Waziri wa Elimu, Sayansi na
Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako Leo ametembelea na kukagua hatua za mwisho za
usimikaji wa vifaa mbalimbali ndani ya maabara ya kisasa ya Kuhakiki
vifaa vinavyopima mionzi katika Tume ya nguvu za Atomiki- TAEC
iliyopo mkoani Arusha.
Akizungumza mara baada ya
kutembelea maabara hiyo Waziri Ndalichako amesema serikali imejenga
maabara hiyo ya kisasa ili kudhibiti masuala ya mionzi kwa nchi za Afrika.
Waziri wa
Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akipokea maelezo
kuhusu usimikaji wa vifaa vya kisasa katika maabara ya nyuklia kwenye Tume ya
nguvu za Atomiki iliyoko mkoani Arusha.
Alisema maabara hiyo ambayo sasa
ipo katika hatua za kufungwa vifaa mbalimbali vya kisasa itawezesha nchi
mbalimbali kuja kujifunza namna ya kupima masuala mbalimbali ya mionzi.
Waziri Ndalichako
amesema kuwa hadi sasa serikali imeshatoa kiasi cha sh. bilioni
2.38 huku Umoja wa Ulaya (EU) ikitoa vifaa vyenye thamani ya
sh. bilioni 11.
Waziri wa
Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako akiangalia kwa karibu
moja ya kifaa kilichosimikwa kwa ajili ya upimaji wa mionzi kwenye maabara ya
kisasa ya nyuklia kwenye Tume ya nguvu za Atomiki, TAEC mkoani Arusha.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
Zingatia: Mwanachama wa blogu hii tu ndiye anayeweza kuchapisha maoni.