Waziri
wa Elimu, Sayansi na Teknolojia
Joyce Ndalichako amemuagiza
Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dk. Leonard Akwilapo kumsimamisha kazi Afisa
manunuzi Audifasy Myonga na watumishi
wengine wawil wa Chuo cha Ualimu Morogoro.
Waziri
Ndalichako ametoa maagizo hayo mkoani Morogoro baada ya kutembelea chuo Cha
Ualimu Morogoro na kukuta idadi kubwa ya
vifaa vya maabara visivyotumika huku muda wa matumizi ya vifaa hivyo ukikaribia kuisha muda wake wa matumizi.
Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia
Prof. Joyce Ndalichako akikagua baadhi ya vifaa vya maabara katika Chuo cha
Ualimu Morogoro kilichopo mkoani Morogoro ambapo amekuta vifaa na madawa ya
maabara ambayo yamehifadhiwa bila kutumika tangu mwaka 2016.
Ndalichako
amesema ununuzi wa vifaa hivyo unaonyesha kuwa na shaka kwani vifaa hivyo
vilinunuliwa kwa awamu mbili ndani ya mwezi mmoja huku gharama ya manunuzi
ikionyesha kupanda mara mbili hadi tatu kutoka gharama ya awali.
“Mkuu
wa Chuo ameeleza vizuri kabisa kuwa vifaa hivyo vilinunuliwa bila wao
kushirikishwa, sasa unajiuliza mnunuzi amewezeje kununua vifaa vya maabara bila
kuwashirikisha watumiaji,” alihoji Waziri Ndalichako .
Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia
Prof. Joyce Ndalichako akizungumza na watumishi wa Chuo cha Ualimu Morogoro
kilichopo mkoani Morogoro. Waziri pia alisikiliza changamoy=to walizonazo
watumishi hao.
Pia,
Waziri Ndalichako ametembelea shule ya
Sekondari ya Mzumbe kwa lengo la kukagua maendeleo ya ukarabati wa miundombinu
ya shule hiyo unaofanywa na wizara ambapo amewataka walimu na wanafunzi
kuhakikisha wanafanya vizuri katika masomo yao ili wafaulu kwa viwango vya juu.
Waziri
wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako na Naibu Katibu Mkuu Dk.
Avemaria Semakafu wakikagua baadhi ya miundombinu iliyokarabatiwa katika shule
ya Sekondari Mzumbe iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero mkoani
Morogoro.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
Zingatia: Mwanachama wa blogu hii tu ndiye anayeweza kuchapisha maoni.