Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu,
Sayansi na Teknolojia Dkt. Leonard Akwilapo amewataka washiriki wa mafunzo ya
Force Akaunti kuhakikisha wanazingatia Kanuni, taratibu na Sheria wakati wa
usimamiaji wa ujenzi na ukarabati wa miradi ya serikali.
Dkt. Akwilapo ametoa kauli hiyo
wakati akifunga mafunzo ya siku mbili ya matumizi ya Force Akaunti
yanayofanyika mkoani Morogoro ambayo yameshirikisha watumishi wa Serikali
wakiwemo Wakurugenzi wa Halmashauri, Wakurugenzi wa kanda VETA, Maafisa
Kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na Maafisa kutoka VETA.
Katibu Mkuu wa Wizara
ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Leonard Akwilapo amefunga mafunzo ya Force
Akaunti ambapo pia amewataka watendaji kuzingatia taratibu,kanuni na sheria za
Fedha.
Katibu Mkuu huyo amewaeleza
washiriki hao kuwa utaratibu wa Force Akaunti upo kisheria, hivyo amewasisitiza
washiriki kuhakikisha wanakuwa na utunzaji wa kumbukumbu ikiwa ni pamoja na
kuwepo kwa risiti za kielektroniki (EFD).
Dkt. Akwilapo amesema kuwa
Force Akaunti ikisimamiwa vizuri inaonyesha thamani ya Fedha, mradi unakamilika
na kuwa yote hayo yanawezekana enadapo ushirikiahwaji na uwazi miongoni
mwa Jamii utakuwepo katika eneo ambalo mradi unatekelezwa.
Washiriki wakifuatilia mafunzo ya
Force Akaunti yenye lengo la kuwajengea uwezo washiriki namna bora ya kusimamia
miradi ya ujenzi na ukarabati yanayofanyika Mkoani Morogoro.
Mafunzo hayo ya siku mbili
yanaratibiwa na mradi wa kukuza Maarifa, Stadi na ujuzi (ESPJ) yamehusisha
Wakurugenzi wa halmashauri za Kasulu,Ngorongoro,Kongwa,Nyasa, Wakurugenzi
wa Kanda VETA, Wakurugenzi wasaidizi kutoka Makao Makuu VETA na Maafisa
kutoka VETA.
Katibu Mkuu wa
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Leonard Akwilapo
akisindikizwa na Mkurugenzi wa Elimu ya Ufundi Dkt. Noel Mbonde pamoja na
mratibu wa mafunzo ya kukuza maarifa, stadi na Ujuzi (ESPJ), Dkt. Keneth Hosea
baada ya kufunga mafunzo ya Force Akaunti yaliyofanyika mkoani Morogoro.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
Zingatia: Mwanachama wa blogu hii tu ndiye anayeweza kuchapisha maoni.