Wanafunzi wa kike nchini
wametakiwa kushiriki kikamilifu katika michezo ili kuimarisha afya ya akili
katika masomo na kuepuka vishawishi vinavyoweza kuharibu ndoto zao.
Kauli hiyo imetolewa na
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako wakati wa bonanza la mpira wa miguu maarufu
kama MIRIAM CUP lililoshirikisha wanafunzi wa kike kutoka shule za msingi, secondari,
vyuo vya ualimu na vile vya Maendeleo ya wananchi lililofanyika wilayani
Kasulu, mkoani Kigoma.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako akikabidhi kombe wa wanachuo wa Chuo cha Ualimu Kasulu kilichopo Wilaya ya Kasulu Mkoani Kigoma baada ya kuibuka kidedea katika mechi zilizoshindanisha wanafunzi wa kike kutoka shule za Msingi, Sekondari, Vyuo vya Ualimu na vile vya Maendeleo ya wananchi vilivyopo katika Halmashauri ya Kasulu.
Waziri Ndalichako
amesema lengo la bonanza hilo ni kutoa
hamasa kwa watoto wa kike kujiepusha na mimba za utotoni na kuwa michezo ikitumika vizuri ina nafasi
kubwa ya kumkomboa mtoto wa kike kielimu.
'' Michezo inachangamsha
akili, michezo inajenga afya iliyobora lakini pia michezo ni ajira na inaondoa
vishawishi,” alisisitiza Waziri Ndalichako.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako akisalimiana na wanafunzi wa kike ambao wameshiriki bonanza la mpira wa miguu almaarufu MIRIAM CUP lililoandaliwa na mdau wa Elimu Miriam Ntakisivya kwa lengo la kuhamasisha wanafunzi wa kike kukataa mimba za utotoni na kuendelea na masomo.
Waziri Ndalichako amempongeza muandaaji wa
bonanza hilo ambaye ni Mdau wa Elimu Miriam Ntakisivya na kusema kuwa bonanza
hilo liwe endelevu ili kuleta hamasa kwa wanafunzi wa kike mkoani Kigoma
kufanya vizuri katika masomo na kupunguza mimba za utotoni.
Kwa upande wake Mkuu wa
Wilaya ya Kasulu Kanali Simon Anange amesema wilaya hiyo kwa miaka mitatu
mfululizo kuanzia mwaka 2016 kumekuwa na ufaulu mdogo kwa wanafunzi wa kike
wanaomaliza kidato cha nne, hivyo bonanza hilo limewaleta pamoja wazazi, walimu
na jumuiya nzima ya Kasulukwa lengo la kukumbushana umuhimu wa kuwapa nafasi
watotowa kike kwenye masomo.
Wanafunzi wa kike walioshiriki bonanza la mpira wa miguu wakicheza mpira katika kiwanja cha mpira kilichopo Wilaya ya Kasulu Mkoani Kigoma.
Naye muandaaji wa Bonanza
hilo Miriam Ntakisivya amesema ameamua kuanzisha bonanza hilo baada ya kuona
watoto wa kike mkoani humo
wanashawishiwa na vitu vidogo na kuacha shule wakiwa na umri mdogo na
hivyo kuamua kuwaleta pamoja kukataa vitendo hivyo kupitia michezo.
Bonanza hilo limeshirikisha
timu za wasichana nane kutoka wilaya ya Kasulu na mechi kubwa iliyohusisha timu za watani wa jadi Kasulu United FC na
Bodaboda FC.
Muandaaji wa Bonanza la mpira wa miguu kwa wanafunzi wa kike katika wilaya ya Kasulu Miriam Ntakisivya akimpa cheti cha shukrani Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako
Muandaaji wa Bonanza la mpira wa miguu kwa wanafunzi wa kike katika wilaya ya Kasulu Miriam Ntakisivya akimpa cheti cha shukrani Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako