Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia
William Ole Nasha amesema Serikali
inatambua na kuthamini umuhimu wa
mtoto wa kitanzania na ndio maana imekuwa ikizifanyia kazi haki za msingi za
mtoto ili aweze kuishi katika mazingira mazuri ikiwa ni pamoja na kupata
elimu.
Naibu
Waziri Ole Nasha ameyasema hayo Jijini Dar es Salaam wakati wa maadhimisho ya Siku
ya Mtoto wa Afrika yaliyoandaiwa na Shirika
la Wanawake katika Sheria na Maendeleo Afrika (WiLDAF)
ambapo amesema watoto wanapaswa kulindwa na kuwezeshwa ili waweze kushiriki
katika fursa mbalimbali zilizopo kwenye
elimu.
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha akizungumza wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afirika yaliyofanyika Jijini Dar es Salaam Juni 20, 2019. |
Ole Nasha amezitaja jitihada hizo kuwa ni pamoja
na kuridhiwa kwa mikataba mbalimbali ya Kimataifa inayolinda haki za watoto, kutunga sheria zinazolinda haki za watoto dhidi ya
uonevu na ubaguzi wowote na pia imepitisha Sera zinazowalinda na kuwapatia
fursa watoto.
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha akichangia mjadala wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika yaliyofanyika jijini Dar es Salaam. |
Jitihada nyingine ni
pamoja na ujenzi wa shule karibu na makazi ya watu ili kupunguza watoto
kutembea umbali mrefu, ujenzi wa mabweni na pia mafunzo mbalimbali ikiwa
ni pamoja na kuweka mkazo juu ya stadi za maisha, elimu ya afya ya uzazi na
ujinsia katika shule za msingi na sekondari na vyuo vya ualimu.
Katika hatua nyingine Naibu Waziri Ole Nasha ameutaka umma kutambua
kuwa jukumu la kuwaendeleza watoto kielimu ni la kila mmoja wetu na kwamba
ifahamike kuwa watoto wa kike na wa kiume wote ni sawa, hivyo hatuna budi kuwapunguzia
watoto wa kike mzigo wa kazi za nyumbani ili wapate muda wa kujisomea sawa na
ilivyo kwa watoto wa kiume.
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha akipokea risala kutoka kwa mmoja wa watoto walioshiriki Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika Jijini Dar es Salaam. |
Siku ya Mtoto wa Afrika huadhimishwa Juni 16 ya
kila mwaka ambapo kwa mwaka 2019 maadhimisho hayo Kitaifa yamefanyika Mkoani
Geita na yalikuwa na Kauli Mbiu isemayo “Mtoto
ni Msingi wa Taifa Endelevu: Tumtunze, Tumlinde na Kumuendeleza.”
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
Zingatia: Mwanachama wa blogu hii tu ndiye anayeweza kuchapisha maoni.