Waziri
wa Elimu, Sayamsi na Teknolojia Prof.
Joyce Ndalichako amewataka walimu wa shule ya sekondari Manga Delta iliyoko
wilayani Kibiti mkoani Pwani kuhakikisha wanawasaidia wanafunzi kimasomo ili taaluma
katika shule hiyo iweze kupanda.
Waziri
Ndalichako ametoa agiza hilo katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja
vya Shule hiyo ambapo amesema hajaridhishwa na mwenendo wa taaluma katika shule
hiyo.
Amesema
pamoja na serikali kuwekeza fedha nyingi katika kuboresha miundombinu ya shule
hiyo bado imekuwa ikishuka kitaaluma mwaka hadi mwaka.
Waziri wa Elimu, Sayansi na
Teknolojia Prof. Joyce Ndalich ako akizungumza na wanafunzi, walimu na wazaza
wa shule ya Sekondari Manga Delta iliyoko wilayani Kibiti mkoani Pwani. Waziri
Ndalichako amewataka walimu wa shule hiyo kuhakikisha wanawasaidia wanafunzi kimasomo
ili taaluma katika shule hiyo iweze kupanda.
“Serikali imeshatoa zaidi ya shilingi milioni
256 kwa ajili ya ukarabati na ujenzi wa miundombinu ya vyumba vya madarasa na
bweni juhudi hizi ziende sambamba na ufundishaji ili taaluma ipande” Alisisitiza Ndalichako
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce
Ndalichako akikabidhi ufunguo wa pikipiki kwa mmoja wa Waratibu Elimu Kata
ambapo amekabidhi Pikipiki kumi na sita katika mkutano wa hadhara uliofanyika
wilayani Kibiti Mkoani Pani. Waziri Ndalichako amewataka Waratibu Elimu Kata
hao kutumia Pikipiki hizo katika shughuli zitakazosaidia kuboresha Elimu.
Aliongeza
kuwa Serikali ya Awamu ya Tano kila mwezi imekuwa ikitoa kiasi cha silingi
bilioni 20. 8 kugharamia Elimu bila malipo pamoja na kutoa shilingi laki mbili
na nusu za posho ya madaraka kwa Wakuu wa Shule na Waratibu Elimu Kata hivyo
amewataka kuwajibika ili kupandisha taaluma ya shule hiyo.
Waziri
wa Elimu amehitimisha ziara yake ya siku mbili ya kikazi wilayani Kibiti mkoni
Pwani kwa kukabidhi gari ya Idara ya Udhibiti Ubora kwa Mkurugenzi Mtendaji wa
Wilaya hiyo pamoja na pikipiki kumi na sita kwa Waratibu Elimu Kata.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce
Ndalichako akifungua gari kabla ya kumkabidhi Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya
Kibiti Alvera Ndabagoye kwa ajili ya Idara ya Udhibiti Ubora ya wilaya hiyo. Waziri
Ndalichako amewataka Wadhibiti ubora nchini kufanya kazi zao kwa weledi
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
Zingatia: Mwanachama wa blogu hii tu ndiye anayeweza kuchapisha maoni.