Naibu Waziri wa Elimu
Sayansi na Teknolojia Mheshimiwa William Ole Nasha ameahidi atashughulikia
changamoto zinazokikabili Chuo Kikuu cha Mwalimu Julius K. Nyerere cha Kilimo
na Teknolojia (MJNUAT) ili kukiwezesha Chuo hicho kuanza kudahili wanafunzi.
Naibu waziri Ole Nasha
ametoa ahadi hiyo alipofanya ziara ya kukagua shughuli za Maedeleo
zinazofanyika katika Chuo hicho kilichopo Wilayani Butiama mkoani Mara.
Ole Nasha amesema Chuo
hicho kilianzishwa si tu kwa lengo la kumuenzi Baba wa Taifa Mwalimu Julius K.
Nyerere lakini pia kuendeleza dhamira yake ya dhati aliyokuwa nayo kuhusu
kilimo.
Akiwa Chuoni hapo Naibu Waziri
huyo amebaini kuwepo kwa baadhi ya Watumishi wa Wizara yake wanaosaidia
mchakato wa watumishi wa Chuo Kikuu cha Mwalimu Nyerere kuhama kwa madai kuwa
katika Chuo hicho hakuna kazi za kufanya jambo ambalo linazidi kurudisha
nyuma juhudi za Serikali za kuhakikisha kuwa Chuo hicho kinaanza kazi mapema
iwezekanavyo.
Kwa upande wake Makamu
Mkuu wa Chuo hicho Profesa Dominick Kambarage amesema Chuo hicho
kimeshindwa kuanza kazi kutokana na kukosa Miundombinu inayokidhi vigezo vya
Tume ya Vyuo Vikuu.
Awali kabla ya kutembelea
Chuo Kikuu hicho Naibu Waziri huyo alitembelea Shule ya Msingi
Mwisenge, Shule ambayo amesoma hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius K. Nyerere
ambapo akiwa shuleni hapo aliahidi kuwajengea vyumba vitatu vya madarasa.
Naibu Waziri wa Wizara ya
Elimu, Sayansi na Teknolojia Mheshimiwa William Ole Nasha akifuatilia namna
Wanafunzi wa darasa la Tatu katika Shule ya Msingi Mwisenge wanavyopata Elimu
kupitia Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, TEHAMA
Naibu Waziri wa Elimu,
Sayansi na Teknolojia Mheshimiwa William Ole Nasha akiwa amekaa kwenye dawati
ambalo hayati Baba wa Taifa Mwalimu Jullius Kambarage Nyerere aliwahi Kukalia
dawati hilo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
Zingatia: Mwanachama wa blogu hii tu ndiye anayeweza kuchapisha maoni.