Waziri
wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof.
Joyce Ndalichako amekiagiza Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere
kuhakikisha kinaandaa wanafunzi mahiri na wenye ujuzi utakaowawezesha kuchangia
katika uchumi wa Taifa.
Ndalichako
ametoa agizo hilo wakati wa uzinduzi wa hosteli ya wanafunzi, uliofanyika katika
Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Kigamboni jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia
Profesa Joyce Ndalichako akizungumza na watendaji pamoja na wanafunzi wa Chuo
cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (hawapo pichani) wakati wa kuzindua hosteli ya wanafunzi yenye uwezo wa kuchukua
wanafunzi 720 kwa mara moja.
Amesema kwa kufanya hivyo mtakuwa mnatekeleza
Dira ya Elimu ambayo inataka Taifa kuwa na Mtanzania aliyeelimika na mwenye
maarifa, stadi, umahiri, uwezo na mitazamo chanya ili kuweza kuchangia katika
maendeleo ya Taifa.
Waziri Ndalichako ameupongeza uongozi wa chuo
hicho kwa kuingiza masomo ya uongozi, maadili na uzalendo katika mitaala ya
ngazi zote za kitaaluma kwa kuwa ni muhimu katika kuwajengea vijana uzalendo,
moyo wa kujituma na kulipenda Taifa.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia
Profesa Joyce Ndalichako akizindua hosteli katika Chuo cha Kumbukumbu ya
Mwalimu Nyerere na kuwataka wanafunzi wa Chuo hicho kutunza miundombinu hiyo ili
iweze kuwasaidia wanafunzi wengine watakaojiunga na Chuo hicho.
Kwa
upande wake Mkuu wa Chuo Profesa Shadrack Mwakalila amesema hosteli hiyo ni ya
ghorofa 5 na ina uwezo kuchukua wanafunzi 720 kwa mara moja hivyo kupunguza
tatizo la malazi ya wanafunzi katika chuo hicho.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia
Profesa Joyce Ndalichako akikagua baadhi ya miundombinu katika hosteli mpya
aliyoizindua katika Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
Zingatia: Mwanachama wa blogu hii tu ndiye anayeweza kuchapisha maoni.