Ijumaa, 13 Oktoba 2017
Jumatano, 11 Oktoba 2017
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa Dkt. Hussein Mwinyi wampokea Mtukufu Agha Khan
Mtukufu Aga khan muda mfupi
Mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa jijini Dar es Salama
na amepokelewa na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce
Ndalichako pamoja na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa Dkt. Hussein Mwinyi.
Mtukufu Aga Khan akikagua
gwaride lililoandaliwa kwa ajili yake muda mfupi baada ya kuwasili katika
uwanja wa ndege wa Kimataifa jijini Dar es salaam.
Waziri wa Elimu, Sayansi na
Teknolonia Profesa Joyce Ndalichako, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa
Dkt. Hussein Mwinyi wakiwa katika picha ya pamoja na Mtukufu Aga Khan
ambaye amewasili leo.
Jumanne, 10 Oktoba 2017
Mradi wa TEHAMA wazinduliwa Mkoani Pwani
Katibu Mkuu Wizara ya
Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Leonard Akwilapo amezindua mradi wenye
thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 4
wa ujifunzaji na ufundiashaji wa TEHAMA kwa shule za Sekondari.
Akizindua mradi huo
mkoani Pwani hii leo Dkt. Akwilapo amsema Serikali inahitaji kuona mradi huu
unakuwa endelevu na usiishie katika mkoa
wa Pwani pekee bali usambae kwa nchi nzima.
Pia amewataka
waratibu wa mradi huo - gesci -
kuhakikisha mpango huu unafanikiwa kwa kushirikisha wadau wote wa Elimu ili mradi ufanikiwe.
Dkt. Akwilapo amesema
TEHAMA ni nyenzo muhimu katika ulimwengu wa mawasiliano, na kwa sasa ndiyo
nyenzo kuu ya utoaji na usambazaji wa taarifa kwa umma.
Katibu Mkuu Akwilapo
amewataka wale wote wenye miradi au mipango ya namna hiyo wawasiliane na wizara
ili miradi yao iweze kuratibiwa na
kutekelezwa kwa taratibu za Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.
Mradi huo
unatekelezwa katika baadhi ya nchi za Afrika ikiwemo Tanzania, Kenya, na
Cotedvoire
Jumatatu, 9 Oktoba 2017
VIONGOZI WA WIZARA YA ELIMU,SAYANSI NA TEKNOLOJIA WAAHIDI KUFANYA KAZI KWA USHIRIKIANO
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako amesema kuwa kitendo cha Rais John Magufuli kumbakisha kwenye Wizara hiyo ni sawa na kumchagua upya, hivyo ameahidi kufanya kazi kwa bidii.
Waziri Ndalichako amesema hayo wakati akimkaribisha Naibu waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha ambaye ameapishwa leo kuitumikia Wizara hiyo.
Wakati akizungunza na Watumishi wa Wizara hiyo Naibu Waziri Ole Nasha amesema katika utumishi wake anaamini katika mambo manne ambayo ni uadilifu na uaminifu, kufanya kazi kwa bidii, ubunifu na ushirikiano ili kutimiza malengo ya Kitaifa.
Alhamisi, 5 Oktoba 2017
Waziri Ndalichako azindua Bodi ya Wakurugenzi HESLB na Baraza la TET
Waziri wa Elimu, Sayansi na
Teknnolojia Prof. Joyce Ndalichako amelitaka Baraza la Taasisi ya Elimu Tanzania na Bodi ya
wakurugenzi ya Bodi ya mikopo ya Wanafunzi
wa elimu ya juu kufanya kazi kwa kufuata kanuni, sheria na taratibu za
kazi.
Waziri Ndalichako ameyasema
hayo leo jijini Dar es salaam wakati wa uzinduzi wa bodi hizo ambapo amezitaka
pia kuhakiksha zinarudisha hadhi ya Taasisi
za serikali wanazozisimamia katika kutoa huduma kwa wananchi kwa kuweka
miongozo ya utendaji kazi na kuhakikisha wanaisimamia miongozo hiyo ili kuleta
ufanisi katika kazi.
Ndalichako amezitaka bodi
hizo kuhakikisha zinatembea katika ahadi za Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli za kuhakikisha zinawasaidia wanyonge
kupata Elimu bora.
Waziri Ndalichacho amelitaka
Baraza la Taasisi ya Elimu Tanzania kuhakikisha vitabu vyote vyenye makosa vinarekebishwa
na kwamba bodi ijiridhishe na mfumo na utaratibu utakaotumika katika kuvirekebisha vitabu
hivyo.
Baraza hili ambalo
litahudumu kwa miaka mine (4) kuanzaia septemba 2017 hadi septemba 2021
limetakiwa pia kusimamia Kitengo cha Mawasiliano kwa Umma vizuri kwa sababu
kumekuwa na upotoshaji kuhusiana na Taasisi lakini pia amewataka kuhakikisha
kunakuwa na vipindi vya kuelimisha namna Taasisi inavyotekeleza majukumu
yake.
Kwa upande wake Mwenyekiti
wa Baraza la Taasisi ya Elimu Tanzania Profesa Bernadetta Kilian amesema
atahakikisha Taasisi inatekeleza majukumu yake kwa mujibu wa sheria na kwamba
maelekezo yote yaliyotolewa yatafanyiwa kazi ili kukidhi matarajio ya
watanzania.
Jumanne, 26 Septemba 2017
MBINU ZA KUFUNDISHIA ZIMEPUNGUZA UTORO - KKK MKOANI SINGIDA
Walimu wanaofundisha
darasa la awali hadi la tatu katika shule ya msingi Nyerere, Mughanga na shule
ya wanafunzi wenye mahitaji Maalumu Ikungi zote zilizopo mkoani Singida
wameeleza kuwa mbinu za kuimba, kucheza, kujifunza kwa kushirikisha
wanafunzi zinawasaidia wanafunzi kuelewa kwa haraka pamoja na kuwa na umahiri
wa kusoma na kuandika na kuhesabu.
Akizungumza na timu ya
wanahabari walio katika ziara ya kufuatilia hali ya ufundishaji na ujifunzaji
wa KKK na kuangalia hali ya uboreshaji wa miundombinu mkoani humo Mwalimu
Salome Kyomo amepongeza jitihada za serikali za kuwapatia walimu mafunzo ya KKK
kwa kuwa mbinu na zana za kufundishia zimeboreshwa.
Kwa upande wake
mratibu wa taaluma wa shule ya msingi Nyerere Lisu Mnyambi amesema shule
hiyo ilipokea kiasi cha shilingi Milioni 192 kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na
Teknolojia kupitia Programu ya Lipa kulingana na matokeo. ambazo zimetumika
kujenga vyumba vya madarasa 8, ujenzi wa matundu ya vyoo na hivyo kupunguza
msongamano wa wanafunzi madarasani.
Walimu wa shule ya
Msingi Mughanga mkoani Singida wakiwa kwenye moja ya darasa la Pili
ambalo mbinu mbalimbali za kujifunzia na kufundishia , (KKK) zipo katika darasa
hilo.
Baadhi ya vyumba vya
madarasa katika shule ya msingi Nyerere iliyopo mkoani Singida ambayo imejengwa
na fedha zilizotolewa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kupitia
Program ya lipa kulingana na Matokeo, (P4R)
Mwanafunzi wa darasa
la Pili katika Shule ya Endeberg iliyopo Manyara vijijini akisoma kile
kilichoandaliwa na Mwalimu wake huku wanafunzi wengine wakimsikiliza. Lengo la
Mwalimu hapo ni kujua wanafunzi wake wanaelewa kile alichowafundisha.
KKK NA UBORESHAJI MIUNDOMBINU GEITA
Mkuu wa mkoa wa Geita
Meja Jenerali Ezekiel Kyunga amesema ujenzi na uboreshaji wa miundombinu
unaotekelezwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kupitia programu
ya Lipa kulingana na Matokeo ( P4R ) umepunguza changamoto ya uhaba wa madarasa
uliokuwa unaukabili mkoa huo kutokana na kuwepo kwa mwitikio mkubwa wa wazazi
wa kuandikisha watoto kujiunga na darasa la kwanza.
Kyunga amesema mkoa
huo ulipatiwa kiasi cha shilingi milioni 194 kutoka Programu ya P4R ambazo
zimejenga madarasa Nane, kuweka umeme shuleni hapo na uchimbaji wa
kisimana hivyo kutatua changamoto ya upatikanaji wa maji.
Shule za msingi
zilizotembelewa ni pamoja na Nguzombili, Kalangalala ambazo zina
madarasa ya awali mpk darasa la tatu, (madarasa yanayoongea)pamoja na kituo cha
wanafunzi wenye mahitaji maalumu kilichopo kwenye shule ya Mbugani.
Mwanafunzi wa
darasa la kwanza wa Shule ya msingi kalangalala iliyopo mkoani Geita
akisoma ubaoni mbele ya wanafunzi wenzako pale alipotakiwa kufanya hivyo na
Mwalimu wake. Hii ni kufuatia ziara ya Maafisa wa kitengo cha mawasiliano
Wizarani pamoja na wanahabari ambao wanafuatilia ujifunzaji na ufundishaji wa
KKK.
Moja ya darasa
linaloongea lililopo kalangalala, mkoani Geita ambalo hutumiwa na wanafunzi wa
awali shuleni hapo. Kuanzishwa kw mtaala wa KKK kumewafanya wanafunzi kupenda
shule, imesaidia kupunguza utoro kwa wanafunzi na pia imechangia ufaulu wa
wanafunzi.
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)