Serikali
ya China imekabidhi vitendea kazi kwa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia
kwa ajili ya kuwezesha wizara kufanya kazi kwa weledi. vifaa hivyo
vilikabidhiwa kwa Naibu Katibu Mkuu Prf. Saimon Msanjila ofisini kwake na Liu Yun
Akizungumza
wakati wa makabidhiano hayo Liu Yun alimwelezea Naibu Katibu Mkuu kuwa
wanajisikia faraja kubwa kukabidhi vifaa hivyo kwa wizara kwani China na
Tanzania zimekuwa zikishirikiana kwa karibu sana katika sekta ya elimu hasa
katika upande wa elimu ya juu.
Vitendea
kazi vilivyokabidhiwa ni pamoja na Dell desk compture 6, mashine ya kudurufu
moja, scanner moja, video camera moja na komputa mpatako 10 vyote vikiwa na
thamani ya zaidi ya shilingi milioni ishirini na tano
Ushirikiana
huo umewezesha serikali hizi mbili kuweza kubadilishana wanafunzi wa elimu ya
juu katika fani mbali mbali. Pia alimuelezea uanzishwaji wa mafunzo ya lugha ya
kichina katika vyuo vikuu vya Dodoma na Dar es Salaam ambapo alisema hii ni
ishara tosha ya ushirikiano uliotukuka.
Naye
Naibu Katibu Mkuu alimshukuru Yun kwa msaada huo wa vitendea kazi ambapo
alimuahidi kuwa vitafanyia kazi iliyokusudiwa na kuhakikisha kwamba inaongeza
ufanisi katika kuwahudumia wananchi wanaofika ofisi hapo kupata huduma
mbalimbali za kielimu.
Baadhi ya vtendea kazi vilivyotolewa na serikali ya China kwa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa ajili ya kuboresha na kurahisisha utendaji kazi wa watumishi
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Simon Msanjila akiongea na Mwakilishi wa Serikali ya China Liu Yun wakati wa makabidhiano ya vitendea kazi
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Simon Msanjila na Mwakilishi wa Serikali ya China Liu Yun wakiweka saini makubaliano ya kupokea vifaa vilivyotolewa na China wakati wa makabidhiano ya vitendea kazi
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
Zingatia: Mwanachama wa blogu hii tu ndiye anayeweza kuchapisha maoni.