Katibu
Mkuu wa Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Dk. Leonard Akwilapo leo
amefungua mafunzo yanayoelekeza matumizi ya Force Akaunti kwa Wakuu wa Vyuo
vya Maendeleo ya Jamii- FDCs mkoani
Morogoro na kusisitiza kuwa utaratibu huo umekuwa na thamani ya matumizi ya
fedha, (value for money).
Akizungumza
na Wakuu wa Vyuo, Wakufunzi, Maafisa Ugavi na Wahasibu kutoka Vyuo hivyo Katibu
Mkuu Akwilapo amesema lengo ni kuwajengea uelewa wa namna ya kusimamia
ukarabati ili kuhakikisha Vyuo na Wizara kwa pamoja vinapata thamani ya
matumizi ya fedha.
Dk.
Akwilapo ameeleza kuwa Force Akaunti ni
utaratibu wa manunuzi ya huduma unaotambulika Serikalini na umekuwa ukitumia
sehemu kubwa ya bajeti yake katika ununuzi wa vifaa mbalimbali inayotumika
katika ujenzi.
Dk.
Akwilapo amesema lengo la kutumia
utaratibu huo ni kupunguza gharama za ujenzi na ukarabati pamoja na kufanya
utekelezaji wa mradi kukamilika kwa wakati, kukabiliana na dharura zinazohitaji kuchukuliwa hatua za
haraka pamoja na kuiwezesha taasisi husika kufanya kazi ya ujenzi na ukarabati
kwenye taasisi yake pale ambapo ujenzi ni shughuli za kila siku katika Taasisi
hiyo.
Ameongeza
kuwa Wizara ilitumia wataalam wake katika ujenzi na ukarabati ambapo fedha
iliyotumika kwa ajili ya kazi zilionekana kuwa kidogo.
"Kwa majaribio force Akaunti ilitumika
katika halmashauri 129 kujenga madarasa, mabweni, mabwalo, maabaara, Ofisi za
walimu, nyumba za walimu na umeonesha
mafanikio makubwa mahali ambapo kwa
kutumia mkandarasi wastani wa shilingi bilioni 2 hadi 3 zingetumika ila kwa
utaratibu wa Force Account Wizara imeweza kutumia shilingi milioni 800 hadi
bilioni 1 tu".alisema Dk.Akwilapo.
Kwa
upande wake mratibu wa mradi wa ESPJ Dk. Jonathan Mbwambo amewataka Washiriki
wa mafunzo hayo kuzingatia mafunzo na pia kutumia fedha watakazopewa za ujenzi
na ukarabati kama zilivyokusudiwa.
Kati
ya vyuo 55 vya FDCs vyuo 20 vitakarabatiwa na kujengwa katika awamu hii ya
kwanza ambapo upembuzi yakinifu unatarajiwa kuanza mapema wiki ijayo.
Mafunzo
hayo yameratibiwa na mradi wa kukuza stadi za kazi na ajira, ESPJ.