Waziri
wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako amesema Mipango
ya Taifa haliwezi kufanikiwa bila kuwa na vijana waadilifu,wachapakazi na wenye
hofu ya mungu hivyo amewataka vijana kuzingatia masomo ili kuweza kufikia
malengo yanayikusudiwa Katika Taifa.
Waziri
Ndalichako amesema hayo mwishoni mwa wiki wakati wa ibada maalumu iliyifanyika
katika kanisa la City Christian Center lililopo Upanga Jijini Dar es Salaam ambapo
amesema ili mtu yeyote afanikiwe katika maisha lazima hofu ya mungu iwepo
katika maisha ya kila siku.
Waziri
Ndalichako amesema vijana wengi wamekuwa wakitumia muda wao mwingi kufanya
mambo ambayo siyo msingi wa maisha kama vile kujiingiza kwenye makundi ya
utumiaji wa dawa za kulevya, uporaji, unywaji wa pombe vitendo ambavyo havina
faida na matokeo yake ni kijana kuangamia.
Kwa
upande wake Askofu Mkuu wa Kanisa hilo la City Christian City Dkt. Reinwell
Mwenisongole amepongeza juhudi zinazofanywa na serikali UA awamu ya Tano katika
kusimamia Elimu ikiwa ni pamoja na kuongeza udahili katika vyuo vikuu, kujenga
na kuboresha miundombinu ya vyuo vikuu kwa lengo la kusaidia kuongeza wataalamu
ili kutimiza azma ya serikali ya kufikia uchumi wa viwanda.
Askofu
Mwenisongole amesema kanisa la kanisa la Christian Center lilianzishwa mwaka
1978 kwa lengo la kuwasaidia vijana kuwa na hofu ya mungu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
Zingatia: Mwanachama wa blogu hii tu ndiye anayeweza kuchapisha maoni.