Kamati ya
Bunge ya Kudumu ya Huduma na Maendeleo ya Jamii imekamilisha ziara ya kukagua
utekelezaji wa Miradi mitatu mikubwa inayogharimiwa na Serikali kupitia bajeti
ya Mwaka 2018/19 katika baadhi ya Vyuo vilivyo chini ya Wizara ya Elimu ,
Sayansi na Teknolojia na kuridhishwa na utekelezaji wa Miradi hiyo.
Kamati hiyo
imetembelea Chuo Kikuu kishiriki cha Elimu (DUCE) katika mradi wa upanuzi na
ukarabati wa jengo la Utawala ambalo linagharimu shilingi Bilioni 3.2 ambapo kazi hiyo inaendelea na
litakapo kamilika litaongeza nafasi kwa ajili ya ofisi za watumishi na vyumba
vya mikutano.
Aidha kamati
imetembelea mradi wa upanuzi wa vyumba vya mihadhara
katika Chuo
Kikuu Ardhi kazi ambayo imekamilika kwa hatua ya kwanza na
itagharimu
shilingi Bilioni 2.5 hadi kukamilika
kwake.
Kamati imekamilisha
ziara yake katika Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, ambapo Wajumbe
watembelea Jengo la jipya la Mihadhara linalojengwa kwa mapato ya ndani ya Chuo
hicho, ambalo linauwezo wa kuchukua wanafunzi zaidi ya 300 kwa wakati
mmoja. Aidha kamati imepongeza wizara na
uongozi wa Chuo kwa kazi nzuri na kubwa iliyofanyika katika kusimamia ujenzi huo.
Jengo hilo limekamilika kwa asilimia 95.
Waziri wa Elimu, Sayansi na
Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako na Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia
Wiliam Ole Nasha akijadiliana jambo katika kikao na wajumbe wa Kamati ya Kudumu
ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii (Hawapo Pichani) walipofanya ziara
katika Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere kukagua mradi wa upanuzi na
ukarabati wa Chuo hicho.
Aidha
Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Mh. Prof. Joyce Ndalichako
amepongeza uongozi wa Chuo kwa kusimamia vema matumizi ya fedha za zinazotokana
na Mapato ya ndani na kutumika kwa kutekeleza miradi yenye tija kwa Chuo. Ametumia nafasi hiyo kumpongeza
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh Dkt. John Pombe Magufuli kwa kusimamia
suala la kubana matumizi na kuelekeza fedha katika kazi zenye faida kwa jamii
kama ilivyo kwa Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere.
Katika
majumuisho ya ziara hiyo, Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumuya Bunge ya
Huduma na Maendeleo ya Jamii Mh. Oscar
Mukasa(Mb) ameipongeza wizara na taasisi zilizotembelewa kwa kusimamia
utekelezaji wa miradi na kushauri taasisi hizo kujikita katika kusimamia Dira
na dhima za uanzishwaji wake. Kamati pia imeshauri Serikali kupitia Wizara
kuhahakisha inatoa fedha za miradi kwa wakati kulingana na bajeti.
Naibu Waziri wa Elimu,
Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha akiongoza wajumbe wa Kamati ya Kudumu
ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii wakati wa kukagua maendeleo ya ujenzi
wa ukumbi wa kisasa wa Mihadhara unaojengwa kwa mapato ya ndani ya Chuo cha
Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere.
Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu
Nyerere Prof. Shadrack Mwakalila (Mwenye Tai Nyekundu) akitoa maelezo kuhusu
mradi wa ujenzi wa ukumbi mpya wa mihadhara wa Chuo chicho uliyojengwa kwa
fedha zinazotokana na mapato ya ndani kwa Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge
ya Huduma na Maendeleo ya Jami.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
Zingatia: Mwanachama wa blogu hii tu ndiye anayeweza kuchapisha maoni.