Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce
Ndalichako amemuagiza Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Afya na Tiba
Shirikishi Muhimbili- MUHAS kumsimamisha kazi Mkuu wa Kitengo cha Manunuzi wa Chuo
hicho.
Waziri Ndalichako amtoa agizo hilo alipofanya ziara katika Chuo
hicho jijini Dar es Salaam ambapo amesema Mkuu wa Kitengo hicho Nuru Mkali
amekuwa akikuka taratibu za manunuzi na kupelekea kuwepo Kwa ufisadi mkubwa wa
fedha za serikali.
Aidha, amemtaka Mwenyekiti wa baraza la Chuo hicho Mariam
Mwafisi kupitia mikataba yote ya manunuzi kwa miaka mitatu ili kuona watu wote
walioshiriki katika mchakato huo mbovu wa manunuzi na endapo itabainika basi
hatua za kisheria zichukuliwe.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa baraza la Chuo hicho Mariam
Mwafisi amesema wamepokea maelekezo na watayafanyia kazi ikiwemo
kumsimamisha kazi Mkuu wa Kitengo cha Manunuzi.
Akiwa katika Chuo cha Taaluma na Tiba kilichopo Mloganzila
nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam Waziri Ndalichako amemuagiza Makamu Mkuu wa
Chuo hicho anaeshughulikia huduma za Hospitali katika kampasi hiyo Said
Abood kuhakikisha anawatembelea wagonjwa kwa lengo la kutatua changamoto
zinazowakabiki pindi wanapokuwa hospitalini hapo.
Prof Ndalichako pamoja na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii,Jinsia Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile wamefanya
ziara katika hositali hiyo ili kujionea changamoto mbalimbali na namna
bora ya kuzipatia ufumbuzi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
Zingatia: Mwanachama wa blogu hii tu ndiye anayeweza kuchapisha maoni.