Naibu
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. William Ole Nashaa mesema Sayansi,
Teknolojia na ubunifu ina mchango mkubwa katika ukuaji wa uchumi wa viwanda.
Naibu
Waziri Ole Nasha amesema hayo leo wakati wa kufungua mashindano ya kitaifa ya Sayansi,
Teknolojia na ubunifu yanayofanyika mkoani Dodoma na kusisitiza kuwa ubunifu na
ugunduzi una fursa ya kuchagiza katika kuongeza tija kwenye viwanda vikubwa,
hivyo uhamasishaji wa pamoja unahitajika.
Naibu Waziri Mhe. William Ole Nasha akizungumza wakati akifungua mashindano ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu ambayo kitaifa yanafanyika mkoani Dodoma. |
“Hulka
ya ubunifu ni mtu anazaliwa nayo, na kwa jinsi nilivyotembelea mabanda mbalimbali
ya maonesho haya tayari mimi naona wote hapa ni washindi, sasa niishauri Tume ya
Taifa ya Sayansi na Teknolojia - COSTECH ione namna ya kuwaendeleza wabunifu wote
na isiwe ni kwa wabunifu wachache,” alisema Naibu Waziri Ole Nasha.
Mhe.
Ole Nasha amesema kutokana na umuhimu wa wabunifu na wagunduzi nchini ni vyema wananchi
wakaendelea kuhamasishwa ikiwa ni pamoja na mashindano hayo yakawa yanafanyika kila
mwaka.
Mwanafunzi wa shule ya Sekondari Ilboru, Maximillian akimuelezea Naibu Waziri Ole Nasha na Viongozi wengine namna anavyotekeleza ubunifu wake. |
Akizungumza
kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Kaimu Katibu Mkuu Profesa James Mdoe amesema lengo
la mashindano hayo ni kukuza hamasa za ubunifu na kuchochea ugunduzi utakaohamasisha
Mapinduzi ya Viwanda.
Mwanafunzi wa Chuo Cha Usafirishaji - NIT akimuendesha Naibu Waziri kwenye gari ambalo linatumia mfumo wa umeme kufanya kazi, na kuwa gari hilo halina injini. |
Baada
ya mashindano hayo kutangazwa Wabunifu zaidi ya 400 walijitokeza kushiriki na kati
yao wabunifu 60 walichaguliwa kiushindani na ndiyo ambao wameshiriki mashindano
ambayo yanafanyika kitaifa mkoani Dodoma.
Bustani ya mbogamboga ambayo haitumii udongo ikiwa imeoteshwa mboga mbalimbali za majani. |