JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA
YA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA
Anuani ya simu “ELIMU”
Simu: 026
296 35 33
Baruapepe:info@moe.go.tz
|
|
Chuo cha Masomo
ya Biashara na Sheria,
Chuo Kikuu cha
Dodoma (UDOM), Jengo Na. 10,
S. L. P. 10,
40479 DODOMA.
|
TAARIFA
KWA UMMA
KUFANYA
MALIPO KUPITIA MFUMO MPYA WA SERIKALI WA GePG
Wizara ya Elimu, Sayansi na
Teknolojia inapenda kuutaarifu Umma ya kwamba kuanzia tarehe 01 Novemba 2018,
itahamia rasmi katika mfumo wa kukusanya mapato ya Serikali kwa njia ya kieletroniki
ujulikanao kama ‘Government e-Payment Gateway’ (GePG) kwa matakwa ya Sheria ya
Fedha za Umma, Sura 348.
Wizara, itaanza kutumia
mfumo huu kwenye makusanyo yake yote ya mapato kwa Vyuo vya Ualimu vya Serikali,
Vyuo vya Maendeleo ya Wananchi na Kanda za Uthibiti Ubora wa Shule.
Hivyo mteja atapaswa kufika au kuwasiliana na kituo husika anachotaka kufanya
malipo ili kupata namba ya utambulisho wa malipo husika (Payment Control Number) kabla ya kufanya malipo.
Wizara kwa kushirikiana na
Wataalamu wa mfumo kutoka Wizara ya Fedha na Mipango itahakikisha mfumo huu
unafanya kazi bila kuathiri utoaji wa huduma. Aidha, Wizara ya Elimu, Sayansi
na Teknolojia inaungana na Wizara na Taasisi nyingine za Serikali zinazotumia
mfumo huo kwa mafanikio. Baadhi ya Wizara na Taasisi hizo ni Polisi, Brella,
Wizara ya Ardhi, Nyumba na Makazi, TRA, Bodi ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu
Tanzania (NBAA) pamoja na Mamlaka ya Maji.
Namna ya kulipa kwa kutumia
mfumo wa kieletroniki (Government e-Payment Gateway);
1. Malipo
yanaweza kufanywa kwa njia ya kibenki kwa kufuata hatua zifuatazo;
a)
Unapopata kumbukumbu ya malipo (Control
Number);
b)
Tembelea Tawi lolote la Benki ya CRDB, NMB na
NBC;
c)
Baada ya kuwasili kwenye benki, mpe mtoa
huduma wa dirishani namba kumbukumbu ili kukamilisha mchakato wa malipo yako.
2. Malipo
yanaweza pia kufanywa kwa njia ya mtandao wa simu za mikononi (M-pesa, Tigo
Pesa na Airtel Money) kwa kufuata hatua zifuatazo;
a)
Kupitia simu yako, piga *150*00#, au *150*01#
au *150*60#;
(Kupata M- pesa, Tigo Pesa na Airtel Money);
b)
Chagua ‘Lipia malipo (Pay-Bills)’;
c)
Chagua ‘Malipo ya Serikali’;
d)
Chagua ‘Ingiza namba ya malipo’ na uingize
namba ya kumbukumbu ya malipo (Control Number);
e)
Weka kiasi cha fedha unachotaka kulipa;
f)
Thibitisha muamala wako kwa kuingiza neno au
namba yako ya siri; na
g)
Hifadhi ujumbe wa simu uliopokea kama
ushahidi wa malipo endapo utahitajika kuonyesha kwa kituo husika.
Imetolewa na;
Dkt.
Leonard D. Akwilapo
KATIBU MKUU
WIZARA YA ELIMU,
SAYANSI NA TEKNOLOJIA