mdoe ameishukuru IAEA kwa kuisaidia nchi ya
Tanzania mashine ya kuchunguza na kutibu saratani ambayo inatumika katika
hospitali ya Bugando iliyopo mkoani Mwanza na misaada ya kiufundi katika
hospitali ya Saratani ya Ocean Road iliyopo jijini Dar es salama pamoja na misaada
ya kuwasomesha wataalam kwenye eneo la Teknolojia ya nguvu za
nyuklia.
Naibu Katibu
Mkuu Profesa James Mdoe akizungumza katika mkutano wa kimataifa unaofanyika
mjini Vienna, nchini Austria kuhusu matumizi salama ya nyuklia.
Profesa Mdoe pia amekieleza kikao
hicho cha kimataifa kuwa nchi ya Tanzania iko tayari kushirikiana na
IAEA katika kuendeleza matumizi salama ya nguvu ya nyuklia.
Balozi wa kudumu kwenye Mashirika
ya Umoja wa Mataifa mjini Geneva nchini Uswis James Msekele naye anashiriki
mkutano huo.
Mkutano huo ulioanza Septemba 17
utahitimishwa Septemba 21, 2018 huko mjini Vienna nchini Austria.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
Zingatia: Mwanachama wa blogu hii tu ndiye anayeweza kuchapisha maoni.