Wanafunzi wa shule ya Sekondari
Chidya iliyopo Wilaya ya Masasi mkoani Mtwara wameipongeza serikali kwa
kuboresha miundombinu ya shule hiyo pamoja na kuchimba kisima ambacho kimewapungizia
adha ya upatikanaji wa Maji kwa urahisi.
Wanafunzi hao wametoa kauli hiyo
wakati walipofanya mahojiano na waandishi wa habari kufuatia ziara ya
ufuatiliaji wa uboreshaji wa miundombinu ya shule na ujifunzaji na ufundishaji
wa Kusoma, Kuandika na Kuhesabu - KKK.
Wanafunzi hao wamesema mwanzoni miundombinu
ilikuwa imechakaa pia walikuwa wanafuata Maji umbali takribani kilometa moja na
pia iliwalazimu kila siku kuamka alfajiri ili kufuatilia Maji hivyo iliwafanya
wachoke na hata kupunguza morali ya kusoma.
Jengo la Utawala lililokarabatiwa katika Shule ya Sekondari Chidya Wilayani
Masasi Mkoani Mtwara.
“Kwa kweli hili la Maji wanafunzi lilikuwa
linakera sana maana inatulazimu kuamka kila siku alfajiri kufuatilia maji na
kisha kujindaa kuelekea shuleni kwa ajili ya masomo, kwa kweli hii ilikuwa
inatuchosha na pia ilikuwa ni hatari kwa sababu tulikuwa tunakutana na wadudu
wabaya kama vile nyoka,” anasema mmoja wa wanafunzi hao Saidi Mnguvu.
“Nakumbuka tulikuwa tunatolewa darasani kwa
ajili ya kuafuatilia maji, hata vipindi wakati mwingine vilikuwa vinakatishwa
ili tuweze kwenda kufuata Maji sasa adha hii ya Maji kwa kweli imeisha na sasa
tunaishi kwa raha na tunapata Maji muda wote,” anasema Mnguvu.
Muonekano wa
vyumba vya madarasa vilivyojengwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia
kupitia Programu ya Lipa Kulingana na Matokeo (EP4R) katika Shule ya Sekondari
Chidya iliyopo Wilayani Masasi Mkoani Mtwara.
Mkuu wa shule hiyo ya Sekondari ya Chidya
Zawadi Mdimbe ali
sema shule hiyo ilipokea zaidi ya milioni Mia mbili kutoka
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kupitia Programu ya Lipa kulingana na
matokeo yaani (EP4R) ambazo zimetumika kukarabati Miundombinu ya vyumba vya
madarasa, ujenzi wa Nyumba za walimu, kuboresha miundombinu ya Maji, bwalo,
Jiko pamoja na kukarabati ofisi za walimu za shule hiyo.
Muonekano wa majengo
mawili yenye vyumba vya madarasa vilivyokarabatiwa katika Shule ya Sekondari
Chidya Wilayani Masasi Mkoani Mtwara.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
Zingatia: Mwanachama wa blogu hii tu ndiye anayeweza kuchapisha maoni.