Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce
Ndalichako amewataka Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) kuhakikisha
inakamilisha ukarabati wa shule za Jangwani na Azania kabla ya Januari
22, mwaka huu ili kuwezesha masomo kuanza.
Waziri Ndalichako ametoa agizo hilo leo jijini Dar es
Salaam alipofanya ziara ya kukagua Maendeleo ya ukarabti wa
shule hizo.
Waziri ndalichako amesema ameridhishwa na namna
ukarabati wa shule hizo unavyofanyika, licha ya kuwa bado kuna kazi kubwa
ambayo bado haijafanyika.
Waziri ameitaka TBA kuhakikisha wanakamilisha miundombinu muhimu
mapema ikiwemo madarasa, mabweni, na vyoo ili kuwawezesha wanafunzi kuanza
masomo kabla ya januari 22, mwaka huu.
Kwa upande wake
Msanifu Majengo Cecilia Muhongo wa TBA amesema wamejipanga kuhakikisha
ukarabati wa miundombinu muhimu itakayowawezesha wanafunzi kuanza
masomo inakamilika mapema.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
Zingatia: Mwanachama wa blogu hii tu ndiye anayeweza kuchapisha maoni.