Mkuu wa mkoa wa Geita
Meja Jenerali Ezekiel Kyunga amesema ujenzi na uboreshaji wa miundombinu
unaotekelezwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kupitia programu
ya Lipa kulingana na Matokeo ( P4R ) umepunguza changamoto ya uhaba wa madarasa
uliokuwa unaukabili mkoa huo kutokana na kuwepo kwa mwitikio mkubwa wa wazazi
wa kuandikisha watoto kujiunga na darasa la kwanza.
Kyunga amesema mkoa
huo ulipatiwa kiasi cha shilingi milioni 194 kutoka Programu ya P4R ambazo
zimejenga madarasa Nane, kuweka umeme shuleni hapo na uchimbaji wa
kisimana hivyo kutatua changamoto ya upatikanaji wa maji.
Shule za msingi
zilizotembelewa ni pamoja na Nguzombili, Kalangalala ambazo zina
madarasa ya awali mpk darasa la tatu, (madarasa yanayoongea)pamoja na kituo cha
wanafunzi wenye mahitaji maalumu kilichopo kwenye shule ya Mbugani.
Mwanafunzi wa
darasa la kwanza wa Shule ya msingi kalangalala iliyopo mkoani Geita
akisoma ubaoni mbele ya wanafunzi wenzako pale alipotakiwa kufanya hivyo na
Mwalimu wake. Hii ni kufuatia ziara ya Maafisa wa kitengo cha mawasiliano
Wizarani pamoja na wanahabari ambao wanafuatilia ujifunzaji na ufundishaji wa
KKK.
Moja ya darasa
linaloongea lililopo kalangalala, mkoani Geita ambalo hutumiwa na wanafunzi wa
awali shuleni hapo. Kuanzishwa kw mtaala wa KKK kumewafanya wanafunzi kupenda
shule, imesaidia kupunguza utoro kwa wanafunzi na pia imechangia ufaulu wa
wanafunzi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
Zingatia: Mwanachama wa blogu hii tu ndiye anayeweza kuchapisha maoni.