Waziri
wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako amezitaka Taasisi za Elimu
ya Juu nchini ambazo matokeo ya uhakiki yalibainisha kuwa na mapungufu
kurekebishe kasoro hizo kama walivyoelekezwa na Mamlaka husika.
Waziri
Ndalichako ametoa agizo hilo Leo Jijini
Dar es Salaam wakati wa ufunguzi wa
Maonesho ya kumi na tatu ya Elimu ya Juu ambapo amesema taasisi hizo
zisipofanya hivyo basi hatua stahiki zitachukuliwa, ikiwa ni pamoja na kufutiwa
usajili.
Waziri wa Elimu, Sayansi na
Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akizungumza na wadau wa Elimu ya Juu (hawapo
pichani) ambao wanashiriki katika maonesho ya kumi na tatu ya Elimu ya Juu wakati
wa ufunguzi wa maonesho hayo yanayofanyika katika viwanja vya Mnazi mmoja
Jijini Dar es alaam ambapo amezitaka Taasisi zote za Elimu nchini kuzingatia
ubora wa Elimu wanayoitoa.
Waziri Ndalichako pia amewaagiza Tume ya Vyuo Vikuu
nchini (TCU) na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) kuendelea kusimamia
kwa karibu na kwa umakini masuala yote
yanayohusu ubora wa Elimu inayotolewa na Taasisi za Elimu ya Juu.
”
Katika Awamu hii ya Tano watu wanaofanya kazi kwa mazoea hawana nafasi, lazima
muwe wabunifu nampitie upya zana mnazotumia kuhakiki ubora wa vyuo. Haiwezekani
kila siku tunasikia malalamiko kuhusu ubora wa wahitimu wakati TCU na NACTE
mpo” amesisitiza Prof. Ndalichako.
Waziri wa Elimu, Sayansi na
Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Prof.
James Mdoe wakisikiliza ufafanuzi kuhusu masuala mbalimbali ya elimu kutoka kwa mmoja wa washiriki wa maonesho ya
kumi na tatu ya Elimu ya Juu yanayofanyika jijini Dar es Salaam, ambapo washiriki
hao wametakiwa kujitadhimini kuhusu utoaji wao wa Elimu ya Juu
Kwa
upande wake Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo
Prof. James Mdoe amesema maonesho hayo ya Elimu ya Juu yatazisaidia
Taasisi mbalimbali za Elimu kujitathmini na kupata mrejesho kutoka kwa wadau namna wanavyotekeleza majukumu yao.
Maonesho
ya Taasisi za Ellimu ya Juu ambayo yatafanyika kwa siku nne yanalenga kutoa
elimu kwa umma kuhusu fursa zinazopatikana kwenye Taasisi za Elimu ya Juu,
kutoa nafasi kwa wananchi wanaotarajia kujiunga na Elimu ili elimu ya
kujiridhisha na programu za masomo na huduma zinazotolewa.
Waziri wa Elimu, Sayansi na
Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo
Prof. James Mdoe akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa Tume ya
Vyuo Vikuu ambao ni waandaaji wa maonesho ya kumi na tatu ya Elimu ya Juu
yanayofanyika jijini Dar es Salaam.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
Zingatia: Mwanachama wa blogu hii tu ndiye anayeweza kuchapisha maoni.