Serikali imesema imetenga
kiasi cha shilingi bilioni 18 kwa ajili ya kujenga Chuo cha Ufundi kipya katika
makao makuu ya nchini, jijini Dodoma.
Kauli hiyo ya Serikali
imetolewa na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako
wakati wa maonesho ya kwanza ya Elimu ya Ufundi na Mafunzo, mjini Dodoma.
Waziri Ndalichako amesema
Serikali itaendelea kuimarisha vyuo vya kati, kuhuisha mitaala ili kuendana na
Teknolojia, ambapo tayari serikali imetenga kiasi cha shilingi Bilioni 40 kwa
ajili ya ujenzi wa vyuo vya ufundi Stadi nchini.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce
Ndalichako akihutumia washiriki wa maonesho ya kwanza ya Elimu ya Ufundi na
Mafunzo pamoja na wananchi wa jiji la Dodoma (Hawapo pichani) wakati wa
uzinduzi wa Maonesho hayo.
Waziri amevitaka vyuo vyote
vya ufundi nchini kuzingatia taratibu, kanuni na sheria katika kuendesha vyuo
hivyo na yeyeote ambaye hatakidhi vigezo basi chuo hicho kitanyang’anywa
ithibati.
“Zoezi la ukaguzi kwa vyuo
vya Ufundi ni endelevu, hivyo vyuo ni lazima vizingatie taratibu, kanuni
na sheria , na chuo ambacho hatakidhi vigezo kitanyang’anywa ithibati.
Kwa upande wake Mwenyekiti
wa baraza la Uongozi wa baraza la Taifa la Ufundi (NACTE), Prof. John Kondoro
amesema vyuo vilivyoshiriki ni zaidi ya 100 ambapo washiriki watapata fursa ya
kukuza ushirikiano miongoni mwao.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce
Ndalichako akisikiliza maelezo ya baadhi ya bidhaa zilizotengenezwa na wanafunzi kutoka
moja ya chuo kinachoshiriki katika maonesho ya kwanza ya Elimu ya Ufundi na
Mafunzo Jijini la Dodoma.
Prof.Kondoro amesema ndani
ya miaka miwili serikali imesaidia kuweza kukaguliwa kwa vyuo vyote 500 vya
ufundi vilivyopo nchini Jambo ambalo halikwahi kufanyika katika miaka ya nyuma.
Prof. Kandoro amesema
maonesho hayo ni jukwa la kukutanisha wadau, kutangaza na kuona namna watu
wanavyoweza kujiajiri na siyo kusubiria kuajiriwa.
Waziri wa Elimu, Sayannsi na Teknolojia Profesa Joyce
Ndalichako akipata maelezo kuhusu gari linalotumia gesi lililobuniwa na
wataalamu kutoka Chuo cha Ufundi Dar es Salaam (DIT) lililopo katika maonesho
ya kwanza ya Elimu ya Ufundi na Mafunzo yanayofanyika jiji la Dodoma.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
Zingatia: Mwanachama wa blogu hii tu ndiye anayeweza kuchapisha maoni.