Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa amesema Teknolojia ya Habari na Mawasiliano(TEHAMA)
ikitumika vizuri katika sekta ya elimu itasaidia kujenga mazingira mazuri na
kuwezesha kuwepo kwa mbinu bora katika ufundishaji na ujifunzaji.
Waziri
Mkuu Majaliwa ametoa kauli hiyo jijini Dar Es Salaam katika halfa ya utoaji wa
tuzo kwa washindi wa mashindano ya
Teknolojia ya Habari na Mawasiliano kwa mwaka 2018 yaliyoandaliwa na Taasisi ya
Huawei Tanzania, na kusisitiza kuwa kutumia TEHAMA katika ufundishaji na
ujifunzaji Mwalimu mmoja anaweza
kufundisha wanafunzi wengi waliosehemu tofauti.
Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa akimkabidhi zawadi
mshindi wa kwanza wa mashindano ya TEHAMA yaliyoandaliwa na Huawei Tanzania
Emannuel Chaula kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Mhe.
Majaliwa amewataka wanafunzi kutumia fursa ya mashindano hayo kuendelea
kujifunza TEHAMA ili wewe na uwezo wa
kumiliki mifumo ambayo itasaidia nchi
katika kurahisisha utendaji wa shughuli zake kupitia sayansi na Teknolojia
Aidha,
Waziri Mkuu Majaliwa amesema serikali inaendelea kuunganisha mkongo wa Taifa wa
Mawasiliano kwenye taasisi zake ili kufanikisha azma ya serikali ya kurahisisha
utendaji kazi.
Akizungumza
katika hafla hiyo Waziri wa Elimu, Sayansi naTeknolojia Prof. Joyce Ndalichako
amewataka vijana walioshiriki katika mashindano hayo kuendelea kujifunza zaidi
kwani nchi bado inahitaji Maendeleo katika kipindi ambacho serikali imekusudia
kujenga uchumi wa viwanda.
Waziri
wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akimkabidhi mmoja wa washindi wa mashindano ya TEHAMA tuzo katika hafla ya utoaji wa tuzo kwa washindi wa
mashindano ya TEHAMA iliyofanyika jijini Dar es Salaam ambapo amewataka vijana
walioshiriki katika mashindano hayo kuendelea kujifunza zaidi.
Naye
Mkurugenzi Mkuu wa HUAWEI Tanzania Frank Zhou amesema kabla ya vijana hao
kuingia katika mashindano hayo walipatiwa mafunzo ili kuwawezesha kuzitambua
Teknolojia za kisasa kwa kuwa Teknolojia
inakua kila siku.
Mashindano
hayo ya TEHAMA yalianza na vijana 500 lakini mpaka mwishoni vijana 10 tu ndio wamefanikiwa kushinda ambapo washindi
watatu wa juu wanatarajiwa kwenda katika nchi za Afrika Kusini na China kwa
lengo la kujifunza zaidi masuala ya TEHAMA.
Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa pamoja na Waziri wa
Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako wakiwa katika picha ya
pamoja na Balozi wa China na Viongozi wa Taasisi ya Huawei Tanzania wakati wa
hafla ya kutoa tuzo kwa washindi wa mashindano ya TEHAMA 2018 iliyofanyika
jijini Dar es Salaam.