Waziri
Mkuu, Mhe. Kayanza Peter Mizengo Pinda (MB) ametembelea na kukagua Mradi
wa Sayansi, Teknologia na Elimu ya Juu
katika Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine Mkoani Morogoro, na kujionea maendeleo ya
utekelezaji wa mradi huo chuoni hapo.
Mhe,
Waziri Mkuu amefanya ziara hiyo jana, ambapo alipata nafasi ya kujionea majengo
matatu, vifaa vya kisasa vya kujifunzia na kufundishia katika maabara za chuo
pamoja na kupata nafasi ya kuongea na wanajumuiya ya chuo wakiwemo waliopata
ufadhili wa mafunzo kutoka katika mradi huo.
Mradi
wa Sayansi, TeknoloJia na Elimu ya Juu katika
chuo Kikuu cha Sokoine umejenga jengo la ghorofa mbili kwa ajili ya
idara ya Uchumi kilimo na biashara, jengo la ghorofa moja katika idara ya
uandisi kilimo na Mipango Ardhi. Pia imejenga maabara ya kisasa ya Zoolojia.
Aidha,
mradi umewezesha kuanzishwa kwa mitaala mipya miwili ya Shahada ya Uzamili
katika uhakiki wa ubora na Usalama wa Chakula na Mtaala mwingine ni ule wa
Uhandisi na Usimamizi wa Uchakataji mazao baada ya kuvunwa.
Makamu
Mkuu wa Chuo Bw Gerald Monella, alisema mradi huo umesaidi kupatika kwa ofisi
za wahadhiri na wafanyakazi wengine wa Chuo, kufadhili wahadhiri 21 katika
mafunzo Uzamili na Uzamivu, ujenzi wa miundombinu ya madarasa na maabara pamoja
na ununuzi wa vifaa vya maabara na TEHAMA.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
Zingatia: Mwanachama wa blogu hii tu ndiye anayeweza kuchapisha maoni.