Alhamisi, 22 Novemba 2018


JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA

Anuani ya simu “ELIMU”
Simu: 026 296 35 33
Baruapepe:info@moe.go.tz
Tovuti: www.moe.go.tz


  
Chuo cha Masomo ya Biashara na Sheria,
Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Jengo Na. 10,
S. L. P. 10,
40479 DODOMA.           

TAARIFA KWA UMMA

Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia inaufahamisha umma kuwa taarifa zinazosambazwa na Mtandao wa Programu ya Wanafunzi Tanzania (TSNP) kwenye mitandao ya kijamii zinazoelezea kuwa Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Semina ya Kuwajengea Uwezo Viongozi wa Wanafunzi wa Vyuo Vikuu Tanzania siyo sahihi.

Kwa mujibu wa taarifa inayosambaa semina hiyo imepangwa kufanyika Desemba 1, 2018 katika ukumbi wa Kisenga uliopo katika Jengo la LAPF Kijitonyama, Jijini Dar es salaam.

Mhe. Waziri hajapokea mwaliko rasmi kutoka kwenye Mtandao huo hivyo hatarajii kushiriki semina hiyo, pia katika tarehe tajwa atakuwa na majukumu mengine kwa mujibu wa ratiba yake.

Wizara haina taarifa ya mwaliko au ushiriki wa kiongozi mwingine yeyote wa ngazi ya Wizara.
Imetolewa na;
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI
WIZARA YA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA
22/11/2018

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni