Serikali
inajenga Shule ya Sekondari Maalum ya
mfano kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu katika Chuo cha Ualimu Patandi kilichopo
mkoani Arusha yenye uwezo wa kudahili wanafunzi 600 kwa mara moja ikiwa ni
mkakati wake wa kuongeza fursa za udahili kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum.
Kauli
hiyo ya Serikali imetolewa na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof.
Joyce Ndalichako katika ufunguzi wa Bonanza la Kilimanjaro Committee for Sports
iliyofanyika katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi mkoani
Kilimanjaro ambapo amesema kwa Mkoa wa Kilimanjaro, ambapo amesema Serikali
imekarabati miundombinu kwenye shule kongwe ya Moshi Ufundi inayopokea wanafunzi
wenye mahitaji maalum.
Waziri wa Elimu, Sayansi na
Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akimpongeza mwanafunzi mwenye mahitaji maalum
baada ya kufanya vizuri katika maonyesho ya mavazi katika ufunguzi wa Bonanza
la Kilimanjaro Committee for Sports iliyofanyika katika viwanja vya Chuo Kikuu
cha Ushirika Moshi mkoani Kilimanjaro ambapo amesema kwa Mkoa wa Kilimanjaro
“Serikali inaendelea kutekeleza mipango
mbalimbali inayolenga kuongeza upatikanaji wa fursa na kuimarisha ubora wa
elimu inayotolewa katika ngazi zote kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu ambapo
tayari serikali imekarabati miundombinu ya shule kongwe ya Moshi Ufundi ambayo
inapokea wanafunzi wenye mahitaji maalumu”. Alisisitiza Prof. Ndalichako.
Waziri
Ndalichako amesema watu wenye mahitaji maalum wana fursa sawa ya kushiriki
katika michezo na kufanya hivyo kunasaidia kuondoa kasoro za kimwili na kiakili
na baadhi ya ulemavu unaweza kurekebishwa kwa kushiriki katika michezo na
burudani.
Prof
Ndalichako amesisitiza kuwa ushiriki katika michezo, hususan kwa watoto wenye
mahitaji maalum ni muhimu sana kama ilivyowekwa bayana katika kifungu cha 52
cha Sheria ya Watu wenye Ulemavu Namba 9 ya mwaka 2010 kinachosisitiza umuhimu
wa Watu wenye ulemavu kushiriki katika michezo, starehe na burudani.
Akizungumza
katika Bonanza hilo Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Walemavu) Stella Ikupa
amewataka wanafunzi wenye mahitaji maalum kuunga mkono juhudi za serikali ya
Awamu ya Tano kwa kuendelea kujitambua, kujikubali na kujituma ili kujikwamua
katika changamoto wanazokutana nazo katika masomo yao.
Waziri
Ikupa amewataka wanafunzi hao pia kujiunga na vyuo vya ufundi ambavyo
vitawawezesha kupata satadi ambazo watazitumia kwa ajili ya kujiari wenyewe badala ya kuwa tegemezi.
Waziri wa Elimu, Sayansi na
Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akibadilishana mawazo na Naibu Waziri, Ofisi
ya Waziri Mkuu (Walemavu) katika ufunguzi wa Bonanza la Kilimanjaro Committee
for Sports iliyofanyika katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi mkoani
Kilimanjaro ambapo amesema kwa Mkoa wa Kilimanjaro
Naye
Mratibu wa Bonaza hilo ambaye ni Mbunge wa Viti Maalum (Vyuo Vikuu) Esther
Mmasi amesema wakati wa maandalizi ya
Bonanza hilo amebaini kuwepo kwa uhaba wa viwanja vya michezo katika shule
zenye wanafunzi wenye mahitaji maalumu ambapo ameiomba serikali kuhakikisha
inaboresha miundominu ili kuwajengea uwezo wanafunzi hao.
Waziri wa Elimu, Sayansi na
Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akizungumza na wadau wa Elimu pamoja na
wanafunzi wenye mahitaji maalum ( Hawapo Pichani) katika ufunguzi wa Bonanza la
Kilimanjaro Committee for Sports iliyofanyika katika viwanja vya Chuo Kikuu cha
Ushirika Moshi mkoani Kilimanjaro.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
Zingatia: Mwanachama wa blogu hii tu ndiye anayeweza kuchapisha maoni.