Waziri
wa Elimu, Sayansi na Teknolojia ambaye pia ndiye Rais wa Skauti Profesa Joyce Ndalichako
amewaahidi ushirikiano Viongozi wa Chama cha Skauti Tanzania katika kufanya maandalizi
ya sherehe za Zanzibar Jambo Ree inayotarajiwa kufanyika mwezi wa sita mwaka huu Visiwani
Zanzibar..
Waziri
Ndalichako amesema hayo wakati alipokutana na kuzungumza na Viongozi wa Juu wa Skauti Tanzania kwa lengo la kumuelezea
Waziri hatua iliyofikiwa katika
maandalizi ya sherehe hizo.
Waziri
Ndalichako amewaambia viongozi hao wa skauti kuwa ni vyema wakaliangalia kwa
makini pendekezo lao la kutaka kupeleka washiriki 24 Visiwani Zanzibar kutoka
kila mkoa wa Tanzania bara kwani namba hiyo itakuwa ni kubwa, na kuzifanya
sherehe hizo kuonekana ni za Bara badala ya Zanzibar.
“Ninawashauri kuangalia kwa undani na makini
suala la idadi ya washiriki kutoka Bara kwa kila mkoa washiriki 24, idadi hii
ni kubwa na tutawazidi kwa kuwa Zanzibar ina mikoa michache kuliko sisi na sherehe hizi
zitaonekana kuwa ni za Bara na si Zanzibar,” alisema Waziri.
Skauti
Mkuu Mwantumu Mahiza alimwelezea Waziri kuwa Chama cha Skauti Tanzania
kinatekeleza agizo la Makamu wa Rais alilolitoa wakati wa maadhimisho ya Siku
ya Skauti Dunia na Maadhimisho ya miaka mia moja ya Skauti hapa nchini ya
kukitaka chama hicho kufanya sherehe hizo
Visiwani Zanzibar.
Mahiza
pia alimtambulisha Kamishna Mkuu mpya Grace Joseph Kado aliyeteuliwa hivi
karibuni na kueleza kuwa sasa safu ya uongozi kwa sasa imekamilika.
Skauti Mkuu Mwantumu Mahizi akisisitiza jambo kwa Rais wa Skauti
Tanzania ambaye pia ni Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce
Ndalichako wakati wa kujadiliana kuhusu maandalizi ya sherehe za Jambo Ree
zinazotarajiwa kufanyika visiwani Zanzibar.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
Zingatia: Mwanachama wa blogu hii tu ndiye anayeweza kuchapisha maoni.