Katibu Mkuu Wizara y Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Leonard Akwilapo akimkabidhi cheti mmoja wa wahitimu wakati wa Mahafali ya 26 yaliyofanyika katika Chuo Cha ADEM, Bagamoyo mkoani Pwani
Amewataka wahitimu hao kuhakikisha kuwa wanaenda kufundisha pamoja na
kuhakikisha wanawalinda na kusimamia haki za watoto kwa mujibu wa Sheria.
“Mategemeo ni kuongezeka kwa utendaji kazi, ikiwa ni pamoja na wanafunzi
kuhudhuria shule, kiwango cha ufaulu kuongezeka pamoja na kubaini
changamoto zinazowakabili wanafunzi na kuzipatia ufumbuzi kwa utaratibu
unaofaa,”alisema Dkt. Akwilapo.
Katibu Mkuu akizungumza na wahitimu hawapo pichani wakati wa mahafali ya
26 katika Chuo cha ADEM, Wilayani Bagamoyo Mkoani Pwani.
Dkt. Akwilapo amewataka wahitimu hao kujenga mahusiano na mazingira mazuri kati ya shule na Jamii, kuhakikisha umoja unakuwepo kati ya pande zote tatu kwa maana ya walimu, wanafunzi na wazazi na eneo hilo likifanikiwa basi Elimu yetu itakuwa imefanikiwa.
Akizungumza katika mahafali hayo Mtendaji Mkuu wa ADEM Dkt. Siston
Masanja amesema Chuo hicho kinawajibu wa kutoa mafunzo na
ushauri wenye lengo ka kuboresha Elimu nchini, huku akiendelee kuiomba Wizara
kutenga fedha kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya Chuo hicho.
Wahitimu wa mafunzo katika Chuo cha ADEM wakati wa mahafali ya 26 yaliyofanyika chuoni Bagamoyo Mkoani Pwani
Dkt. Masanja pia amewataka wahitimu kuacha kubweteka kwa Elimu waliyoipata ADEM, na badala yake waende wakajiendeleze zaidi kama vitabu vya dini vinavyoelekeza.