Naibu waziri wa Elimu, Sayansi
na Teknolojia William Ole Nasha ametoa wiki moja kwa mtaalamu Elekezi wa Kampuni
ya Archquants Service Limited kuhakikisha inawasilisha michoro ya kazi za nje
ya Chuo cha ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi Namtumbo kilichopo Mkoani Ruvuma
ili ujenzi wa chuo hicho uweze kukamilika.
Mheshimiwa Ole Nasha ametoa
agizo hilo wakati wa kukagua maendeleo ya ujenzi wa chuo hicho ambapo amesema
ucheleweshwaji wa michoro hiyo unapelekea kuchelewesha ukamilishaji wa mradi
huo.
Naibu
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha akipokea taarifa ya
Elimu ya Mkoa wa Ruvuma kutoka kwa Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Pololet Mgema
wakati wa ziara ya kukagua miradi ya Elimu Mkoni huko.
Katika hatua nyingine Naibu
Waziri Ole Nasha ameitaka Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi VETA
kuhakikisha wanaanzisha kozi ya ufundi
wa zana za kilimo (Agro mechanics) katika Chuo cha Ufundi na Mafunzo ya Ufundi
Stadi kilichopo Songea ili kupata vijana wengi watakaosomea fani hiyo.
Naibu Waziri amesema ukanda
wa Nyanda za Juu Kusini unategemea sana kilimo, hivyo kuanzishwa kwa kozi hiyo kutasaidia
wananchi wengi kupata uelewa wa kina kile wanachokisoma na baadae kutekeleza
kwa vitendo.
“Serikali inatilia mkazo Elimu ya ufundi na
imejielekeza katika kuhakikisha inapanua fursa ya vijana wengi kupata Elimu ya
ufundi na ndio maana Serikali ya awamu
ya Tano imeamua kuweka Vyuo vya VETA katika kila Wilaya na Mkoa,” alisisitiza
Naibu Waziri Ole Nasha
Naibu
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha akipata maelezo kutoka
kwa mwalimu wa somo la uchomeleaji (welding) Onesmo Pela katika Chuo cha Ufundi
Veta Songea namna anavyotekeleza majukumu yake.
Naibu Waziri Ole Nasha yuko
mkoani Ruvuma kwa ziara ya kikazi ya siku mbili kwa ajili ya kukagua miradi ya
Elimu inayotekelezwa na Wizara ya Elimu, Sayasni na Teknolojia.
Naibu
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha akikagua maendeleo ya
ujenzi wa Chuo cha Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi cha Namtumbo kilichopo
katika Wilaya ya Namtumbo Wilayani Ruvuma
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
Zingatia: Mwanachama wa blogu hii tu ndiye anayeweza kuchapisha maoni.