Naibu Katibu Mkuu Dk. Ave Maria
Semakafu amewataka Maafisa Elimu na Wathibiti ubora kuhakikisha wanafanya
ufuatiliaji na kutoa taarifa kwenye Mamlaka zinazohusika ili changamoto hizo
ziweze kupatiwa ufumbuzi.
Dk. Semakafu ametoa kauli hiyo
leo Wilaya Magu mkoani Mwanza wakati akishiriki zoezi la ufuatiliaji wa miradi
inayofadhiliwa na washirika wa Maendeleo kuhusu ufundishaji na ujifunzaji
AJESR.
Naibu Katibu Mkuu Dk. Ave Maria Semkafu akizungumza na timu ya
ufuatiliaji wa Maendeleo ya ujifunzaji na ufundishaji shuleni (Hawapo
Pichani), Wilayani Magu, mkoani Mwanza.
Dk. Semakafu amesema suala la ufuatiliaji
kwa viongozi waliopewa Mamlaka ni la lazima kwani itasaidia zaidi kubaini
changamoto lakini pia ni sehemu ya uwajibikaji katika kutimiza malengo ya
Taifa.
“Viongozi ni lazima
tuwajibike katika kushughulikia masuala ya wananchi na siyo kusubiri kiongozi
wa juu aje atoe maelekezo ndiyo tuanze kukimbizana, mfano wewe mthibiti ubora
wa shule, au Afisa Elimu unakagua shule zako? unatatua changamoto au unasubiri
mpaka Mkurugenzi wa Halmashauri atoe maelekezo?” Alisisitiza Dk. Semakafu.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa
Halmashauri ya Wilaya ya Magu Lutengano Mwalwiba ameahidi kuendelea kufanyia kazi
changamoto mbalimbali zilizopo katika Halmashauri hiyo ili Taifa liweze kusonga
mbele.
Baadhi ya wajumbe wa timu ya ufuatiliaji wa miradi
inayotekelezwa na washirika wa Maendeleo wakipokea taarifa kutoka kwa
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Magu Lutengano Mwalwiba, Mkoani Mwanza.
Amesema hakuna jambo ambalo
litaweza kuwa mbadala wa Elimu, Elimu ni kila kitu sasa ikivurugwa Elimu Taifa
haliwezi kusonga mbele.
“Tukiwa na misingi mizuri ya
Elimu lazima Taifa tutafanikiwa, changamoto zipo na ndiyo maana viongozi tupo
kama changamoto zisingekuwepo basi hata viongozi tusingekuwepo,” alisisitiza
Mkurugenzi huyo.
Naibu Katibu Mkuu Dk. Semakafu akipokelewa katika Kituo Cha
Ufundi Ihushi kilichopo Wilayani Magu, mkoani Mwanza
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
Zingatia: Mwanachama wa blogu hii tu ndiye anayeweza kuchapisha maoni.