Jumatano, 28 Novemba 2018
Jumanne, 27 Novemba 2018
RAIS MAGUFULI AZINDUA MAKTBA YA KISASA KATIKA UKANDA WA AFRIKA MASHARIKI.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli leo amezindua
Maktaba ya kisasa kwa ukanda wa Afrika Mashariki iliyopo katika Chuo Kikuu Cha
Dar es Salaam (UDSM) iliyojengwa kwa thamani ya dola milioni 41 Sawa na fedha
za Kitanzania shilingi bilioni 90.
Akizungumza jijini Dar es salam wakati wa hafla ya kuzindua Maktaba hiyo
iliyojengwa kwa msaada wa Serikali ya China Rais Magufuli amempongeza
mkandarasi alyojenga Maktaba hiyo kwa kukamilisha mradi kwa wakati na kwa
kiwango Cha juu.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Magufuli akizindua jengo la Maktaba ya kisasa katika Chuo kikuu cha Dar es salaam ambapo Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako na balozi wa China nchini Tanzania Dkt. Wang Ke walishiriki uzinduzi huo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Magufuli akizindua jengo la Maktaba ya kisasa katika Chuo kikuu cha Dar es salaam ambapo Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako na balozi wa China nchini Tanzania Dkt. Wang Ke walishiriki uzinduzi huo.
Rais Magufuli pia ameishukuru serikali ya China kwa kuwa marafiki wa kweli kwa
nchi ya Tanzania Kwa kutoa msaada wa ujenzi wa maktaba hiyo pamoja na
misaada mingine ya Maendeleo bila masharti yeyote.
“Tutaendelea kuenzi mahusiano mazuri yaliyoanzishwa na waasisi wa serikali hizi mbili ambazo ni Tanzania na China, na kuwa kuwepo kwa mahusiano kumekuwa na tija katika Kujiletea Maendeleo na kuwa misaada imekuwa ikitokewa bila masharti yoyote,” alisema Rais Magufuli.
Rais Magufuli katika hotuba yake amekitaka Chuo Kikuu kuendelea kusimamia maadili, heshima ya Chuo kikuu na kuhakikisha Elimu inayotolewa ni ya viwango ili kulinda hadhi ya Chuo hicho.

“Tutaendelea kuenzi mahusiano mazuri yaliyoanzishwa na waasisi wa serikali hizi mbili ambazo ni Tanzania na China, na kuwa kuwepo kwa mahusiano kumekuwa na tija katika Kujiletea Maendeleo na kuwa misaada imekuwa ikitokewa bila masharti yoyote,” alisema Rais Magufuli.
Rais Magufuli katika hotuba yake amekitaka Chuo Kikuu kuendelea kusimamia maadili, heshima ya Chuo kikuu na kuhakikisha Elimu inayotolewa ni ya viwango ili kulinda hadhi ya Chuo hicho.
Rais John Magufuli
akikabidhiwa mfano wa ufunguo na balozi wa China nchini Tanzania Dkt. Wang Ke
kwa ajili ya kufungulia maktaba ya kisasa ambayo amezindua leo katika Chuo
kikuu cha Dar es salaam, jijini Dar es salaam.
Rais Magufuli pia amewataka wanafunzi wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam na
wale wa nje ya Chuo kuhakikisha wanaitunza maktaba hiyo ili idumu na iweze
kutumiwa na vizazi vijavyo.
Akizungumza katika uzinduzi huo Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako amezitaka Taasisi za Elimu ya Juu kuacha kutumika kama vichaka vya kuvunja sheria na kufanya ubadhirifu wa fedha za Umma.
“Tunazitaka Taasisi zote za Elimu ya Juu kuhakikisha zinakuwa ni mfano wa kuigwa na siyo kuwa mstari wa mbele katika kushiriki vitendo vya ubadhirifu, na kuwa watumishi wa Taasisi hizo ni watumishi wa Umma na kama walivyo watumishi wengine na kuwa yeyeote atakyekwenda kinyume Sheria itachukua Mkondo wake,” alisisitiza Waziri Ndalichako.
Akizungumza katika uzinduzi huo Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako amezitaka Taasisi za Elimu ya Juu kuacha kutumika kama vichaka vya kuvunja sheria na kufanya ubadhirifu wa fedha za Umma.
“Tunazitaka Taasisi zote za Elimu ya Juu kuhakikisha zinakuwa ni mfano wa kuigwa na siyo kuwa mstari wa mbele katika kushiriki vitendo vya ubadhirifu, na kuwa watumishi wa Taasisi hizo ni watumishi wa Umma na kama walivyo watumishi wengine na kuwa yeyeote atakyekwenda kinyume Sheria itachukua Mkondo wake,” alisisitiza Waziri Ndalichako.
Viongozi waandamizi wa
Serikali kutoka Wizara na Taasisi mbalimbali za serikali wakifuatilia uzinduzi
wa maktaba ya Kisasa ya UDSM jijini Dar es salaam, maktaba hiyo imejengwa kwa
msaada wa Serikali ya china kwa gharama ya shilingi bilioni 90.
Naye Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu hicho Prof. William Anangisye amesema Maktaba ni
chombo muhimu katika kujiendeleza na kuwa maktaba hiyo ya kisasa itatumiwa na
wafunzi pamoja na watafiti mbalimbali katika kujiongezea maarifa.
Rais John Magufuli akimshukuru balozi wa China nchini Tanzania Dkt. Wang Ke kwa kufanikisha ujenzi wa maktaba ya kisasa iliyojengwa katika Chuo kikuu cha Dar es salaam
Jumatatu, 26 Novemba 2018
TANZANIA NA CHINA ZATILIANA SAINI KUANZA UJENZI WA CHUO CHA VETA KAGERA
Serikali
ya Tanzania na ile ya Jamuhuri ya watu wa China leo zimetiliana saini makubaliano ya kuanza kwa ujenzi wa Chuo
cha Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) ambacho kinatarajiwa kujengwa
mkoani Kagera na kuwa ujenzi huo unatarajiwa
kukamilika mwaka 2020
Katibu
Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Leornald Akwilapo ndiye
aliyesaini mkataba huo kwa niaba ya Serikali ya Tanzania na kwa upande wa China mkataba huo umesainiwa na Mwakilishi
wa Uchumi na Biashara nchini Tanzania Yuan Lin na kuwa tukio hilo limefanyikia
jijini Dar es salaam.
Katibu
Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dk. Leornald Akwilapo pamoja na Mwakilishi
wa Uchumi na Biashara nchini Tanzania Yuan Lin wakitia saini mkataba wa makubaliano wa ujenzi wa chuo cha
VETA kinachotarajiwa kujengwa mkoani Kagera na ujenzi wake unatarajiwa kukamilika mwaka 2020.
Mara
baada ya kusaini mkataba huo Dkt. Akwilapo amesema kuwa Chuo hicho kitakuwa na
uwezo wa kuchukua wanafunzi 400 wa kozi za muda mrefu na wanafunzi 1000 wa kozi za muda.
Miundombinu
itakayojengwa katika chuo hicho ni pamoja na vyumba vya madarasa, Karakana za
Kufundishia, Majengo ya Utawala, mabweni
na Viwanja vya michezo na kuwa mpaka kukamilika kitagharimu zaidi ya
shilingi bilioni 22.
Dkt. Akwilapo amewataka wakandarasi wanaopewa mikataba ya ujenzi na Wizara yake
kuhakikisha wanatekeleza makubaliana ya mikataba hiyo kwa wakati na kwamba serikali haitasita kuvunja mkataba
wowote ambao unatekelezwa kinyume na makubalino ikiwa ni pamoja na kuchukulia hatua za kisheria kwa kwenda
kinyume na mikataba hiyo.
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na
Teknolojia Dk. Leornald Akwilapo pamoja na Mwakilishi wa Uchumi na Biashara
nchini Tanzania Yuan Lin wakibadilisha hati za mkataba wa makubaliano ya ujenzi
wa chuo cha VETA kinachotarajiwa kujengwa mkoani Kagera.
Kwa
upande wake Mkurugenzi Mkuu wa VETA Dkt. Pancras Bujulu amesema Chuo hicho kitasaidia
kuongeza udahili wa wanafunzi katika fani mbalimbali za VETA kutokana na ukweli
kwamba mkoa huo ni mkubwa na kuwa hapo awali ulikuwa na chuo cha VETA kimoja
kinachojulikana kama Rwamishenye ambacho kilikuwa kidogo.
Naye
Mwakilishi wa China anayeshughulikia masuala ya Uchumi na Biashara nchini
Tanzania Yuan Lin amesema Serikali ya Tanzania na China zimekuwa marafiki kwa
muda mrefu na ndio maana China imeona umuhimu wa kusaidia ujenzi wa chuo hicho
ikiwa ni hatua ya kuunga mkono Juhudi za Serikali ya awamu ya Tano ya kuwa nchi
ya uchumi wa viwanda hadi ifikapo mwaka 2020.
Katibu
Mkuu Waizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dk. Leornald Akwilapo akisoma
mkataba wa makubaliano wa ujenzi wa chuo cha VETA kinachotarajiwa kujengwa mkoani
Kagera.
Jumamosi, 24 Novemba 2018
WAZIRI NDALICHAKO ASEMA AFRIKA ITAENDELEZWA NA WAAFRIKA WENYEWE
Waziri
wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako amesema wajibu wa kuiendeleza
Afrika uko mikononi mwa Waafrika wenyewe huku jukumu la wadau wengine wa
Maendeleo ni kusaidia kukua kwa
Maendeleo hayo.
Waziri
Ndalichako ametoa kauli hiyo Leo katika Mahafali ya Programu za ESAMI
yaliyofanyika katika Makao Makuu ya ESAMI jijini Arusha ambapo amesisitiza kuwa Waafrika wanapaswa kujisimamia wenyewe katika
nyanja za Kijamii na Kiuchumi kwa lengo
la kutimiza malengo ya bara hilo.
Waziri wa Elimu, Sayansi na
Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akimkabidhi cheti mmoja wa wahitimu wa kozi
za ESAMI katika Mahafali yaliyofanyika jijini Arusha
“
Ili Afrika iweze kuendelea lazima ijisimamie yenyewe katika masuala ya kijamii
na kiuchumi na hii itawezekana tu kupitia
vijana ambao wameandaliwa vyema
na wakawa tayari kuhakikisha wanaliendeleza bara la Afrika kwa ujasiri bila
kuhofia changamoto watakazokutana nazo,” alisisitiza Waziri Ndalichako
Kiongozi
huyo amesema bara la Afrika linahitaji Viongozi wenye ujasiri, ambao wapo
tayari kuhakikisha Afrika inakwenda mbele kiuchumi na Kijamii.
Waziri wa Elimu, Sayansi na
Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akiwa katika maandamano ya kitaaluma wakati
wa mahafali ya Programu za ESAMI yaliyofanyika katika Makao Makuu ya ESAMI
jijini Arusha
Akizungumza
katika mahafali hayo Mkurugenzi Mkuu wa ESAMI Prof. Bonard Mwape amesema wahitimu wote wameandaliwa
vyema kwenda kuleta Mabadiliko na
Maendeleo katika nchi zao pamoja na kuhakikisha
bara la Afrika linakuwa lenye
maendeleo.
Mahafali
hayo yamejumuisha zaidi ya wahitimu 360 kutoka nchi za Afrika ikiwemo Kenya,
Uganda, Rwanda, Namibia, Mali, Malawi DR- Congo, Burundi, Zimbambwe na wenyeji
Tanzania.
Baadhi ya wahitimu wa kozi
mbalimbali wakimsikiliza Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia (Hayupo
Pichani) wakati wa mahafali wakati wa mahafali ya Programu za ESAMI
yaliyofanyika katika Makao Makuu ya ESAMI jijini Arusha
Ijumaa, 23 Novemba 2018
THE
UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
MINISTRY
OF EDUCATION, SCIENCE AND TECHNOLOGY
Tender
No. ME-024/2016-17/HQ/G/36
For
SUPPLY
OF VARIOUS GOODS FOR EDUCATION SUPPORT RESOURCE AND ASSESSMENT CENTRE (RETENDERED)
Invitation
for Tender
Date: 26th November, 2018
- This
Invitation for Tender follows the General Procurement Notice for this
Project which appeared in Daily News and Procurement Journal Issue no.
1768 dated 16th October, 2016.
- The Government
of Tanzania through Ministry of
Education, Science & Technology has received a Grant from the
Global Partnership for Education (GPE) towards the cost of Literacy &
Numeracy Education Support (LANES) and it intends to apply part of the
proceeds of this Grant to cover eligible payments under the contract for
the supply of various goods for Education Support Resource and Assessment Centre.
- The
Permanent Secretary, Ministry of
Education, Science & Technology now invites sealed tenders from
eligible suppliers as tabulated below:
Lot
|
Description of Items
|
Qty
|
Delivery Period (after contract signing)
|
1
|
Office equipment
|
Various
|
Within 12 weeks
|
2
|
Intellectual- Toys
(Teaching Materials)
|
Various
|
Within 12 weeks
|
3
|
Stationery &
related Supplies
|
Various
|
Within 4 weeks
|
4
|
Specialized
Equipment( Intellectual and Hearing Equipment)
|
Various
|
Within 12 weeks
|
5
|
Cleaning Materials
|
Various
|
Within 4 weeks
|
6
|
Visual Impairment
Items
|
Various
|
Within 4 weeks
|
Tenderers are required to quote for one lot or combination of two, three, four,
five or all lots but in any case Tenderers are required to quote for all items and quantities specified in
each lot. Tenderers who do not quote
for all items and quantities will be considered non responsive and rejected in
evaluation.
- Tendering will be conducted through the
National Competitive Tendering procedures specified in the Public
Procurement Regulations, 2013 – Government Notice No. 446 and are open to
all Tenderers as defined in the Regulations.
- Interested
eligible Tenderers may obtain further information from and inspect the
Tendering Documents at the office of the Secretary of Tender Board, Ministry of Education, Science &
Technology, College of Business Studies and Law, Universities of Dodoma,
(UDOM), Block 10, P.O Box 10 40479Dodoma,
Office number 320 from 0900 to 1500 hours on Mondays to
Fridays inclusive except on public holidays.
- A complete set of Tendering Document (s) in English and additional sets may
be purchased by interested
Tenderers on the submission of a written application to the address given
under paragraph 5 above and upon payment of a non-refundable fee of Tzs. 100,000/= (Tanzania Shillings:
One hundred Thousand Only), Payment should be done through
Government e- Payment Gateway (Gepg) where the tenderer should get Control
number at office No. 327, at Ministry of Education, Science and
Technology.
7.
Tenders
for Lots 1, 2 & 4 must be accompanied by a Tender Security in an acceptable form in the amount of TZS. 20,000,000.00 (Tanzanian
shillings Twenty million).
8.
Tenders
for Lots 3, 5 & 6 must be accompanied by a Tender Securing Declaration in a
format provided.
- All tenders in one original
plus two copies properly filled in, and enclosed in plain envelopes must be
delivered to the Secretary of
Tender Board, Ministry of Education, Science & Technology, College of
Business Studies and Law, Universities of Dodoma, (UDOM), Block 10, P.O
Box 10 – 40479 Dodoma, Room 320
at or before 10:30am local hours on Tuesday, 11th December, 2018.
Tenders will be opened promptly thereafter in
public and in the presence of Tenderers’ representatives who choose to
attend in the opening at the Conference
Room, Ground Floor, Ministry of
Education, Science & Technology, College of Business Studies and Law,
Universities of Dodoma, (UDOM), Block 10, P.O Box 10 40479Dodoma.
10. late Tenders, Portion
of Tenders, Electronic Tenders, Tenders not received, Tenders not opened and
not read out in public at the tender opening ceremony shall not be accepted for
evaluation irrespective of the circumstances.
PERMANENT
SECRETARY,
MINISTRY
OF EDUCATION, SCIENCE & TECHNOLOG
University
of Dodoma (UDOM), Block No. 10, P.O. Box 10 40479 DODOMA
OLE NASHA: SERIKALI INATAMBUA MCHANGO WA WAHISANI KATIKA SEKTA YA ELIMU
Serikali imesema inatambua
mchango wa wahisani na wadau wa Elimu katika kuunga mkono juhudi za Serikali ya
awamu ya Tano katika kuendelea kuchangia ujenzi wa mabweni ya Wanafunzi wa
kike, ujenzi wa vyumba vya madarasa, ununuzi wa vifaa vya TEHAMA pamoja na
ununuzi wa vifaa vya wanafunzi wenye mahitaji maalum.
Kauli hiyo ya Serikali
imetolewa na Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe.William Ole Nasha
wakati akitunuku hati za utambuzi kwa Wahisani na Wadau ambao wamekuwa mstari
wa mbele katika kuchangia Miradi ya Elimu kupitia Mamlaka ya Elimu Tanzania
(TEA) kwenye hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha
akimkabidhi hati ya utambuzi kwa mchangiaji wa Miradi ya Elimu Kupitia Mamlaka
ya Elimu Tanzania (TEA) katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Akizungumza katika hafla
hiyo Naibu Waziri Ole Nasha amewahakikishia wahisani hao usalama wa fedha zao
na kuwa zitatumika kwa malengo yaliyokusudiwa na si vinginevyo.
“Niwahakikishie kuwa
Serikali inatambua mchango wenu katika kuunga mkono juhudi za Serikali katika
kuchangia Elimu, ikiwa ni pamoja na kuchangia ujenzi wa mabweni ya Wanafunzi wa
kike, ujenzi wa vyumba vya madarasa, ununuzi wa vifaa vya TEHAMA pamoja na
ununuzi wa vifaa vya wanafunzi wenye mahitaji maalum,”
“Pia fedha zilizotolewa na
Taasisi zenu zitatumika kama zilivyokusudiwa na si vinginevyo na endapo
itabainika kuwepo kwa matumizi ambayo siyo sahihi basi Serikali haitasita
kuchukua hatua za kisheria kwa wale wote watakaobanika kwenda kinyume na
maelekezo”alisisitiza Naibu Waziri Ole Nasha.
Wachangiaji wa Miradi ya Elimu kupitia Mamlaka ya Elimu Tanzania
(TEA) wakiwa katika picha ya pamoja na Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na
Teknlojia Mhe. William Ole Nasha mara
baada ya wahisani hao kutunukiwa hati za utambuzi.
Jumla ya Taasisi 18 za ndani
na nje ya nchi zilitunukiwa hati baada ya kuchangia takribani Shilingi bilioni 11 ambazo zimetumika kuboresha Miundombinu
mbalimbali ya Elimu.
Alhamisi, 22 Novemba 2018
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA ELIMU, SAYANSI NA
TEKNOLOJIA
Anuani ya simu “ELIMU”
Simu: 026 296 35 33
Baruapepe:info@moe.go.tz
|
|
Chuo cha Masomo ya Biashara na Sheria,
Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Jengo Na. 10,
S. L. P. 10,
40479 DODOMA.
|
TAARIFA KWA UMMA
Wizara ya Elimu,
Sayansi na Teknolojia inaufahamisha umma kuwa taarifa zinazosambazwa na Mtandao
wa Programu ya Wanafunzi Tanzania (TSNP) kwenye mitandao ya kijamii
zinazoelezea kuwa Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako
anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Semina ya Kuwajengea Uwezo Viongozi wa
Wanafunzi wa Vyuo Vikuu Tanzania siyo
sahihi.
Kwa mujibu wa taarifa
inayosambaa semina hiyo imepangwa kufanyika Desemba 1, 2018 katika ukumbi wa
Kisenga uliopo katika Jengo la LAPF Kijitonyama, Jijini Dar es salaam.
Mhe. Waziri hajapokea
mwaliko rasmi kutoka kwenye Mtandao huo hivyo hatarajii kushiriki semina hiyo,
pia katika tarehe tajwa atakuwa na majukumu mengine kwa mujibu wa ratiba yake.
Wizara haina taarifa
ya mwaliko au ushiriki wa kiongozi mwingine yeyote wa ngazi ya Wizara.
Imetolewa na;
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI
WIZARA YA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA
22/11/2018
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)