JAMHURI
YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA ELIMU, SAYANSI
NA TEKNOLOJIA
Anuani
ya simu “ELIMU”
Simu:
026 296 35 33
Baruapepe:info@moe.go.tz
Tovuti:
www.moe.go.tz
|
|
Chuo cha Masomo ya Biashara
Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Jengo Na.
10,
S.L.P. 10,
40479 DODOMA.
Tarehe: 14 Desemba, 2018.
|
WARAKA
NA. 1 WA MWAKA 2018
MWONGOZO
WA UUNDAJI NA UENDESHAJI WA KAMATI NA BODI ZA SHULE
Kwa mujibu wa Sheria ya
Elimu Na. 25 ya mwaka 1978 na Rekebisho lake Sura 353 ya mwaka 2002 kila Shule ya
Msingi na Sekondari sharti iwe na Kamati ya Shule (kwa shule za Awali na
Msingi) au Bodi ya Shule (kwa shule za Sekondari) iliyo hai. Aidha, Serikali imekuwa
ikitoa miongozo juu ya utaratibu wa kuunda na kuendesha Kamati
na Bodi hizo.
Waraka huu unalenga kutoa
mwongozo mahsusi kuhusu muundo, wajibu na uendeshaji wa Kamati na Bodi za shule.
1.0
KAMATI
ZA SHULE ZA AWALI NA MSINGI/BODI ZA SHULE ZA SEKONDARI
1.1
Kamati
za Shule za Awali na Msingi za Serikali na Zisizo za Serikali
Shule
zote zitakuwa na Kamati (Kwa Shule za Awali na Msingi) na Bodi kwa Shule za Sekondari).
1.2 Sifa
za Wajumbe na Utaratibu wa Uundaji wa Kamati na Bodi za Shule
a)
Itaundwa na wajumbe wasiopungua tisa (9),
b)
Diwani,
Mwenyekiti na Katibu wa Serikali ya Kijiji/Mtaa (wa eneo shule ilipo) hawatakuwa
na sifa ya kuwa wajumbe wa Kamati/Bodi ya shule. Hii ni kuepusha mgongano wa
kiutendaji kutokana na jukumu lao la kuiwakilisha Serikali katika ngazi zao za
utawala,
c)
Kamati itakuwa na vikao visivyopungua viwili (2) kwa mwaka. Mwenyekiti anaweza kuitisha kikao cha dharura kama kuna
suala linalohitaji kujadiliwa,
d)
Wajumbe wa Kamati/ Bodi wanatakiwa wawe na
sifa zifuatazo:
i.Wawe na elimu ya Kidato cha Nne au
zaidi,
ii.Wawe na shughuli halali za kujipatia
kipato,
iii.Uwiano wa wajumbe uzingatie jinsi
zote mbili,
iv.Mwenyekiti
na Makamu Mwenyekiti achaguliwe na Wajumbe wa Kamati kutoka miongoni mwao.
e)
Kamati ya Shule itakuwa na kamati ndogondogo
tatu (3) zifuatazo:
i. Kamati
ya Taaluma, Malezi na Unasihi,
ii.Kamati ya Fedha, Mipango na Miundombinu,
na
iii.Kamati ya Mazingira, Afya na Chakula.
f)
Wajumbe wa Kamati/Bodi za Shule watathibitishwa
na Afisa Elimu wa Wilaya.
1.3 Wajibu na Majukumu ya Kamati ya
Shule
a)
Kuandaa/kuidhinisha Mpango wa Maendeleo ya
shule na mikakati ya utekelezaji wake,
b)
Kuitisha na kuendesha vikao vya wazazi na
kutoa taarifa ya maendeleo ya shule,
c)
Kwa shule za serikali kuidhinisha matumizi
ya fedha za shule na kusimamia matumizi bora ya fedha za uendeshaji na
maendeleo ya shule,
d)
Kwa shule zisizo za serikali, kushauri
namna bora ya matumizi ya fedha kwa
miradi ya maendeleo ya shule ikiwemo ukarabati wa miundombinu,
e)
Kuhimiza ujenzi wa shule na usafi wa
mazingira ya shule na wanafunzi,
f)
Kwa shule za serikali, kusimamia ujenzi na
ukarabati wa madarasa na miundombinu mingine na utunzaji wa mazingira ya shule,
g)
Kusimamia ufundishaji na ujifunzaji
shuleni kwa kuhakikisha kuwa walimu wanafanya kazi zao kwa ufanisi,
h)
Kuhakikisha wanafunzi wote wanahudhuria
masomo kwa mujibu wa sheria,
i)
Kuhakikisha shule inakuwa na Sanduku la
Huduma ya Kwanza na pia shule inadumisha elimu ya afya shuleni kwa njia
mbalimbali,
j)
Kuhakikisha huduma za Malezi na Unasihi
kwa wanafunzi zinaendeshwa kwa ufanisi shuleni,
k)
Kutathmini uhalali wa
kumsimamisha/kumfukuza shule mwanafunzi bila upendeleo wala kushawishiwa na mtu
au kikundi chochote kabla ya kuhalalisha uamuzi huo,
l)
Kuhakikisha Kamati inakutana ndani ya wiki mbili inapotokea shule
imependekeza kumsimamisha/kumfukuza mwanafunzi ili uamuzi sahihi utolewe kwa
wakati kuepusha ucheleweshaji unaoweza kuathiri haki za kielimu za mwanafunzi
husika pasipo sababu za msingi, na
m)
Kamati
itafanya
kazi kwa muda wa miaka mitatu (3).
2.0 MUUNDO WA KAMATI/BODI ZA SHULE
Katika kuunda Kamati na Bodi za Shule
za Serikali na zisizo za Serikali mambo yafuatayo yatazingatiwa:
2.1 Wajumbe
wa Kamati za Shule za Awali na Msingi za Serikali
i.
Mwalimu
Mkuu ambaye pia atakuwa Katibu wa Kamati,
ii.
Mwalimu
wa Taaluma katika shule,
iii.
Wawakilishi
wawili (2) wa walimu shuleni,
iv.
Iwapo
shule ina kitengo kwa ajili ya watoto wenye mahitaji maalum, Mkuu wa Kitengo
naye atakua Mjumbe,
v.
Wajumbe
watatu (3) watakaochaguliwa na mkutano wa wazazi, na
vi.
Mkazi
jirani atakayeteuliwa na Mkuu wa shule.
2.2
Kamati
za Shule za Awali na Msingi Zisizo za Serikali
i.
Mkuu
wa shule ambaye atakuwa Katibu wa Kamati ya shule,
ii.
Mmiliki
wa shule,
iii.
Mwalimu
wa Taaluma,
iv.
Wajumbe
watatu (3) watakaoteuliwa na Mmiliki wa Shule,
v.
Mwakilishi
mmoja (1) wa walimu shuleni.
vi.
Iwapo
shule ina kitengo kwa ajili ya watoto wenye mahitaji maalum, Mkuu wa Kitengo
naye atakua Mjumbe,
vii.
Mzazi
mmoja (1) anayewakilisha wazazi wenye watoto katika shule hiyo atakayechaguliwa
na Mkutano Mkuu wa Wazazi,
viii.
Mkazi
mmoja jirani atakayeteuliwa na Mwenye shule.
2.3 Bodi
za Shule za Sekondari za Serikali
i.
Mkuu
wa Shule ambaye atakuwa Katibu wa Bodi,
ii.
Mwalimu
wa Taaluma katika shule,
iii.
Wawakilishi
wawili (2) wa walimu shuleni,
iv.
Iwapo
shule ina kitengo kwa ajili ya watoto wenye mahitaji maalum; Mkuu wa Kitengo pia
atakua mjumbe katika Bodi ya shule,
v.
Wajumbe
watatu (3) wanaowakilisha wazazi wenye watoto katika shule hiyo watakaochaguliwa
na Mkutano Mkuu wa wazazi, na
vi.
Mkazi
jirani atakayeteuliwa na Mkuu wa shule.
2.4 Bodi
za Shule za Sekondari Zisizo za Serikali
i.
Mkuu
wa shule ambaye atakuwa Katibu wa Bodi ya shule,
ii.
Mmiliki
wa shule,
iii.
Mwalimu
wa Taaluma,
iv.
Wajumbe
watatu (3) watakaoteuliwa na Mmiliki wa Shule,
v.
Mwakilishi
mmoja (1) wa walimu shuleni.
vi.
Iwapo
shule ina kitengo kwa ajili ya watoto wenye mahitaji maalum, Mkuu wa Kitengo
pia atakua Mjumbe,
vii.
Mzazi
mmoja (1) anayewakilisha wazazi wenye watoto katika shule hiyo atakayechaguliwa
na Mkutano Mkuu wa Wazazi,
viii.
Mkazi
mmoja jirani atakayeteuliwa na Mwenye Shule.
Waraka huu unafuta Nyaraka
zote za awali zilizokuwa zinatoa Mwongozo kuhusu Kamati za Shule za Awali na
Msingi na Bodi za Shule za Sekondari na utaanza kutumika kuanzia Januari, 2019.
Dkt. Edicome C. Shirima
KAIMU KAMISHNA WA ELIMU
Nakala: Makatibu Tawala wa Mikoa,
Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya/Mji/Manispaa/Jiji,
Wathibiti
Ubora wa Shule Wakuu Kanda na Wilaya.