Waziri
Ndalichako ameyasema hayo wakati akizungumza na wananchi wa halmashauri ya
Mbulu iliyopo mkoani Manyara ambapo amesema ni kweli serikali inahitaji ziwepo
shule nyingi ambazo zinavigezo, siyo kuwa na shule ambazo hazina vigezo.
"Shule
za nyasi katika Serikali hii ya awamu ya tano zitabaki kuwa historia kwa kuwa
serikali inajenga na kuboresha miundombinu ya kujifunzia na ile ya kufundishia,
sasa ili shule isajiliwe lazima iwe imekidhi vigezo siyo bora shule bali
tunahitaji shule zilizobora na zenye viwango vinavyokubalika" amesema
Waziri Ndalichako.
Waziri
Ndalichako amesema kazi ya usajili ni nyepesi sana ambayo haichukui
muda mrefu endapo vigezo vinakuwa vimetimia, lakini kazi kubwa ni
kuhakikisha miundombinu bora inayokubalika inakuwepo ili shule iweze
kusajiliwa.
Hivyo
amewasihi wadau wote wa Elimu kuhakikisha shule zinapojengwa zinazingatia na
kukidhi vigezo kabla ya kusajiliwa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
Zingatia: Mwanachama wa blogu hii tu ndiye anayeweza kuchapisha maoni.