Naibu
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha ameiagiza Tume ya
Nguvu za Atomiki kuhakikisha inaweka vituo vya ukaguzi wa viwango vya mionzi
kwa bidhaa zote zinazoingia na kutoka nchini katika mipaka yote kwa lengo la
kudhibiti mionzi katika bidhaa hizo.
Naibu
Waziri ametoa rai hiyo jijini Arusha alipotembelea Tume hiyo ili kujionea jinsi
inavyofanya kazi, ambapo amesema ni muhimu vituo hivyo kuwekwa katika
mipaka ili kuhakikisha bidhaa zinazoingia na kutoka nchini zinakuwa
na viwango vya mionzi inayokubalika kimataifa.
Naibu
Waziri Ole Nasha ameitaka Tume hiyo kutokuishia katika kutekeleza majukumu ya
kudhibiti na kuhamasisha matumizi bora ya mionzi bali inapaswa kuanza kuangalia
namna bora ya kuhamasisha matumizi chanya ya nyuklia kwa maendeleo ya taifa
katika nyanja za Afya, Kilimo, maji na teknolojia.
Naibu
Waziri Nasha pia alitembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa
maabara ya kisasa kwa ajili ya upimaji wa ubora wa vifaa mbalimbali vya mionzi
ikiwemo vifaa tiba vya Tume hiyo, maabara hiyo inajengwa na fedha za serikali
kiasi cha shilingi bilioni mbili.
Kwa
upande wake Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya nguvu za Atomiki Brigadia Jenerali
Fulgence Msafiri amesema kutokana na upungufu mkubwa wa watumishi walio na
weledi katika Teknolojia ya nyukulia imefanya Taasisi hiyo kukosa
watumishi kutokana na kuanzishwa kwa vituo vya kudhibiti uingizwaji wa bidhaa
katika mipaka ya Rusumo, Mtukula, Kabanga, Kigoma,
Tunduma, Kasumulu na Daraja la Mkapa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
Zingatia: Mwanachama wa blogu hii tu ndiye anayeweza kuchapisha maoni.