Wizara
ya Elimu, Sayansi na Teknolojia inatangaza nafasi za kujiunga katika Vyuo vya
Maendeleo ya Wananchi (FDC) kwa mwaka
2020.
Sifa za
Mwombaji ni mwananchi yeyote mwenye nia ya kupata ujuzi na maarifa mbalimbali.
Aina ya
Mafunzo yanayotolewa ni:
1. MAFUNZO YA UFUNDI STADI- NGAZI YA I, II
&III
- Ufundi Umeme wa Magari : (Ifakara, Katumba, Nzovwe, Rubondo, Same,
Sofi, Kisangwa, Mto wa Mbu,Chala,Handeni, Ikwiriri, Karumo, Kilosa, Katumba,
Kibondo, Kilwa Masoko, Kihiga, Mamtukuna, Malampaka, Kiwanda,Malya).
- Ufundi Mekanika, (Vyuo vyote vinavyofundisha Ufundi
Magari).
- Ufundi
Umeme wa Majumbani, (Vyuo
vyote vinafundisha kozi hii).
- Ufundi Magari : (Bigwa, Chala, Chilala, Handeni, Ifakara,
Ikwiririri, Karumo, Kilosa, Kisarawe, Katumba, Kibondo, Kilwa Masoko, Kisangwa,
Kihinga, Singida Mamtukuna, Malampaka, Malya, Masasi, Mbinga, Msinga, Mtawanya,
Musoma, Mwanhala, Mwanva, Mto wa Mbu, Munguri, Nandembo, Newala, Ngara, Njombe,
Nzega, Nzovwe, Rubondo, Same, Sengerema, Sofi, Urambo).
- Useremala:
(Bariadi, Mtawanya, Chala, Chilala, Chisala,
Handeni, Ifakara, Ilula, Ulembwe, Kiwanda).
- Uashi: (Vyuo vyote vinavyofundisha Uashi
isipokuwa Mtowambu, Nzega, Ikwiriri, Buhangija, Kiwanda, Chilala, Bigwa na
Sikonge).
- Ushonaji: (Vyuo
vyote vinafundisha ushonaji isipokuwa, Arnatouglu, Handeni, Sofi).
- Upishi:
(Urambo,
Sofi, Singida, Same, Nzovw, Nzega, Njombe, Mto wa Mbu, Mwanhala, Mtawanya,
Msanginya, Masasi, Mamtukuna, Kiwanda, Kisarawe, Kilosa, Ilula, Ikwiriri, Ifakara,
Handeni, Arnatouglu, Bigwa na Bariadi).
- Uchomeleaji: (Gera,
Ifakara, Karumo, Kisarawe, Kisangwa, Kiwanda, Malya, Mtawanya, Mwanhala, Munguri,
Newala, Njombe, Nzovwe, Sikonge, Nzega, Sengerema, Sikonge, Sofi, Ulembwe na
Urambo).
- Kompyuta:
vyuo vyote vinafundisha isipokuwa, (Sofi,
Sikonge, Same, Newala, Nandembo, Munguri, Mto wa Mbu, Musoma, Mtawanya, Msingi,
Msanginya, Muhukuru, Masasi, Mamtukuna, Kiwanda, Kisangwa, Kisarawe, Ifakara,
Handeni, Gera, Chilala na Arnatouglo).
- Kilimo
na Ufugaji: (Chisalu, Gera, Kiwanda, Handeni, Ifakara,
Ikwiriri, Kilosa, Kilwa Masoko, Kisangwa, Mamtukuna, Malampaka, Mamtukuna Malampaka,
Malya, Muhukuru, Msanginya, Msingi, Mwanhala, Njombe, Nzovwe, Same, Singida, Bigwa, Tango,
Urambo).
- Utunzaji
wa watoto (Day care): (Nzovwe, Bigwa, Mtawanya, Msingi, Mtawanya,
Msinga, Masasi, Katumba, Chisalu).
- Elimu
haina mwisho (Sekondari nje ya mfumo rasmi kwa
wasichana tu): (Chilala, Ilula, Karumo,
Katumba, Malya, Masasi, Muhukuru, Msanginya, Msinga, Msingi, Mtawanya, Mwanva,
Mputa, Mto wa Mbu, Ngara, Njombe, Nzega, Nzovwe, Bigwa, Rubondo, Sengerema).
- Mpira fursa kwa Wanafunzi wa
kike tu: (Sengerema, Nzovwe, Mputa, Masasi, Katumba,
Bigwa na Nzega).
- Uongozaji Watalii: (Kilwa Masoko, na Ngara).
- Udereva: (Tarime, Kiwanda, Tango, Sofi, Sikonge,
Rubodo, Nzega, Malya, Kilwa Masoko, Ikwiriri, Chala).
- Ufundi Bomba: (Kiwanda).
2. MAFUNZO
MAALUM
Muda
hulingana na Mahitaji ya Wahusika
i.
Elimu ya Sekondari Nje ya Mfumo Rasmi
(Elimu haina Mwisho)
ii.
Utunzaji wa Watoto Wadogo (Day Care)
iii.Mpira fursa (Michezo)
3. MAFUNZO
YA MUDA MFUPI
Mafunzo
haya hutolewa kwa wananchi mbalimbali sambamba na vikundi mbalimbali kulingana
na mahitaji yao.
Aidha,
pamoja na mafunzo haya yaliyoainishwa hapo juu, washiriki watajifunza masomo
yafuatayo ya Uelewa kulingana na mahitaji ya wahusika. Masomo hayo ni pamoja na:
Kiingereza, Uraia, Uchumi, Hifadhi ya Mazingira,
Ujasiriamali na Afya ya Jamii.
GHARAMA YA WASHIRIKI
Gharama
kwa Mafunzo ya Ufundi Stadi na Mafunzo Maalum kwa mwanachuo wa Bweni na Kutwa
malipo ni kama ifuatavyo:-
a) Gharama kwa Wanachuo wa Bweni ni shs. 250,000/=
- Ada
ya Mafunzo -TShs.
100,000/=
- Gharama
nyingine -TShs. 150,000/=
Jumla TShs. 250,000/=
NB: Gharama nyingine inajumuisha:
i) Kitambulisho -TShs
5,000/=
ii) Fedha ya ukarabati -TShs. 25,000/=
iii) T-shirt
(sare) -
TShs. 15,000/=
iv) Godoro
- TShs. 5,000/=
v) Vifaa vya mafunzo - TShs 100,000/=
b) Gharama kwa Wanachuo wa Kutwa ni shs. 245,000/=;
a) Ada ya
Mafunzo -TShs. 100, 000/=
b) Gharama
nyingine -TShs. 145,000
Jumla -TShs- 245,000/=
NB:
Gharama nyingine inajumuisha:
i) Kitambulisho - TShs 5,000/=
ii) Fedha ya ukarabati -TShs. 25,000/=
iii) T-shirt
(sare) - TShs. 15,000/=
iv) Vifaa
vya mafunzo - TShs 100,000/=
- TShs 145,000/=
c)
Kwa
mafunzo ya Muda Mfupi ni Tshs 20,000/= kwa mshiriki kwa mwezi.
N.B - Ada kiasi
cha Tshs. 100,000/- ilipwe kwenye
mfumo wa Serikali na mwanafunzi atalazimika kupata Namba ya Malipo (Control Number) toka chuoni ili afanye
malipo na gharama nyingine zilipwe kwenye akaunti ya Chuo na zitakatiwa risiti
ya Chuo. Ada inaweza kulipwa kwa awamu mbili (2) tu.
Imetolewa na:
KATIBU
MKUU
WIZARA YA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA