Waziri
wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako ameitaka Bodi mpya ya
Huduma za Maktaba Tanzania kuhakikisha inaanzisha Maktaba za Wilaya ili
kuwawezesha watanzania wengi kunufaika na Elimu na Maarifa yatokanayo na
usomaji wa vitabu.
Waziri
Ndalichako ametoa agizo hilo Jijini Dar es Salaam wakati akizindua Bodi hiyo na
kusisitiza kuwa kuwepo kwa maktaba hizo kutaondoa changamoto ya wananchi
kutembea umbali mrefu kufuata maktaba za mikoa.
Waziri
wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akimkabidhi Mwenyekiti
wa Bodi ya Huduma za Maktaba Tanzania Prof. Rwekaza Mkandala Sheria za Bodi
hiyo.
“Wananchi wanapenda kusoma vitabu sasa natoa
rai kwenu Bodi mpya mshirikiane na Halmashauri za Wilaya, Miji na Manispaa
kuanzisha Maktaba katika Wilaya zote, sisi kama Serikali tutaendelea kutoa
ushirikiano kuhakikisha tunaimarisha utoaji wa huduma za maktaba nchini.”
Alisisitiza Ndalichako.
Waziri
wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akimkabidhi Mwenyekiti wa
Baraza laUsimamizi la Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW) Naomi Katunzi
Sheria za Bodi hiyo. Ameiagiza Baraza hilo kuweka vigezo vitakavyotumika kutoa
Elimu nje ya mfumo rasmi.
Katika
hatua nyingine Waziri Ndalichako ametemblea Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima na
kuzindua Baraza la Usimamizi la Taasisi hiyo ambapo amelitaka baraza hilo kuboresha vigezo vinavyotumika
kusajili vituo vinavyotoa Elimu ya sekondari nje ya mfumo rasmi pamoja na
kusimamia ubora wa elimu inayotolewa.
Waziri
wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akiongea na Watumishi wa
Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (Hawapo Pichani) wakati wa uzinduzi wa Baraza
la Taasisi hiyo uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
Zingatia: Mwanachama wa blogu hii tu ndiye anayeweza kuchapisha maoni.