Waziri
wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof Joyce Ndalichako amewataka walimu wa shule
za Sekondari kuwahamisha na kuwasaidia wanafunzi kuandaa bunifu zao ili waweze kushiriki katika maonesho mbalimbali ya sayansi, teknolojia na ubunifu
yanayofanyika nchini.
Akizungumza
katika sherehe za utoaji wa zawadi kwa washindi wabunifu walioshiriki katika Monesho
ya nane ya taasisi ya Wanasayansi Chipukizi (YST) Jijini Dar es Salaam Waziri
Ndalichako amesema ushiriki wa wanafunzi katika maonesho hayo utawasaidia kuinua vipaji vyao na kupenda masomo ya
sayansi.
Waziri
wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akikabidhi zawadi kwa
washindi wa maonesho ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu kutoka Shule ya
Sekondari Msalato. Waziri Ndalichako amewahimiza wanafunzi nchini kushiriki katika
maonesho mbalimbali ya namna hiyo ili kukuza vipaji vyao.
Ndalichako
amesema anatambua kuwa maonesho hayo yamesaidia mamia ya wanafunzi wa shule za
sekondari nchini kuonyesha bunifu zao ambazo zimewawezesha kuendelea kutafuta maarifa ya kisayansi yatakayosaidia nchi kufikia uchumi wa viwanda.
Waziri Ndalichako amesema Wizara yake kupitia
Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia COSTECH) itaendelea kushirikiana na taasisi
hiyo kuangalia namna bora ya kuinua vipaji na kuboresha tatifi zinazofanywa na
wanafunzi.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof.
Joyce Ndalichako akimpongeza mmoja wa washindi wa kwanza wa bunifu
zilizoonyesho katika maonesho ya Sayansi , Teknolojia na Ubunifu kutoka Shule
ya Sekondari Msalato.
Katika kipindi cha miaka 7 iliyopita, Taasisi
hiyo imeweesha zaidi wanafunzi elfu tano (5,000) kushiriki katika maonesho ya
Sayansi, Teknolojia na Ubunifu pamoja na kutoa mafunzo kwa walimu zaidi ya 1000
wa shule za sekondari ya namna ya kusaidia na kuboresha tafiti zinazofanywa na
wanafunzi.
Waziri
wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akishangilia na
kufurahia pamoja na wanafunzi walioshinda zawadi mbalimbali katika maonesho ya
Sayansi, Teknolojia na Ubunifu yaliyoshirikisha shule mbalimbali nchini.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
Zingatia: Mwanachama wa blogu hii tu ndiye anayeweza kuchapisha maoni.