Waziri wa
Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof. Joyce Ndalichako amekipongeza Chuo Kikuu Mzumbe kwa usimamizi
mzuri wa mradi wa ujenzi wa hosteli za wanafunzi unaoendelea Chuoni hapo.
Waziri
Ndalichako ametoa pongezi hizo Mkoani Morogoro wakati akikagua maendeleo ya
ujenzi wa hosteli za wanafunzi unaoendelea Chuoni hapo ambapo amesema
ameridhishwa na kasi na ubora wa majengo yanayojengwa
Waziri wa Elimu, Sayansi
na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akiongozana na Viongozi pamoja na
wakandarasi wa ujenzi wa mradi wa hosteli za wanafunzi unaoendelea katika Chuo
Kikuu Mzumbe wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya ujenzi huo.
Mradi huo unaogharimu
Shilingi bilioni 6.5 unahusisha ujenzi wa Majengo manne ya ghorofa ya hosteli
za wanafunzi ambayo yatachukua wanafunzi 1,024 kwa mara moja pindi
yatakapokamilika. Mradi huo pia unahusisha ujenzi wa nyumba za waangalizi
pamoja na maeneo ya kufulia na kuanikia nguo za wanafunzi.
Aidha,Waziri
Ndalichako ametoa pongezi kwa SUMA JKT kwa kutekeleza mradi huo kwa kasi na kwa
ubora huku akiwataka wakandarasi wengine wanaofanya kazi katika miradi
mbalimbali ya ujenzi ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kuiga mfano wa
SUMA JKT katika utendaji.
Waziri wa Elimu, Sayansi
na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akikaga baadhi ya majengo ya hosteli za wanafunzi
yanayoendelea kujengwa katika Chuo Kikuu Mzumbe. Mradi huo unafadhiliwa na
serikali.
Nae Makamu
Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Prof. Lughano Kusiluka ameishukuru Serikali ya Awamu
ya Tano kwa uwekezaji mkubwa uliofanyika katika kuboresha miundo mbinu ya Chuo
hicho katika Kampasi ya Mbeya na Kampasi Kuu Morogoro, akieleza kuwa uwekezaji
wa kiasi hicho kwa Chuo Kikuu Mzumbe haujafanyika kwa zaidi ya miaka 40.
Waziri wa Elimu, Sayansi
na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akikapata maelezo juu yamradi wa ujenzi wa
hoasteli za wanafunzi katika Chuo Kikuu Mzumbe .
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
Zingatia: Mwanachama wa blogu hii tu ndiye anayeweza kuchapisha maoni.