Serikali imekipongeza Chuo
Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST) kwa kusimamia kwa ufanisi
ukarabati wa Chuo cha Ualimu Tandala kilichopo Wilaya ya Makete Mkoani Njombe.
Kauli hiyo ya Serikali
imetolewa na Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha wakati
akikagua ukarabati wa miundombinu ya Chuoni hapo mradi ambao unafadhiliwa na
Wizara hiyo.
“Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya wamekuwa
wakifanya kazi nzuri za kuridhisha katika miradi yao yote waliokabidhiwa na
Wizara na hivi ndivyo inavyotakiwa, Serikali inapotoa fedha kwa ajili ya kurejesha
hadhi ya miundombinu ya shule, vyuo na miundombinu mingine zilenge kukamilisha
kazi hizo na sio kutanguliza maslahi binafsi na kuingiza Serikali kwenye
hasara,” alisema Naibu Waziri Ole Nasha
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na
Teknolojia William Ole Nasha akiangalia katika picha muonekano wa zamani kabla
ya ukarabati na baada ya ukarabati wa miundombinu ya Chuo cha Ualimu Tandala
kilichopo Wilaya ya Makete Mkoani Njombe wakati alipotembelea Chuoni hapo
kukagua ukarabati uliofanyika.
Naibu Waziri huyo amezitaka
Taasisi nyingine za Serikali kuwa waadilifu katika matumizi ya fedha pindi
Serikali inapotoa fedha kwa ajili ya kuboresha miundombinu ili malengo
yaliyokusudiwa yaweze kutimia huku akiwataka wanafunzi wa chuo hicho kusoma kwa
bidii na kufaulu kwa kiwango cha juu.
Kiongozi huyo ameeleza kuwa Serikali
ilisitisha kutoa ajira kwa wingi kwa lengo la kupitia mifumo ya ajira upya
kwani iliyokuwepo ilizalisha wafanyakazi hewa na wenye vyeti feki hivyo ilikuwa
ni lazima kufanya hivyo ili kuiepusha Serikali kuingia kwenye hasara.
Naibu
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha akikagua miundombinu
ya Chuo cha Ualimu Tandala kilichopo Wilaya ya Makete Mkoani Njombe baada ya ukarabati.
Nae Mkuu wa Chuo cha Ualimu
Tandala Philip Khamisi alisema mpaka sasa Chuo hicho kina wanachuo 225 huku
wakitegemea kupokea wanachuo 342 ambapo itafanya idadi ya kufika 567.
Wizara ilitoa zaidi ya
shilingi bilioni moja kwa ajili ya kukarabati miundombinu ya Chuo cha Tandala ambacho
miundombinu yake ilikuwa imechakaa.
Muonekano
wa sasa wa mabweni ya wavulana katika Chuo cha ualimu Tandala kilichopo
wilayani Makete mkoani Njombe.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
Zingatia: Mwanachama wa blogu hii tu ndiye anayeweza kuchapisha maoni.