Alhamisi, 14 Machi 2019

SERIKALI IMESEMA INATAMBUA MCHANGO WA VYUO VIKUU BINAFSI HAPA NCHINI


Rais Mstaafu wa awamu Tatu Benjamin William Mkapa amekipongeza Chuo Kikuu Kishiriki cha Jordan JUCo kwa kutimiza jubilee ya miaka 25 ya utoaji huduma ya Elimu ya Juu nchini  na kuwa Serikali inatambua mchango mkubwa wa Chuo hicho na vyuo vingine binafsi katika kuwezesha upatikanaji wa elimu nchini hususan elimu ya juu .

Mhe. Mkapa amesema hayo katika kilele cha sherehe za Jubilee  zilizofanyika katika Chuo hicho jijini Morogoro na kuhudhuriwa na wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi. Aidha amesema pamoja na kazi nzuri wanayofanya vyuo binafsi, ada zinazotozwa katika vyuo hivyo bado ziko juu, hivyo amevitaka kuhahakisha wanajiendesha kwa gharama nafuu bila kuathiri ubora na kuhakikisha wanatoza ada kwa viwango ambavyo Watanzania walio wengi watamudu na kuweza kupata elimu hiyo kwa maendelo yao na taifa kwa ujumla.

“Niseme kuwa Elimu pekee ndiyo inachangia maendeleo ya mtu mmoja mmoja na baadae Taifa kwa ujumla, hivyo ni vyema gharama za ada ziwe ni zile ambazo wananchi wa kawaida watamudu, ikumbukwe kuwa wananchi walio wengi wanategemea mikopo inayotolewa na Serikali, sasa Vyuo binafsi ni vyema vikaliangalia hili,” alisema Mzee Mkapa.


Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin William Mkapa akiwa ameongozana na viongozi mbalimbali wakati wa maadhimisho ya Jubilee ya miaka 25 ya Chuo Kikuu Cha Jordan kilichopo Mkoani Morogoro.

Awali akizungumza katika Jubilee hiyo Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako amesema Serikali inaendelea kuboresha mazingira ya utoaji elimu ya juu ili kuongeza ubora na kuwa haitavifumbia macho vyuo ambavyo havitatii na kuzingatia vigezo, sheria, taratibu na kanuni za uendeshaji wa vyuo hapa nchini.

“Nitoe wito kwa vyuo vyote nchini kuhakikisha vinakidhi vigezo vya uendeshaji wa vyuo, tofauti na hapo serikali haitasita kuchukua hatua stahiki kwa vyuo vitakavyokwenda kinyume. Lengo la serikali ni kuhakikisha Elimu bora inatolewa nchini ili kuzalisha wataalamu wenye uwezo na maarifa kwa ukuaji wa uchumi,”alisema Waziri Ndalichako.


Waziri Ndalichako amesema hadi sasa Tanzania kuna vyuo vikuu na vyuo vikuu vishiriki 49 ambapo kati ya hivyo  34 ni vyuo binafsi ambayo ni sawa na asilimia 69.4, hivyo Serikali inatambua mchango mkubwa wa Vyuo binafsi na amekipongeza Chuo Cha Jordan kwa kutimiza miaka 25. 


Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin William Mkapa akizindua Kitabu Maalumu wakati wa maadhimisho ya kutimiza miaka 25 kwa Chuo Kikuu Cha Jordan, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia pia alishiriki maadhimisho hayo.

Aidha Waziri Ndalichako alisisitiza pia kuwa serikali inaendelea kuimarisha Bodi ya Mikopo ili kutoa mikopo zaidi kwa wanafunzi ambapo alisema kumekuwa na ongezeko la idadi ya wanafunzi wanaopata mikopo  hiyo ambapo kutoka mwaka 2004/05 hadi  mwaka 2018/19 wanufaika wa mikopo kwa ujumla ni 480,405.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Steven Kebwe  amesema Chuo Cha Jordan kutimiza miaka 25 ni hatua kubwa na kuwa Chuo hicho ni miongoni mwa vyuo vya mfano katika mkoa huo kwa sababu mkoa haujawahi kupokea taarifa za wanafunzi wa Chuo hicho kujihusisha na makundi wala vitendo viovu. Aidha ameahidi kushirikiana na chuo hicho kwa kutumia watalaamu wanaoandaliwa hapo kwa ajili ya maendeleo ya Mkoa.
Baadhi ya Wanafunzi na wageni mbalimbali wakifuatilia hotuba mbalimbali za Viongozi wakati wa Maadhimisho ya Miaka 25 ya Chuo Kikuu cha Jordan kilichopo Mkoani Morogoro.

Jumatano, 13 Machi 2019

WIZARA YA ELIMU YAAHIDI KUENDELEA KUSHIRIKIANA NA WADAU WA TEHAMA KUENDELEZA VIPAJI VYA WANAFUNZI

Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imeahidi kuendelea kushirikiana na Taasisi za Serikali na zisizo za Serikali ambazo zinajihusisha na masuala ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano(TEHAMA) kuibua vipaji vya wanafunzi na kuviendeleza.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako wakati wa hafla ya kufunga mafunzo na mashindano ya kitaifa ya wasichana na Tehama yaliyoandaliwa na Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) Jijini Dodoma.

Waziri Ndalichako amesema ni vyema vipaji vya wanafunzi washiriki wa mafunzo na mashindano ambavyo vimeibuliwa vikaendelezwa kwa kuwa vinalenga kutumia TEHAMA kutatua changamoto zilizopo katika jamii yetu na kusisitiza kuwa Serikali inahimiza matumizi sahihi ya teknolojia ya habari na mawasiliano kwa maendeleo ya Taifa.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako akitoa zawadi kwa mwanafunzi Khatija Saphy kutoka mkoa wa Tabora mmoja kati ya washindi 6 walioibuka  kidedea katika mashindano ya  wanafunzi wa kike na TEHAMA  yaliyoandaliwa na Mfuko wa Mawasiliano kwa wote jijini Dodoma. 
Kiongozi huyo ameipongeza UCSAF kwa kuandaa mafunzo na mashindano hayo kwa wanafunzi wa kike kutoka shule mbalimbali za umma nchini, ambapo pia amesisitiza kuwa vijana wote wa kike na wa kiume wana vipaji na ni wabunifu wanachohitaji ni vipaji vyao kuibuliwa kwa kupewa fursa na kuendelezwa.

“Niwasihi sana wadau wote, vijana na hususan wanafunzi kuhakikisha mnatumia vema teknolojia ya habari na mawasiliano kwa sababu inaweza kuwakuza kitaaluma, kiuchumi na kijamii kwa ujumla wake kama ikitumika vizuri,” alisema Waziri Ndalichako.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako akizungumza  wakati wa hafla ya kufunga mashindano ya kitaifa ya wasichana na TEHAMA yaliyofanyika katika Chuo Kikuu cha Dodoma, Jijini Dodoma. Amewataka wanafunzi kutumia Teknolojia ya Habari na Mawasiliano katika masuala yanayowasaidia kitaaluma.
Amesema nia ya serikali ni kuona mchango wa sayansi, teknolojia na ubunifu unaongeza tija katika uzalishaji hususan katika sekta ambazo zinagusa wananchi walio wengi ikiwemo kilimo, mifugo, viwanda pamoja na kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma katika jamii.

“Mnaweza kuona hapa wanafunzi wa kike wametengeneza application ya kutoa huduma kwa mama mjamzito na hayo ni mafunzo ya siku nne tu, je wangeongezewa muda? Hii inaonesha watoto wa kike wanaweza,“ aliongeza Waziri Ndalichako.

Aidha Waziri Ndalichako amewataka watanzania hususan vijana kutumia teknolojia ya habari na Mawasiliano kwenye shughuli za kimaendeleo badala ya kujikita katika mitandao ya kijamii ya facebook na instagram huku akiwaasa wanafunzi kutumia Tehama katika masuala yanayoleta tija badala ya kutumia muda mwingi kuchat vitu visivyo na tija.
Baadhi ya wanafunzi walioshiriki mafunzo na mashindano ya kitaifa ya wasichana na TEHAMA wakifuatilia hotuba ya Waziri wa elimu.
Naye Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote, Mhandisi Peter Ulanga amesema Mfuko huo katika mikakati yake imejipanga kuhakikisha inafikisha elimu ya TEHAMA pamoja na kutoa vifaa kwa shule za umma hapa nchini na kwamba hadi sasa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote umekwisha peleka kompyuta katika shule za umma 500 ambapo kila shule imepata kompyuta 5 ikiwa ni pamoja na kutoa mafunzo ya TEHAMA kwa walimu zaidi ya 500.

Mhandisi Ulanga, alieleza kuwa mafunzo na mashindano hayo ni sehemu ya maadhimisho ya kimataifa ya siku ya MTOTO WA KIKE na TEHAMA Duniani yanayoadhimishwa mwezi Aprili kila Mwaka na kuhusisha wanafunzi wa kike toka mataifa mbalimbali. Maadhimisho hayo yaliyoambatana na mafunzo ya siku nne yalikuwa na Kaulimbiu isemayo ‘Kuongeza mipaka na kubadili mitizamo’ na yameshirikisha wanafunzi wa kike zaidi ya 240 kutoka mikoa yote ya Tanzania Bara na Visiwani ambapo wanafunzi 6 kati yao wameibuka washindi na kuzawadiwa vikombe pamoja na kompyuta na fursa ya kushiriki katika Maadhimisho ya kimataifa yatakayofanyika nchini Ethiopia.


Ulanga aliongezea kuwa UCSAF itaendelea na mpango huo na kuongeza idadi ya washiriki ili kukuza ujuzi na kuhamasisha matumizi sahihi ya TEHAMA miongoni mwa wanafunzi wa kike nchini na kuwashukuru wadau wote walioshiriki kufanikisha maadhimisho hayo mwaka huu, ikiwemo, Vodacom, DIT, UDOM, CBA Bank na TERMET.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa kike walioshiriki mashindano ya kitaifa ya wasichana na TEHAMA yaliyofanyika Jijini Dodoma.

Jumanne, 12 Machi 2019


UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
MINISTRY OF EDUCATION, SCIENCE AND TECHNOLOGY 



SCHOLARSHIP TENABLE IN REPUBLIC OF MAURITIUS FOR THE ACADEMIC YEAR 2019/2020

1.0 Call for Application

The General Public is hereby informed that, the Republic of Mauritius has opened the new scholarships for African Union States (Africa Scholarship Scheme Edition 2019) for the Academic year 2019/2020. Interested applicants are invited to visit the Mauritius Ministry of Education Website to access guidelines and application forms: http://ministry-education.govmu.org. Further information can be obtained through the following link: http://ministry-education.govmu.org/English/educationsector/Documents/2019/Guidelines%20for%20Applicants%20.pdf
 Application form can be obtained from the following link:
http://ministry- education.govmu.org/English/educationsector/Documents/2019/Application%20Form%20postgraduate.pdf
The application form must be filled electronically, printed and signed. The hard copy should be submitted to the Ministry of Education, Science and Technology for nomination.

2.0Admission Requirements for the Scholarships
The applicant must submit the following documents:
·        Completed application form;
·        Certified copy of birth certificate;
·        Certified copies of relevant educational certificates and transcripts;
·        Study research plan (of about 750 words for Master’s and 1500 words for PhD applicants);
·        Medical certificate filled and stamped by registered medical practitioners in section 6 of the application form;
·        Certified copy of passport biodata page, if available;
·        For PhD applicants must provide evidence of support from the prospective supervisors from one of the Higher Education Institution(s) (HEIs) in Mauritius at the time of the application (the list of research themes/research interest can be obtained from the website of the different HEIs);
Qualification and Eligibility requirements.

 (i)Diploma programme.
Applicants must have either a minimum of five (5) credits at school certificate (S.C) or general Certificate of Education (G.C.E) O-level or international general Certificate of secondary Education(IGCSE) with a credit in English language.
·        The age limit for applicants should be above 18 years of age and should not reached 26 years by the closing date of application;
·        Should have TOEFL/IELTS (English Proficiency Test) certificate.

(ii) Undergraduate programme
    Applicants should have successfully completed Advance secondary school or Diploma and should satisfy the minimum pass should be division two at A-Level or Upper second for diploma award
·        The age limit for applicants should be above 18 years of age and should not reached 26 years by the closing date of application;
·        Should have TOEFL/IELTS (English Proficiency Test) certificate.

(iii) Master’s programme
Applicants should have successfully completed a Bachelor degree with at least an upper second class.
·        The age limit for applicants should not have reached 35 years;
·        Should have TOEFL/IELTS (English Proficiency Test) certificate.

(iv) Doctoral study programme
Applicant should have a master’s degree or equivalent in the relevant field.
·        The age limit for PhD   applicants should not have reached 45 years by closing date of application;
·        Should have TOEFL/IELTS (English Proficiency Test) certificate.

NB: Any document which is not in English or French Language must be submitted with a certified translation in one of the two languages (i.e English or French)

Kindly submit your applications to the undersigned address below not later than 15th April, 2019.

Permanent Secretary,
Ministry of Education, Science and Technology,
College of Business and Law,
University of Dodoma,
Registry Office Room No. J404,
P. O. Box. 10,
40479 DODOMA.

Jumatatu, 11 Machi 2019

SERIKALI IMEIMARISHA USIMAMIZI NA UDHIBITI WA MATUMIZI SALAMA YA TEKNOLOJIA YA NYUKLIA NCHINI



Serikali ya Tanzania kupitia Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC) imefanikiwa kuimarisha usimamizi na udhibiti wa matumizi ya Teknolojia ya Nyuklia nchini.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Tekenolojia Mheshimiwa William Ole Nasha wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa kimataifa wa waratibu wa miradi ya Sayansi na Teknolojia ya Nyuklia kutoka nchi 46 wanachama wa Shirika la Kimataifa la Nguvu za Atomiki (IAEA) unaofanyika jijini Arusha.
Mkurugenzi wa Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania, Profesa Lazaro Busagala akitoa taarifa na neno la ukaribisho kwa Wajumbe wa Mkutano wa Kimataifa wa Waratibu wa Miradi ya Sayansi na Teknolojia ya Nyuklia kutoka nchi 46 wanachama wa Shirika la Kimataifa la Nguvu za Atomiki (IAEA).
Naibu Waziri Ole Nasha amesema Shirika hilo linafadhili miradi mingi katika sekta mbalimbali hapa nchini ikiwemo sekta ya afya ambapo imewezesha kupatikana kwa vifaa mbalimbali vya uchunguzi wa tiba na maradhi ya saratani ambavyo vimefungwa katika hospitali ya Rufaa ya kanda ya ziwa, Bugando jijini Mwanza na Hospitali ya Ocean Road jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe William Ole Nasha (Kushoto) akifurahia jambo na Mkurugenzi wa Shirika la Kimataifa la Nguvu za Atomiki, Profesa Shaukat Abdulrazak katika Mkutano huo.
Pamoja na vifaa vya uchunguzi katika hospitali hizo mbili, pia taasisi nyingine mbalimbali zimepata vifaa vya maabara ambapo kwa ujumla wake vifaa vyote vina thamani ya kiasi cha Shilingi za Tanzania Bilioni 6.2 na pia kutoa mafunzo kwa wataalamu katika eneo la matumizi ya mionzi na teknolojia ya Nyuklia, mpango ambao uligharimu Shilingi za Tanzania Bilioni 3.3.

Mhe Ole Nasha amelishukuru na kulipongeza shirika hilo kwa kuendelea kuimarisha ushirikiano baina ya mataifa wanachama hususan kwa utaratibu wake wa kuwa na mikutano inayowezesha kubadilishana uzoefu baina ya wanachama.  Amewataka washiriki wa mkutano huo kuhakikisha wanafanya majadiliano yenye tija kwa lengo la kusaidia nchi zao kwenye udhibiti na matumizi salama ya teknolojia ya Nyuklia.

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe William Ole Nasha akitoa hotuba ya ufunguzi wa Mkutano wa kimataifa wa Waratibu wa miradi ya Sayansi na Teknolojia ya Nyuklia kutoka nchi 46 za Kanda ya Afrika, wanachama wa Shirika la Kimataifa la Nguvu za Atomiki (IAEA).

“Majadiliano yenu yalenge katika kuhakikisha mionzi na teknolojia ya Nyuklia katika Afrika inatumika vizuri kwa maendeleo,” alisema Ole Nasha.

Mheshimiwa Naibu Waziri ametumia nafasi hiyo pia kuwakaribisha sana washiki nchini Tanzania na kuwashauri kutembelea vivutio vya kitalii zikiwemo Mbuga za wanyama.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shirika la Nguvu za Atomiki Duniani (IAEA), Profesa Shaukat Abdulrazak amesema wataendelea kushirikiana na serikali ya Tanzania katika kuhakikisha kunakuwa na matumizi salama ya teknolojia ya Nyuklia kwenye sekta mbalimbali ikiwemo sekta ya Afya, Kilimo, Mifugo, Maji, Viwanda na Ujenzi.
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe William Ole Nasha akiwa katika picha ya pamoja na Washiriki wa Mkutano wa kimataifa wa Waratibu wa miradi ya Sayansi na Teknolojia ya Nyuklia kutoka katika nchi wanachama 46 wa Shirika la Kimataifa la Nguvu za Atomiki (IAEA).
Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania, Profesa Lazaro Busagala amesema taasisi yake imeendelea kudhibiti na kuwachukulia hatua za kuwafungia taasisi zinazokiuka taratibu za matumizi salama ya mionzi na teknolojia ya Nyuklia hapa nchini ikiwemo kutokuwa na leseni, kutokuwa na wafanyakazi wenye utaalamu wa matumizi ya mionzi na teknolojia ya Nyuklia na Mionzi.
 
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe William Ole Nasha akisalimiana na Waziri Msaidizi, anayeshughulikia Mashirika ya Nje katika Wizara ya Mambo ya Nje nchini Liberia, Mhe Yaba Freeman Thompson ambaye pia ni Mratibu wa mradi nchini humo na mshiriki katika Mkutano wa kimataifa wa Waratibu wa miradi ya Sayansi na Teknolojia ya Nyuklia Kanda ya Afrika mara baada ya ufunguzi wa Mkutano huo.
Akitoa mfano wa Hospitali amesema mwaka 2018 walifungia hospitali 112 zilizoshindwa kufuata masharti hayo, katika hizi tayari hospitali 40 zimekidhi na kufunguliwa huku hospitali 72 zikiwa bado zimefungiwa kutumia vifaa vinavyotumia mionzi.

Mkutano huo wa siku tano utamalizika tarehe15 Machi, 2019.