Wizara   ya Elimu na Mafunzo  ya 
Ufundi imeendeleza ubabe katika mchezo wa mpira miguu  baada ya Timu yake ya Elimu  Sport kuibuka na ushindi wa kwanza na  kutwaa kombe ikiwa ni mara ya tatu mfululizo
katika Mashindano ya 34 ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali
(SHIMIWI) 2014 .
Katika Ushindi
huo Elimu Sport ilipambana na Vilabu 60 vya 
Wizara na Idara za Serikali mbalimbali, na kufanikiwa kufikia fainali
anbapo ilishindana na timu ya Wizara ya Uchukuzi na kuwashinda kwa mabao 5 – 3
na kupelekea ushindi huo.
 Aidha, Elimu Sport  ilishiriki michezo mingine ambapo katika
mchezo wa  kurusha  vishale  
(Darts) iliibuka  mshindi wa  pili na kuibuka na   kikombe. Katika mchezo wa Riadha  Mita 
mia  moja   kwa upande wa  wanaume 
imepata  medali ya  Fedha baada ya kuibuka mshindi wa pili.


Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
Zingatia: Mwanachama wa blogu hii tu ndiye anayeweza kuchapisha maoni.