Jumamosi, 3 Agosti 2019

SERIKALI IMETOA MILIONI 100 KUJENGA BWENI LA WATOTO WENYE MAHITAJI MAALUM HALMASHAURI YA MJI GEITA

 Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imetoa kiasi cha shilingi milioni 100 kwa ajili ya ujenzi wa bweni la kisasa la wanafunzi katika kituo cha watoto wenye mahitaji maalum katika shule ya msingi Mbugani iliyopo katika halmashauri ya Mji Geita.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Wiliam Ole Nasha wakati wa ziara ya kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa na wizara mkoani Geita ambapo amesema fedha hizo zimetolewa ikiwa ni sehemu ya kuboresha elimu nchini.
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha akikagua maendeleo ya ujenzi wa bweni la watoto wenye mahitaji maalum katika kituo Maalum cha Shule ya msingi Mbugani iliyopo mkoani Geita.
Ole Nasha amesema serikali ya Awamu ya Tano inatambua umuhimu wa kuwajengea fursa na mazingira mazuri ya kusoma watoto wenye mahitaji maalum na ndio maana imeweka mkazo katika kuhakikisha kwamba kunapatikana walimu wa kutosha, vifaa vya kufundishia na kujifunzia  pamoja na vitabu ili kuwawezesha kusoma bila vikwazo vyovyote kutokana na changamoto zao za kimaumbile.

“Kwa miaka mingi jamii nyingi zimekuwa zikiwatenga watoto wenye mahitaji maalim, lakini kwa sasa nashukuru tumeendelea kuwawezesha kupata haki yao ya Elimu kama walivyo watoto wengine na kwamba wanaweza kuwa na changamoto za kimaumbile lakini ubinadamu wao upo palepale” amesema Waziri Ole Nasha.
 
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha akizungumza na watoto wenye mahitaji maalum (Hawapo Pichani)  baada ya kukagua ujenzi wa bweni la Kituo cha Watoto wenye mahitaji Maalum cha Shule ya msingi Mbugani iliyopo mkoani Geita.
Amewataka wanafunzi hao wenye mahitaji maalum kutokatishwa tamaa na changamoto walizonazo za kimaumbile kwani serikali imewawekea mazingira ya kuwawezesha kufika mbali zaidi katika Elimu na kuwataka kuendelea kutumia fursa hizo za kielimu ili kutengeneza maisha yao ya baadaye.

 
“Wanafunzi, mtu hawezi kujua kipaji chako ni kipi lakini serikali inakupa fursa ya kuonyesha kipaji chako, Mhe Rais ametambua uwezo mkubwa wa watu wenye mahitaji maalum na ndio maana siku hizi tunae Naibu Waziri anayeshughulika na watu wenye mahitaji maalum ambaye naye ana changmoto ya ulemavu,” amesema Naibu Waziri.
 
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia akicheza na watoto wenye mahitaji maalum katika kituo cha Watoto wenye mahitaji maalum cha shule ya msingi Mbugani, Waziri huyo yupo mkoani Geita kwa ziara ya siku mbili ya kukagua miradi ya maendeleo ya sekta ya Elimu

Awali Mwlimu Mkuu wa Shule ya msingi Mbugani Edwicka Ndunguru
  amemweleza Naibu Waziri kuwa  kituo hicho kilijengwa kwa lengo la kuwawezesha wanafunzi wenye mahitaji maalum kupata haki ya kielimu katika mazingira wezeshi na kuwapa fursa wengi zaidi wenye mahitaji maalum wanaoishi mbali na shule zinazotoa elimu maalum kupata elimu.

Amesema mafanikio ya kuwepo kwa vituo vya watoto wenye mahitaji maalum mbali na kuwawezesha kupata haki yao ya kielimu, pia imewasaidia kujifunza ujuzi mbalimbali, jamii imetambua nakuthamini umuhimu wa wanafunzi wenye mahitaji maaluma kupata Elimu na wengine kufanikiwa kupata kazi katika maeneo mbalimbali.
 
Sehemu ya bweni lilojengwa na serikali katika Kituo cha watoto wenye mahitaji maalum katika shule ya msingi Mbugani iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Geita Mkoani Geita

“Wanafunzi wenye mahitaji maalum wanapomaliza hapa wanakua na ujuzi katika fani za ushonaji, ufumaji na useremala, fani hizi zimewezesha baadhi kuajiriwa katika maeneo mbalimbali na wengine kujiajiri” amesemu mwalimu Ndunguru.

 
Kituo hicho chenye vitengo vinne vyenye jumla ya wanafunzi 143 ambavyo ni vitengo vya ulemavu wa akili, Viziwi, ulemavu wa viungo na ulemavu wa macho, mbali ya kuhudumia wanafunzi hao wenye uwezo wa kufika shuleni lakini pia vinahudumia watoto 38 wenye ulemavu wa kiwango cha juu ambao hawawezi kufika shuleni.




Ijumaa, 2 Agosti 2019

MAONESHO YA WANASAYANSI WATAFITI WACHANGA

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako  amesema Serikali inatambua umuhimu wa Sayansi Teknolojia na Ubunifu ktk maendeleo ya taifa letu na hivyo itaendelea kusimamia na kuendeleza wanasayansi wabunifu  nchini.
Amesema hayo wakati wa ufunguzi wa maonesho ya tisa ya wanasayansi watafiti wachanga nchini yanayoandaliwa na taasisi ya Young Scientists Tanzania, (YST) jijini Dar Es Salaam
Maonesho hayo huwahusisha wanasayansi wanafunzi kutoka shule za sekondari kote nchini , kuonesha tafiti walizofanya kupitia mpango wa YST. 
Ndalichako amewapongeza wanafunzi walioshiriki kwa kuonesha tafiti zilizofanywa kisayansi na ubora na pia kwa kutumia teknolojia katika kubuni mambo mbalimbali  na mifumo inayotoa utatuzi wa  changamoto za jamii yetu. 
Amepongeza walimu wanaoshiriki katika mpango huo kwa kuweza kutoa hamasa kwa wanafunzi kupenda masomo ya sayansi na hisabati na kwa kufundisha vizuri hali ambayo inajionesha kupitia kazi bora za wanafunzi wao.


  










Ijumaa, 26 Julai 2019

TAARIFA KWA UMMA


UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
MINISTRY OF EDUCATION, SCIENCE AND TECHNOLOGY


PARTIAL SCHOLARSHIPS TENABLE IN MOROCCO FOR THE ACADEMIC YEAR 2019/2020
Call for Application
The General Public is hereby informed that the Kingdom of Morocco through the Moroccan Agency of International Cooperation (AMCI), has granted a scholarship programme to eligible Tanzanian Nationals to pursue  Undergraduate and Postgraduate  studies  at Moroccan Public Institutions for the academic year 2019/2020.
A directory of Training Institution is available on the website of AMCI through  www.amci.ma containing a complete list of the Moroccan Public Institutions of Higher Education as well as specific information about them, including the conditions of access, the subjects and the duration of the studies.
General Admission Requirements  
(i)        Undergraduate Studies
(a)   Bachelor Degree
1.      Applicant must have completed Advanced Certificate of Secondary Education Examination (ACSE) in 2018-2019 and pass with Division I or II / Diploma with minimum of Upper Second Class;
2.      Age not older than 23 years by August 2019;
3.      Not  admitted in any Higher Learning Institution in the country; and
4.   Medical Certificate issued by public medical hospitals certifying that
     your are not suffering from any contagious illness or carrying a   
     pandemic.

(ii)              Postgraduate
(a)   Masters:
1.      Must be holders of a first degree with a minimum of Upper Second Class;
2.      Not admitted in any Higher Learning Institution; and
3.      Medical Certificate issued by public medical hospitals certifying that
      your are not suffering from any contagious illness or carrying a   
      pandemic.

(b)  PhD
            1.      Must be holders of Master’s degree in the required subject/specialties   
                        of studies recognized as being equivalent to Moroccan granted    
                        certificate;
           2.      Not admitted in any Higher Learning Institution;
           3.      Medical Certificate issued by public medical hospitals certifying that
      your are not suffering from any contagious illness or carrying a   
      pandemic.

NB:
·         Applicants with a certificate  level of training  in French language will have            an added advantage;
·         For all programmes  the language of instruction is French except for Islamic           and Arabic Literature which will be conducted in Arabic Language;
·         Application forms can be downloaded at: http://www.amci.ma/fcf.pdf
·         There is no Loan or grant  from the Goverment of Tanzania  for candidates          who will be offered this Scholarship.

       List of documents to be submitted include:
      Two (02) copies of
  1. Completed filled application forms;
  2. Certified true copy of academic certificates, transcripts, birth certificate;
  3. Certified true copy of passport;
  4. Medical certificate issued by public medical hospitals certified that he/she is not suffering from any contagious illness or carrying a pandemic;
  5. Two recent passport size photographs, in colour, (with the name, surname and nationality of the candidate written on the back of the photos); and
  6. Applicant for Masters and PhD must provide a copy of an Abstract of dissertation/thesis of graduation/thesis for PhD degree.
     The scholarship will cover
(a)   (i) Monthly allowance of 750 Dirhams (Approximate to U.S $ 75);
(ii) Tuition fees;

(b)   Other costs will be covered by Applicant (Student)
(i)                 Accommodation;
(ii)              Registration fees; and
(iii)            Air ticket, go and return.
 
 Medical coverage:
Foreign students are required to subscribe to an insurance policy during their study stay in Morocco that offers them the following services:
      ·         Reimbursement of medical expenses;
      ·         Medical care;
      ·         Final medical evacuation to home country in cases of serious illness that will not allow           students to continue with their studies in Morocco; and
      ·         Repatriation of body in case of death in Moroccan territory.

For further information on the scholarships consult the websites: www.enssup.gov.ma  or www.men.gov.ma   or  www.ma2e.com  

Mode of Application 
The application shall be submitted in hard copy to reach the undersigned not later than 5th August, 2019 to:

Permanent Secretary,
Ministry of Education, Science and Technology,
University of Dodoma,
College of Business and Law,
Block 10,
P.O. Box 10,
40479 DODOMA
Room 404

TAARIFA KWA UMMA


UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
MINISTRY OF EDUCATION, SCIENCE AND TECHNOLOGY

SCHOLARSHIPS TENABLE IN THE PEOPLE’S DEMOCRATIC REPUBLIC OF ALGERIA FOR ACADEMIC YEAR 2019/2020

Call for Applications
The General Public is hereby informed that, the People’s Democratic Republic of Algeria  has granted a Scholarship programme to eligible Tanzanian Nationals to pursue Undergraduate studies at Universities in Algeria for the academic year 2019/2020 in the following field categories:

Category A. Higher Education
      1.      Medicine;
      2.      Technical Sciences;
      3.      Science of Matter;
      4.      Mathematics and Computer;
      5.      French;
      6.      Science of Nature and Life; and
      7.      Earth Science and the Universe.

Category B. Religious Affairs and Academic
1.         Imam preacher and/or Quran teacher;
2.         Bachelor degree (Licence) in Imamat.

Application Requirements
1.      Must have completed Advanced Secondary School or Diploma in 2017-2018;
2.      Will be not more than 25 years of age by October, 2019;
3.      Medical Examination Certificate from a Public Hospital; 
4.  Have a good knowledge of the Holy Quran for Imam Preacher/or Koran teacher applicants;
           5.    Have a good knowledge of the Holy Quran for Bachelor degree in Imamat 
            applicants.

Application Package
  §      Certified copies of;
-         Certificate of Secondary Education Examination (CSEE);
-         Certificate of Advanced Secondary Education Examination (ACSEE) or Diploma Certificates (Academic Certificates and Transcripts);
-         Birth Certificates;
  §      Application letter (with your contacts; telephone number and email address); and
     §    Medical Examination Certified by a Public Hospital;

NB:
     ·        Selected applicants will undergo one year for French language before commencing undergraduate degree studies.
     ·        There is no Loan or grant  from the Government of Tanzania  for candidates who will be offered this Scholarship.

Mode of Application
All applicants should submit their application packages to reach the undersigned  not later than 1630Hrs on 10th August 2019 to:

Permanent Secretary,
Ministry of Education, Science and Technology,
University of Dodoma (UDOM)
Business School,
Block 10,
40479 DODOMA.

Jumamosi, 20 Julai 2019

WAZIRI NDALICHAKO ATAKA USIMAMIZI THABITI UDAHILI WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU


Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako ametoa wito kwa Viongozi wa Elimu ya juu nchini kuhakikisha wanasimamia ipasavyo mchakato wa udahili wa wanafunzi wa elimu ya juu kwa mwaka wa masomo 2019/20 ili kuondoa usumbufu usiokuwa wa lazima kwa wanafunzi, wazazi, walezi na wafadhili wa wanafunzi hao.

Waziri Ndalichako ametoa wito huo Jijini Dar es Salaam wakati akifunga maonesho ya 14 ya elimu ya juu yaliyofanyika katika viwanja vya Mnazi ambayo yalikuwa na kauli mbiu isemayo Jukumu la Taasisi za Elimu ya Juu Katika Kuzalisha Ujuzi Unaohitajika kwa ajili ya Viwanda.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akipata maelezo ya programu zinazotolewa na Chuo Kikuu Dodoma wakati wa maonesho ya 14 ya elimu ya Juu yalivyofanyika katika viwanja vya Mnazi mmoja Jijini Dar es Salaam.
Katika hotuba yake amesema asingependa kuona changamoto zilizotokea mwaka jana katika kujiunga na vyuo zinajirudia kwani changamoto nyingine zilisababishwa na Vyuo vyenyewe kutokuwa na mifumo thabiti ambayo wanafunzi wangeweza kufanya maombi na kujithibitisha katika vyuo kwa urahisi.

“Nafahamu kwamba TCU wameshatoa mafunzo na maelekezo ya kutosha kwa wataalamu wa mifumo ya kompyuta na maafisa udahili wa vyuo vyote ambao mnadahili wanafunzi kwa mwaka wa masomo 2019/20 kwa hiyo naamini kwamba zoezi la udahili kwa mwaka huu litafanyika kwa ufanisi zaidi kuliko ilivyokuwa mwaka jana,” alisema Waziri Ndalichako.

Waziri Ndalichako  alisistiza kuwa kwa mujibu wa sheria ya vyuo vikuu sura ya 346 ya sheria za Tanzania jukumu la kudahili wanafunzi ni la Seneti za Vyuo Vikuu au Bodi ya za Chuo husika, hivyo amewataka Viongozi wa Vyuo kutumia mamlaka ya Seneti za Vyuo Vikuu au Bodi kuhakikisha kuwa wanasimamia kikamilifu udahili wa wanafunzi ili waweze kujiunga kwa urahisi huku akisistiza pia  vigezo, masharti, taratibu na sifa za mwanafunzi kujiunga na chuo kuzingatiwa.

“Niwakumbushe tu  Serikali iko macho, katika mchakato wa udahili msipofuata taratibu mkaweka watu wasio kuwa na sifa tutawaondoa lakini kumbukeni na ninyi mloiwaingiza hamtabaki salama, hakikisheni zoezi hilo linafanyika kwa ufanisi,”aliongeza Waziri Ndalichako.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akipata maelezo katika banda la DIT wakati wa maonesho ya 14 ya elimu ya Juu yaliyofanyika katika viwanja vya Mnazi mmoja Jijini Dar es Salaam


Sambamba na hilo amewataka wanafunzi wanaotarajia kujiunga na masomo ya elimu ya juu kutokuwa wavivu wa kusoma maelekezo kabla ya kuanza kujiunga ama  kuchagua kozi katika vyuo. Amewaasa kuzingatia sifa zinazohitajika kwa kulinganisha ufaulu wao wakati wa kuchagua kozi huku akisistiza kuwa Serikali haina utaratibu wa kumpangia mwanafunzi programu ya kusoma isipokuwa inachagua mwanafunzi kutokana na sifa alizonazo katika kozi husika.

Katika hatua nyingine Waziri Ndalichako amezitaka Taasisi za Elimu ya juu na Vyuo vikuu kuendelea kujitathmini ni kwa kiasi gani  tafiti ambazo wamekuwa wakizifanya zinagusa moja kwa moja jamii na kusaidia kutatua changamoto mbalimbali  zilizopo katika jamii.

“Ninyi Taasisi za Elimu ya Juu macho yenu na masikio yawe wazi kila mara ili muweze kusikiliza wapi katiika jamii kuna changamoto na kwa kutumia utaalamu wenu mshiriki kuzitatua, kumbukeni elimu ya juu katika nchi yoyote ile ndio kitovu cha maarifa hivyo muendelee kutumika katika kutatua changamoto hizo,” aliongeza waziri Ndalichako.

 Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akizungumza na baadhi ya wanafunzi waliofika katika viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam kutembelea maonesho ya 14 ya elimu ya juu.

Akizungumza kwa niaba ya washiriki wa maonesho Profesa Uswegi Minga Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Tumaini amesema uwepo wa maonesho hayo umetoa nafasi ya vyuo vyenyewe kujitangaza kuhusu fursa zinazopatikana katika vyuo vyao, lakini pia imekuwa nafasi nzuri ya kubadilishana uzoefu  kutokana na kujifunza namna vyuo vingine vinavyofanya kazi hivyo kusaidia kufanya maboresho katika maeneo ya uendeshaji wa Vyuo lakini pia katika upangaji na ufundishaji wa programu mbalimbali.

Maonesho ya 14 ya Vyuo vya Elimu ya Juu yameandaliwa na Tume ya Vyuo Vikuu nchini na kwa mwaka huu yamekuwa na washiri zaidi ya 80 vikiwemo kutoka nje ya nchi na vile vyaTanzania.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akigawa cheti kwa moja ya Taasisi ambayo imeshiriki katika maonesho ya 14 ya elimu ya ju. Maonesho hayo yamefanyika  katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Da res Salaam.