Naibu Katibu Mkuu Wizara ya
Elimu, Sayansi na Teknolojia Dk. Ave Maria Semakafu leo amekutana na kufanya
mazungumzo na ujumbe kutoka UNICEF kwa lengo la kujengeana uelewa wa pamoja juu
ya kile wanachokitekeleza kuhusuiana na Sekta ya Elimu.
Mazungunzo hayo yamefanyika
katika ukumbi wa Mikutano wa Wizara Jijini Dodoma ambapo wote kwa pamoja
wamekubaliana kuimarisha mawasiliano ili kuwezesha utekelezaji wa majukumu
katika sekta hiyo.
Naibu Katibu Mkuu wa
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dk. Avemaria Semakafu akisisitiza jambo
wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Timu ya Ujumbe kutoka UNICEF juu ya
namna bora ya kutekeleza majukumu ya kielimu katika Sekta hiyo.
Shirika la Kimataifa la
kuhudumia watoto UNICEF wanatekeleza shughuli za kielimu katika mikoa ya Mbeya,
Iringa, Njombe, Songea, Kigoma na Tabora kwa kutoa mafunzo kwa waratibu Elimu
Kata, mafunzo kwa walimu kazini kuhusu Elimu Jumuishi, lishe, uongozi na
utawala kwenye Elimu.
Kikao hicho pia kimejumuisha
wajumbe kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dk. Avemaria Semakafu
na Timu ya Ujumbe kutoka UNICEF, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za
Mitaa (TAMISEMI) wakiwa katika mazungumzo ya namna bora ya kutekeleza shughuli
za kielimu za Sekta hiyo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
Zingatia: Mwanachama wa blogu hii tu ndiye anayeweza kuchapisha maoni.