Waziri
wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako ameliagiza Baraza la
Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) kuendelea kufungia vyuo vinavyotoa mafunzo kwa ubabaishaji ili kulinda ubora wa Elimu na Ujuzi kwa
wanafunzi.
Waziri
Ndalichako ameyasema hayo Jijini Dar es salaam wakati akizindua Baraza la
Uongozi la Taifa la Elimu ya Ufundi ambapo amewataka NACTE kufungia hata
vyuo vya serikali kama itabainika kutoa
mafunzo yasiyo na ubora.
Waziri wa Elimu, Sayansi na
Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akimkabidhi Mwenyekiti mpya wa Baraza la Baraza
la Uongozi la Taifa la Elimu ya Ufundi Prof. John Kondoro Sheria na Kanuni za
Baraza hilo wakati wa uzindzi uliofanyika jijini Dar es Salaam
“Hatutaki
kuwa na utitiri wa vyuo vingi ni bora kuwa na vichache lakini vitoe wahitimu
wenye ujuzi na maarifa ambao wanaweza kuwa na mchango katika Taifa letu.”
Amesisitiza Waziri Nalichako.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dk. Leornald Akwilapo akizungumza na wananchi wa mtaa wa Majimatitu B Kata ya Kilungule mkutano huo ulifanyika katika viwanja vya shule mpya inayojengwa kwa ajili ya kupunguza mlundikano wa wanafunzi wa shule ya msingi Majimatitu A
Pia Waziri
Ndalichako amekagua Maendeleo ya ujenzi wa shule mpya ya Msingi inayojengwa Majimatitu
Wilayani Temeke yenye lengo la kupunguza mlundikano wa wanafunzi katika
shule ya Msingi Majimatitu A yenye wanafunzi zaidi ya 7000.
Waziri wa Elimu, Sayansi na
Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akikagua madaftari ya wanafunzi wa Darasa la
pili katika shule ya Msingi ya Majimatitu A. Waziri Ndalichako alifika shuleni
hapo kujionea mrundikano wa wanafunzi katika shule hiyo
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
Zingatia: Mwanachama wa blogu hii tu ndiye anayeweza kuchapisha maoni.